Ushauri unahitajika: Uchumba matatani...

Hapo kuna mengi ya kutafakari, hawa wazee wakati mwingine wanapotoka. Kuna mzee mmoja amekataa kumuozesha binti yake kwa visingizio kibao, mara tunda la kuvundika si sawa na la kuivia mtini akimaanisha hata kijana akikubali kubadili dhehebu bado asingefaa maana kijana ni mkatoliki na binti ni msabato. Sasa binti ana watoto 3 bado yupo kwa baba ake... watu wanajiuliza ni kweli dhehebu linaweza kusababisha yote haya au mzee ana agenda ya siri na binti yake?

Annina
 
Madhebu yana nafasi ndogo katika maisha ya mwamini.Kwa kuwa binti tayari mambo hot, wakabariki tu kokote.Ila swala la kusaini hilo aachane nalo.
Kumbuka maswala haya baba mkwe asilazimishe maana ni imani.Pasipo imani. Unaweza hata kuigiza!.
 
Mwambie jamaa akomae,kwani hawawezi kuitoa mimba ya miezi mitano,asipokuwa na msimamo sasa hivi hata kwenye ndoa yao watakuwa wanamuingilia sana!!
 
huyo baba kazidi kama ni mm kwavile nimempenda binti sharti la kwanza ningekubali ila nikishaoa babamkwe stop kunipangia nn cha kufanya na nn nisifanye kwani mtu atamwacha babae na ***** na kuambatana na mumewe huyo binti bado ajawaacha wa kwao ataukimwoa atakusumbua kwani kila utakacho mwambia lazima akasililize ushauri wa baba alafu atakwambia babakasema

Truly....ndio maana nilimwomba rafiki yangu anipe muda ili nimpatie ushauri wa kutosha. Kama ukiangalia vizuri utaona yule binti hayuko tayari kukaidi pre-conditions za baba yake; hivyo maana yake even in future hali itaendelea kuwa hivyo, sasa hilo pia ni tatizo!
 
Swala dogo.

Kukata mzizi wa fitina wote waachane na dini zote, wawe hawana dini, na ndugu yeyote atakaye wa mind waue undugu.

Kwanza mungu mwenyewe hayupo na ndugu wengine mzigo mtupu.Kama mtu anaweza kukumind katika maamuzi yako mweyewe kiasi hiki huyu si ndugu ila ni mkoloni anatak kuku control tu.

Kama wanataka kuishi bila complication ndiyo hivyo, ndoa kwa mkuu wa wilaya, mtoto habatizwi kwa moto wala maji, period.

Kwisha kazi, kata mzizi wa fitina, kaput.

To be frank, rafiki yangu ni church boy, most of your comments sidhani kama zitamfaa. Ila hii dossier yote nitampatia, off course with general conclusion. Na nionavyo mimi yule binti yuko very strategic; mimba yenyewe aliipata kipindi fulani alikuwa likizo akaamua kwenda kumsabai best na likizo ilipoisha tu na kitu kilikuwa tayari tumboni. Rafiki yangu ali-oppose hiyo long stay lakini binti aling'ang'ania, kumbe inawezekana alikuwa na yake.
 
Hapo kuna mengi ya kutafakari, hawa wazee wakati mwingine wanapotoka. Kuna mzee mmoja amekataa kumuozesha binti yake kwa visingizio kibao, mara tunda la kuvundika si sawa na la kuivia mtini akimaanisha hata kijana akikubali kubadili dhehebu bado asingefaa maana kijana ni mkatoliki na binti ni msabato. Sasa binti ana watoto 3 bado yupo kwa baba ake... watu wanajiuliza ni kweli dhehebu linaweza kusababisha yote haya au mzee ana agenda ya siri na binti yake?

Annina

yap....even my first reaction nilimwomba jamaa yangu asikubali ku-negotiate under pressure. Akae chini afikiri kila kitu kwa makini sana. Mtu mzima ambaye amekula chumvi nyingi anapokuwekea vikwazo visivyo na logic inabidi kujiuliza mara mbili mbili. Unajua kadri umri unavyoongezeka ndivyo tunatarajia uelewa nao kuongezeka, sasa yule unayetarajia kuwa ni muelewa anapokukwaza inabidi kufikiri sana.
 
........Huyu msichana hana msimamo, dhehebu sio kigezo kabisa hapa. Wangapi wameona madhehebu tofauti na bado ndoa zao ni paradiso ndogo hapa duniani. Kama kweli angekuwa na msimamo angemwambia ukweli baba yake kwamba atafunga ndoa kwenye dhehebu la huyo mwanaume na kuendelea na hilo dhehebu................mimi sioni kikwazo hapa, binti anatakiwa kuwa na msimamo kama kweli anampenda huyo kijana ili wafunge ndoa.
 
Well said..!
 
huyo baba naye anamatatizo ..kama wote ni wakristo kuna tatizo gani hapo?
na huyo baba hajui maandiko yasemayo mwanamke ataacha wazazi wake na ataambatana na mmewe nao watakuwa mwili mmoja
Swala la watoto ni juu ya Baba na mama kuamua wasali na sio babu yao
kaniuzi huyo baba mkwe ..Binti nae ka msimamo kake kako 50/50% Y

Jamani mambo haya yameshatokea sana, na watu wameyazungumzia sana. Lakini tukirejea yote hayo, kwa kuzingatia kuwa mapenzi ni ya watu wawili tu, na wao ndo wenye jukumu wa kulilinda na kulitetea penzi lao, wakiongozwa na kutiwanguvu na upendo thabiti uliojengeka kati yao, waliofanikiwa kupambana ni wale ambao walikuwa wanapendana kweli kweli. Kwani waliweza ku ignore mambo yote ambayo yalikuwa ni ya kuvunja uhusiano wao, na kuendelea na michakato yao ya kuishi pamoja.
Kitendo cha huyo dada kusema kuwa kama ikishindikana basi waachane, ni ishara tosha kuwa upendo wa huyo dada kwa huyu ndugu yetu ni wa mashaka sana. Na sidhani kama ni legible candidate wa kula kiapo cha kuishi na huyo jamaa siku zote za maisha yao na kuwa hakuna kitu cha kuwatenganisha isipokuwa kifo tu!!!!. kwani hata huyo bwana akikubali inaweza kutokea jambo lolote lile ambalo ni upendo wa huyo dada pekee ndo utakao determini whether hiyo ndoa iendelee au la, na kwa upendo duni alionao huyo dada bila shaka hiyo ndoa itavunjika tu.
Unaweza kuwa ni ushauri mgumu sana kuukubali huyu bwana, lakini tusije tukaharibu kwa kutoa ushauri utakao mfurahisha tu huyu bwana. Mimi nakushauri sitisha hilo zoezi kwanza na kuu evaluate upendo wa huyo dada kwako. Ukishadhibitisha kuwa kweli anakupenda, na hakuna kitu wala mtu (e.g Baba, mama, kaka, jirani n.k) anaeweza kuwatenganisha wawili nyie isipokuwa kifo, then anza tena mchakato. Ukiprove otherwise achana nae kuepusha potential frustrations ahead.

Tafakari, chukua hatua.
 
Hapa mambo yote yako mikononi mwa binti,akionesha msimamo wa kumsuport jamaa ndoa itakuwa lakini akiendelea na ninamuogopa baba hapo watakesha na jamaa asipokuwa makini babamkwe atakuwa anaendesha familia yake kwa remote control.Hivyo kuna kila sababu ya kujua msimamo wa binti ukoje.Kwa masharti hayo ya baba mkwe na kama binti nae atakuwa yupo upande wa babamkwe,to me to withdraw is an option.
 
Kitendo cha huyo dada kusema kuwa kama ikishindikana basi waachane, ni ishara tosha kuwa upendo wa huyo dada kwa huyu ndugu yetu ni wa mashaka sana. Na sidhani kama ni legible candidate wa kula kiapo cha kuishi na huyo jamaa siku zote za maisha yao na kuwa hakuna kitu cha kuwatenganisha isipokuwa kifo tu!!!!. kwani hata huyo bwana akikubali inaweza kutokea jambo lolote lile ambalo ni upendo wa huyo dada pekee ndo utakao determini whether hiyo ndoa iendelee au la, na kwa upendo duni alionao huyo dada bila shaka hiyo ndoa itavunjika tu.
Unaweza kuwa ni ushauri mgumu sana kuukubali huyu bwana, lakini tusije tukaharibu kwa kutoa ushauri utakao mfurahisha tu huyu bwana. Mimi nakushauri sitisha hilo zoezi kwanza na kuu evaluate upendo wa huyo dada kwako. Ukishadhibitisha kuwa kweli anakupenda, na hakuna kitu wala mtu (e.g Baba, mama, kaka, jirani n.k) anaeweza kuwatenganisha wawili nyie isipokuwa kifo, then anza tena mchakato. Ukiprove otherwise achana nae kuepusha potential frustrations ahead.

Tafakari, chukua hatua.

Ushauri mzito sana.......it was my first opinion to my friend! Nashukuru kwa mchango.....naimani hii dossier yote akiipata itamsadia kujua amesimama wapi!
 
Mwambie ambebe mchumba wake, mguu kwa mguu wende kwa baba yake amwonyeshe malezi ya dini aliyomlelea binti yake yamemfikisha wapi, kisha ampe muda huyo binti kwa hiyari yake aamue kuolewa na dini anayotaka. Kumlazimisha huku anamimba ataolewa na kinyongo, afu ndo wale wakipata PhD kwasababu anajua hata baba yake hahuifurahia hiyo ndoa anaishia na watoto. Binti awe na msimamo.
 
I got you...thanks!
 
Kwa kweli hili pia na mimi lilinishtua....! Kutokana na msimamo huo hata mshenga amerudi nyuma anataka kujitoa....manake baba mkwe msimamo wake uko hivyo na ameshamwambia mshenga asirudi kwake kama hawajakubaliana na hayo.
eeeeh! hapo kweli mambo mazito, anaweza kuingia kwenye matatizo makubwa, mi ningeshauri apate muda wa kutafakari zaidi jambo hili pamoja na huyo bibie, wazazi wengine bwana! anatema biti kwa mshenga khaah! subiri apate habari ya kuwa bintiye kamimbika kama hajawa mpole
 
Hapo sijaona udini wala udhehebu. Huyo dogo anataka kuoa mchawi ila hajui tu. Kusaini kiapo cha nini vile??? Hayo ndo madogoli live....welcome to withcraft society...ndo hao wanaogombea maiti.

We chukua mzigo....huyo dingi hafai kusikilizwa..hiyo ndoa haimuhusu kihivyo ..anavuka mipaka sasa ebo!!

hii si kitu ya juu juu
Bolded -
-kwa nini binti anakubaliana na baba yake?
-mimba ya miezi mitano baba wa binti hajang'aka?
- nasikia kuna koo na jamii zingine huwa kama zimelaanika hivi, unaoa lakini angalau nusu ya watoto unaodai ni wako, kiuhalisia si wako wanakuwa wa baba yake- na pengine ndiyo maana huyo baba anataka watoto wabatizwe katika dhehebu lake, kwani anajua pengine wengine watakuwa wake, huyo binti ana siri iliyofungwa kati yake na baba yake!

Jamaa yako aangalie pengine hata hiyo mimba si yake.

angekuwa mdogo wangu ningemwambia a-retreat! hapo kuna ushirikina. Mabinti wa siku hizi huo ujinga hawakubaliani nao. Kwanza it is not Biblical.
 
thanks mkuu....with respect!
 
Hii ni kali na nzito! Hivi huyo baba mkwe anauhakika gani wa kuishi na kuona hao wajukuu anaong'ang'ania? Ikitokea Mungu amemchukua (God forbid) ataweza kufurahia chochote anachopanga? Kwa nini kuwaingiza malaika hao (watoto) kwenye mikataba wasioijua?

Binafsi nashauri jamaa awe na msimamo na akatae hilo ombi la baba mkwe mapema. Napata wasiwasi akilegea mwanzoni, yatakuja maombi mengine ambayo huenda yakawa magumu zaidi! Msimamo wake utampa heshima hata kwao kuwa kijana wao atakua baba imara kwenye familia na si legelege.

Kitendo cha kumtisha mshenga pia ni cha kuangaliwa. KiAfrika mshenga ni mtu anayeheshimika na ni kiungo muhimu hata baada ya ndoa. Kama kiungo hicho kinaanza kukosa kupewa umuhimu wake upande mmoja kitakosa maana. Jambo hilo litakua hatari kwa ndoa yenu pia.

Mwisho nashauri huyu ndugu amuombe Mungu amtie nguvu kwani jambo hili ni zito hasa ukizingatia mapenzi aliyonayo kwa mchumba wake na hali ya mchumba wake. Huyu baba mkwe ambaye hata mshenga hamuheshimu anaweza kuwa tatizo baadae katika kusuluhisha matatizo ya ndoa ambayo ni kawaida kwa kila ndoa kuwepo
 
Thanks......with respect! Kwa kweli michango ni mingi na mizuri. Nitamkabidhi best full dossier...!
 
Back
Top Bottom