Ushauri unahitajika: Uchumba matatani... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri unahitajika: Uchumba matatani...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kwetunikwetu, Jan 19, 2010.

 1. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wakuu naomba mnichangie mawazo ya kumpatia ushauri muafaka rafiki yangu. Ni hivi, kuna jamaa ni rafiki yangu wa karibu sana (almost ndugu). Tumesaidiana kwa mambo mengi na kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka kama mitatu amekuwa na urafiki na msichana fulani, hatimaye kufikia uamuzi wa kujiweka tayari ili kufunga ndoa. Baada ya kujitambulisha kwenye pande zote mbili za familia, matatizo ndio yameanza kama ifuatavyo;

  1. Rafiki yangu na huyo mchumba wake ni wakristo ila madhehebu tofauti; wao wameamua kila mtu abaki na thehebu lake ila ndoa ifungwe kwenye dhehebu la mwanamume. Lakini baba wa huyo binti amekataa katakata anataka ndoa ifungwe kwenye dhehebu la binti yake.

  2. Pili, baba wa huyo binti amemtaka rafiki yangu asaini kiapo kuwa watoto wao watabatizwa na kulelewa kiroho kwenye dhehebu la binti yake (ie dhehebu la huyo baba mkwe).

  3. Jamaa yangu alimpomweleza huyo binti kuwa masharti hayo ni magumu sana kwake, na hivyo kumtaka binti atoe msimamo wake, binti alimwambia kama itashindikana basi waachane.
  4. Kwa sasa binti huyo ni mjamzito wa kama miezi mitano hivi, habari hiyo bado haijamfikia huyo baba mkwe.

  Sasa basi, nilipomuuliza rafiki yangu anieleze msimamo wake....alinijibu kuwa mpaka sasa hajui afanye nini. Nilimuomba anipe wiki moja nijaribu kutafakari kwa vile nisingeweza kukurupuka ukizingatia uzito wa suala lenyewe.

  Wadau naomba mistari ili niweze kutoa ushauri muafaka
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hao waoane tuu maana hawafuati dini yayote kwa sababu wameshatungana hadi mimba kuonesha kuwa ni asharati wazoefu.
   
 3. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  duh eee kweli JF kiboko..! Nafikiri nitamuwekea link ya hii thread ili aone watu wanashauri nini
   
 4. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kuandikiana kiapo, huyo Mkwe kazidisha. Wajue kuwa MUNGU ni mmoja na hana dini.. ikibidi Jamaa yako akubali yaishe kwa sababu ameshamjaza! Ila kama ana imani hata wakiandika kiapo ni by the way hakuna litalompata.. Mpe pole sana.
   
 5. M

  MalaikaMweupe Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Aangalie sana,la sivyo baba mkwe atakuwa hadi anamuingilia kwenye kuiongoza familia hiyo baada ya ndoa.
   
 6. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Huu ndio unafiki ninaoupigia kelele kila siku, kuonekana mtakatifu mbele za watu kwa kwenda kanisani kila siku na kupigania dhehebu lako wakati hata Mungu mwenyewe humuogopi.

  Hivi dhehebu ndilo linalompeleka mtu peponi? Hapo kwenye mimba ndiyo starting point nzuri! Jamaa yeye akubali tu kufunga ndoa kwenye dhehebu la binti kwa kuwa dhehebu si kitu. Ila hilo la kusaini mkataba ni BIG NO! After all huwezi kuwachagulia watoto dhehebu kabla hawajazaliwa! Vipi baada ya kuzaliwa wakaaamua kubadili dini baada ya kuwa na umri wa miaka 18 na uhuru wa kuchagua wakitakacho huo mkataba utakuwa umesaidia nini?

  Inabidi tubadilike na kusoma zaidi kuhusu hizi dini na madhehebu. Ukiwa na uelewa mpana zaidi huwezi kufungwa na madhehebu. Hapa nazungumzia madhehebu ya kawaida, siyo yale yenye mambo ya ajabu ajabu!
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  huyo baba naye anamatatizo ..kama wote ni wakristo kuna tatizo gani hapo?
  na huyo baba hajui maandiko yasemayo mwanamke ataacha wazazi wake na ataambatana na mmewe nao watakuwa mwili mmoja
  Swala la watoto ni juu ya Baba na mama kuamua wasali na sio babu yao
  kaniuzi huyo baba mkwe ..Binti nae ka msimamo kake kako 50/50% Y
   
 8. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hapo sijaona udini wala udhehebu. Huyo dogo anataka kuoa mchawi ila hajui tu. Kusaini kiapo cha nini vile??? Hayo ndo madogoli live....welcome to withcraft society...ndo hao wanaogombea maiti.

  We chukua mzigo....huyo dingi hafai kusikilizwa..hiyo ndoa haimuhusu kihivyo ..anavuka mipaka sasa ebo!!
   
 9. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mmmmmh~! Hilo nalo neno, unaweza ukadhani ni msimamo wa dhehebu kumbe kuna mambo ya kafara yamejificha! Watoto wataisiniwaje mkataba kabla hata hawajazaliwa? :)
   
 10. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli hili pia na mimi lilinishtua....! Kutokana na msimamo huo hata mshenga amerudi nyuma anataka kujitoa....manake baba mkwe msimamo wake uko hivyo na ameshamwambia mshenga asirudi kwake kama hawajakubaliana na hayo.
   
 11. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  truly...!
   
 12. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Na ndio maana anaonekana ''mtakatifu'' kumbe tayari anakwenda ''nyama kwa nyama''.

  Njia rahisi ni kumwambia huyo baba mkwe kwamba binti yake tayari ni mjamzito. Atalainika kama mrenda na ndoa itafungwa chap chap ili afiche aibu ya binti yake huko kanisani kwao!
   
 13. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  yeah....nimekupata mkuu
   
 14. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nilighafilika ikabidi nimuulize rafiki yangu hivi huyo binti anampenda kwa asilimia ngapi? Mbona inaonekana binti hana msimamo? Nikaona nitazidi kumchanganya jamaa...bora nivute subira ili nitoe ushauri mzuri usio na jazba
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kweli masaki yaani dingi akigundua binti mjamzito atatamani hata aende bure siku hiyo hiyo ;)
   
 16. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mmmhh
   
 17. B

  BeNoir Member

  #17
  Jan 19, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na mfumo dume kuwa watoto ni wa baba, jambo ambalo naamini ndio alivyokuzwa huyo rafiki yako. Lakini je, kuna maelezo au sababu zo zote alizotoa binti ni kwanini mzazi wake anataka mambo yawe hivyo? Ndoa ifungwe kwenye dhehebu la binti na watoto wafuate hivyo?
  Je, huko nyuma hilo mlilijadili namna gani? Watoto wangekuwa dhehebu gani?
  Na binafsi yako utakuwa umepungukiwa nini endapo watoto watakuwa dhehebu la huyo mwenzako?
   
 18. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu niliuliza mambo mengi sana! Rafiki yangu alinieleza kuwa suala la ndoa walikubaliana ifungwe kwenye dhehebu la mwanaume; ila kuhusu watoto hilo hawakuwahi kuliongelea
   
 19. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  huyo baba kazidi kama ni mm kwavile nimempenda binti sharti la kwanza ningekubali ila nikishaoa babamkwe stop kunipangia nn cha kufanya na nn nisifanye kwani mtu atamwacha babae na mamae na kuambatana na mumewe huyo binti bado ajawaacha wa kwao ataukimwoa atakusumbua kwani kila utakacho mwambia lazima akasililize ushauri wa baba alafu atakwambia babakasema
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Swala dogo.

  Kukata mzizi wa fitina wote waachane na dini zote, wawe hawana dini, na ndugu yeyote atakaye wa mind waue undugu.

  Kwanza mungu mwenyewe hayupo na ndugu wengine mzigo mtupu.Kama mtu anaweza kukumind katika maamuzi yako mweyewe kiasi hiki huyu si ndugu ila ni mkoloni anatak kuku control tu.

  Kama wanataka kuishi bila complication ndiyo hivyo, ndoa kwa mkuu wa wilaya, mtoto habatizwi kwa moto wala maji, period.

  Kwisha kazi, kata mzizi wa fitina, kaput.
   
Loading...