Ushauri: Tuvilinde vyeti vyetu halisi na ugomvi wa wapenzi wetu ni hatari

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
735
Jamani kwa wote wenye vyeti vya taaluma kuweni makini sana hasa pale ugomvi unapotokea na wapenzi wenu usihusike kwenye vyeti ili mkomoane.

Nimeyasema haya kwa sababu kipindi hiki ni rahisi sana mtu akitaka kukuharibia future yako kupitia kuviharibu vyeti vyako kwa maana ya kuvichoma, kuviharibu au kuviiba na kuvificha mbali na wewe ili tu akuharibie.

Matukio kama haya mara nyingi yanaweza kufanywa na watu wetu wa karibu sana hasa pale mtakapokuwa na ugomvi na mwenzako akataka akukomoe zaidi kwa kukuharibia kwa kuviiba vyeti vyako na kuvifanya vile atakavyo ona inafaa. Hivyo kuleta athari kubwa kwa aliye chukuliwa vyeti vyake ikiwemo kusimamishwa kazi pale atakaposhindwa kuvileta ili ahakikiwe au kama bado haja ajiriwa atapata shida sana ili aweze kuajiriwa hasa katika kipindi hiki cha rais wa awamu ya tano.

Mara nyingi tumekuwa tukiwaamini sana wapenzi wetu na tukawaacha huru kwa kujua kila kitu zikiwemo nyaraka zetu nyeti (vyeti) zinapohifadhiwa, sasa ni wakati muafaka pia wa kuwajua wapenzi wetu ikitokea tumekwazana mara nyingi hasira zao zina ishia wapi, ukiona anapenda sana kufanya vitu vya kukukomoa kama vile kuharibu baadhi ya vitu vyako unavyovipenda au vinavyokugusa moja kwa moja basi kuwa naye makini iko siku atakuharibia kwa kukuchukulia vyeti vyako ili akukomoe zaidi.

Mwisho niwaombe kuwa makini sana na vyeti vyenu vya taaluma kwani kwa sasa hizo nyaraka ni muhimu sana tena sana uwe na ajira au usiwe nayo ipo siku zitahitajika.
 
Hili sikuwahi kuliwaza kabisa kuna haja ya kuhifadhi nyaraka hizi kwenye vyombo salama
 
Kama ni halisi, si una report police unaenda kuchukua vingine tu. Wala hakuna haja ya kuwa na wasi wasi. Vyeti hupotea na kuungua na moto, unafuata process unapewa vingine.
 
Ni kweli ila kuhusu huo utaratibu ndugu sio rahis sana tena itokee uko pembezoni mwa nchi utasaga meno hadi uje uvipata... Kikubwa vitunze vizuri vyeti vyako
 
Back
Top Bottom