Model nyingi za baada ya 2003 ukifanya hili haziwaki kwa vile ni digitised au likiwaka basi litaleta shida punde tu. Halafu usifuate sana odometer mtu anaweza kukuuzia gari iliyopiga 50,000 ya ukweli lakini hakuna service wala maintanace iliyofanyika wakati unaweza pia kununua lenye 200,000 (hasa toka UK) lakini likawa limetunzwa vizuri. Hilo za la Dubai si kweli kwa kuwa Dubai hawaruhusu kuendesha used cars na pia wao wantumia upande wa kulia wa barabara na magari toka UK na Japan yanatumia kushoto
Magari nayajua vilivyo, lakini scientifically depreciation ya gari inategemea sana mileage, kwa jinsi nilivyo najua hiyo ni opinion ya mtu na sio fact. by the way magari mawili moja lina 50,000 na limetunzwa vizuri na jingine lina 200,000 na limetunzwa vizuri hayafanani. usiwe compromised na opinions unaponunua kitu cha gharama.
Kwa kusema baadhi modeli za 2003 and above haziwezi kuchezewa adometer automatically umekubali magari mengi below 2003 yanaweza kuchezewa adometer, Vile vile hiyo sio Fact kwa sababu inategemea ni gari gani mbona kuna benz za mwaka 1998 ziko digital kwelikweli na kuna gari za above 2004 tunazijua zilichezewa adometer.
Dubai ni kariakoo ya Uarabuni, Magari yale yanakua hayajatumika pale dubai ila yamepelekwa sokoni, kukuhakikishia nenda kwa waagizaji wengine wa magari waulize hii ishu. Take time kufanya utafiti " NO DATA NO RIGHT TO SPEAK"
Simshauri mtu kununua gari dogo lenye 100,000 and above, hayo mambo ya "lilikuwa well maintained" ni kuingizana mjini tu, wewe utajuaje wakati alokua mmiliki wake humjui.
After all mtu anae uza gari yard anatafuta faida kubwa, so lazima aweke cha juu 3,000,000 then anakula kiulaini.
Mfano hai, nilienda kuuliza yard zaidi ya tano bei ya Nissan Civillian jamaa wanaanzia 37,000,000 and above nakumbuka alikubali kunipunguzia laki mbili tu. Lakini nimeagiza gari hadi kodi kila kitu nimelipa 29,000,000. Na nimepata gari nzuri.
Inategemea ni supplier gani anakuuzia kule japan, kuna upuuzi mwingi ambao kama sio mzoefu sikushauri kabisa kuagiza gari nje coz unakua huajaliona physically. Unapokuwa na supplier wa kuaminika kama niliye naye mimi
kununua gari yard ni gharama sana.