Ushauri unatakikana kwa wazee wetu

Ushauri unatakikana kwa wazee wetu

Ni kweli mimi49 inawezekana kabisa mke kusoma ndani ya ndoa lakini kikubwa ni kuwa na mume muelewa. Kama mume si mulewa au maamuzi yake yanayumbishwa na ndugu, jamaa na marafiki basi mke kusoma ndani ya ndoa ni ngumu mno. Wengine waliokuwemo ndani ya ndoa hupata bahati na kupata scholarship nchi za nje kwa Masters na kama watafanya vizuri basi wataunganisha na PhD. Sasa ukute ndio wana watoto wadogo mume anaweza kutumia sababu ya kuwa na watoto wadogo kumkatalia mwenzie kujiendeleza kielimu kwa kudai watoto wanahitaji "mapenzi ya mama" na kama ndugu, jamaa na marafiki wanampa maneno ya kutomruhusu mwenzie na mume ni rahisi kuyumbishwa basi ndio imetoka hiyo, lakini mke akibahatika kuwa na mume muelewa atamwambia nenda mwenzangu kwani elimu yako si kwa manufaa yako tu bali pia kwa manufaa ya familia yetu. Watoto wadogo ndio lakini mie nitajitahidi sana kuona hawakosi mapenzi yangu kama baba.
Ni kweli kabisa uyasemyo BAK bila ushirikiano na msimamo kutoka kwa upande wa mume kuhusu hilo suala la elimu kutakuwa na utata!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
No sio hivo its ok unaweza soma ukiwa na familia ila umakini wako kwenye masomo utakua tofauti na asie na majukumu kama hayo..matatizo ya familia utayabeba hadi chuoni muda wa discussion huna may be hupati ruhusa au una mambo mengine unafanya...
bi shost yaani nakupa five..maanake ukiwa na mtoto na majukumu kichwa kinakuwa na mambo mengi(overloaded) unakuwa huna nafasi kama mtu ambae anasoma bila majukumu...mara sijui mtoto aumwe...mara sijui huna wa kumtazama ilimradi tafrani!
 
Mie nilisoma na wanawake walioolewa, dah walikuwa makini na wanafaulu sana.
 
Mie nilisoma na wanawake walioolewa, dah walikuwa makini na wanafaulu sana.
ha ha ha sawa nimekusikia...lazima wafanye juhudi zote...waipe elimu 150% kwasababu circumstances ngumu kwahio muhimu wawe focused!!
 
Dunia ya leo elimu ni muhimu sana. Binti akiwa na elimu ya kutosha ya kumuwezesha kupata mahitaji yake muhimu basi si rahisi kunyanyaswa na mume lakini akiwa ni golikipa na mume mnyanyasaji basi itakula kwake na ndoa ataiona chungu sana.

Ni kweli kabisa uyasemyo BAK bila ushirikiano na msimamo kutoka kwa upande wa mume kuhusu hilo suala la elimu kutakuwa na utata!
 
Nadhani kusoma ukiwa na majukumu ya ndoa inakua ngumu kidogo...thats why wanaamua wamalize kwanza kusoma then hiyo hatua nyengine ifuate..
Hakuna mzazi anaetaka mwanae akose stara (ndoa) aendelee kutanga tanga na ulimwengu ila tu kwanza wana focus na dreams za watoto wao..
Wanaume wenyewe wa siku hizi ukiwa golikipa wakunyanyase wee mpaka...

Very true how can someone serve two masters at the same time?Let those tasks be done sequentially!KWani kusoma ni muda gani adi ushindwe kumsubiri.
 
Dunia ya leo elimu ni muhimu sana. Binti akiwa na elimu ya kutosha ya kumuwezesha kupata mahitaji yake muhimu basi si rahisi kunyanyaswa na mume lakini akiwa ni golikipa na mume mnyanyasaji basi itakula kwake na ndoa ataiona chungu sana.
Elimu inamfanya mwanamke awe independent na anakuwa anajua kujenga hoja na kuzitetea...."FREEDOM TO SPEAK"
 
Kwa baadhi ya wanaume hiki wanakiona ni kiburi, kumbe siyo hivyo kabisa.

Elimu inamfanya mwanamke awe independent na anakuwa anajua kujenga hoja na kuzitetea...."FREEDOM TO SPEAK"
 
Mentor mwanamke ataka mume ila wazee wamegoma mpaka amalize chuo wakati umri unaenda nae atamani ndoa hataki kuwa na mahusiano nje bila ndoa

Amefika menopause kwani? Amalize tu shule kwa kweli...!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom