shangwe shangwe
Senior Member
- Oct 17, 2012
- 108
- 24
Wadau mnaofahamu hatua za kufuata ktk kupimisha ardhi mnijuze kwani nina ekali 6 za shamba nahitaji zipimwe. Kama mnafahamu gharama zake pia nijuzeni.
Wadau mnaofahamu hatua za kufuata ktk kupimisha ardhi mnijuze kwani nina ekali 6 za shamba nahitaji zipimwe. Kama mnafahamu gharama zake pia nijuzeni.
zipi? Hizo taratibu unazosema ndio zile zile ndo kaziulizia. Tusaidiane katika hili na mimi pia nahitaji kujua nina hekari 1 yangu mwasonga nataka niipime. msaada wenu mnaofahamu...Zipo wapi hizo ekari sita? Maana bei zina tofautiana mkoa na mkoa ila taratibu ni zilezile
Si ndo mambo hayo bana. Shukrani kwa info nimepata pa kuanzia sema kitu kimoja zaidi, je hiyo hatua ya nne inagharimu shilingi ngapi? au ni bure?Mkuu Mathematician
Mkuu kaulizia na gharama ndio maana nikauliza mahali zilipo sababu gharama ya upimaji ardhi ya Morogoro si sawa na ya Dar japo taratibu ni zilezile
Mwasonga unahitaji kwa ekari moja unahitaji 6.5 kupima unless kama hilo eneo lako lipo ndani ya town plan.
Hatua ya kwanza: kachukue coordinates za eneo,tafuta mtu mwenye GPS,surveyors au engineers wengi wanafanya hii.Gharama yake ni elfu 50 mpaka laki moja
Hatua ya pili: peleka coordinates wizara ya ardhi kucheki kama eneo lako lipo ndani ya town plan.
Hatua ya tatu:
3a)kama eneo lipo kwenye town plan kinachofuata ni kuanza taratibu za kulipima kwa kulichorea mchoro na kuligawa viwanja.Hii hufanywa na halmashauri ya mji husika ila kwa kigamboni inafanywa na KDA.Hii itagharimu kama 2M kwa kila ekari
3b) Au kama eneo halipo kwenye town plan basi inatakiwa liingizwe kwenye town plan,hii ni gharama sana,ina gharimu 4.5M(laki 5 ya kuchukua vipimo vinaitwa differential na 4M ni kupitisha mchoro ardhi),kwa uzoefu wangu wa kigamboni hii ndio gharama ambayo wahusika wengi wa wizara ya ardhi wamenipa.wakisha weka eneo kwenye town plan then hatua ya 3(a) hapo juu ndio inayofuata
Hatua ya nne: kufuatilia offer za viwanja katwa kama vipande na kuwekwa mawe kwenye eneo lako.Hili hufanyika kwenye halmashauri husika
Hatua ya tano: ukishapata offer unapewa barua na halmashauri husika halafu unaipeleka barua na offer wizarani kwa ajili ya kuanza mchakato wa kupata hati
Kwa kigamboni huu mchakato wote unafanyiwa KDA sio Temeke tena.
WADAU WENGINE WATANIREKEBISHA ,ILA HUO NDIO UFAHAMU WANGU NA MPAKA
SASA NDIO UTARATIBU NILIO
UFUATA KWA ENEO LANGU KIGAMBONI
Cc shangwe shangwe KIGAMBONI
Si ndo mambo hayo bana. Shukrani kwa info nimepata pa kuanzia sema kitu kimoja zaidi, je hiyo hatua ya nne inagharimu shilingi ngapi? au ni bure?
Si ndo mambo hayo bana. Shukrani kwa info nimepata pa kuanzia sema kitu kimoja zaidi, je hiyo hatua ya nne inagharimu shilingi ngapi? au ni bure?