Mkuu si kweli unayosema. Kwenye tradecarview magari yaliyopopale tayari makampuni yake yameonyeshwa na baei za magari yao pia na si kwamba magari yanauzwa na tradecarview, wao ni mkusanyiko tu wa makampuni mengi yanayouza magari. Uzuri wa kwenye tradecarview kuna wigo mkubwa wa kuchagua magari tofauti na hiyo beforward.jp maana nimeangalia ni wachovu kwelikweli hawana Harrier ya kuanzia mwaka 2001 hata moja, Suzuki escudo ya kuanzia mwaka 2001 hakuna hata moja na pia hawaonyeshi mileage ya magari yao kitu ambacho ni hatari maana unaweza kununua gari lililokongoroka hasa. Kuna watu kadha wa kadha niliokaribu nao wamenunua kupitia tradecarview magari mazuri kabisa kwa bei nzuri.