Ushauri tafadhali

Ushauri tafadhali

chen

Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
64
Reaction score
7
ndugu zangu naomben busara zenu hapa.Mi bado ni kijana miaka 24 ndo naanza kujenga maisha yangu ila bado nipo kwa wazazi,nili mweleza mama yangu kuwa naomba niondoke nyumban nikajitegemee ila mama yangu kanikatalia na kaniambia nikiondoka ananiachia radhi yeye anachoitaji ni tuiboreshe nyumba na niendelee kukaa nyumban,kitu ambacho mi nakipinga kwan naona nikikaa home sipati changamoto za maisha.najua humu ndan wamo wapo baba zangu,mama,kaka na dada ni uamuzi gan mnao ona ni sahihi na wa busara niufanye
 
Muoneshe jinsi gani unahitaji kujifunza kujitegemea na kwamba utabaki member wa familia hata kama uko kwako.

Mwambie unahitaji akuamini kuwa utabehave na kujilinda (past records zako zitakusaidia).

Muhakikishie kuwa utaendelea kuwa nao ktk shida na raha (kama walikuwa wanakutegemea).

Kikubwa ni kumfanya azione points zako, so angalia mood yake, muda muafaka, tumia lunga nzuri na vitu kama hivyo; atakuelewa tu.
 
Mmmh boresha familia kwanza, kwani mama pia anakukatalia kwenda kutafuta hizo changamoto ukiwa nyumbani au unataka uhuru wa private life?
 
Mmmh boresha familia kwanza, kwani mama pia anakukatalia kwenda kutafuta hizo changamoto ukiwa nyumbani au unataka uhuru wa private life?
hapana sio uhuru wa private life, naomba nikuulize madame x we ulivyo anza life ulianza kujijenga au uliaza kuboresha familia yenu?
 
labda mama anaona "hujaota miguu" vizuri,je umewahi kusoma mbali na nyumbani?...,wewe ni mtoto wa kike au wa kiume?,je wazazi wana kipato kingine au wanakutegemea?una wadogo zako wanaokutegemea katika mahitaji ya kila siku?,unaruhusiwa kuchelewa kurudi,au ni sheria za nyumbani zinakusababisha uishi mwenyewe?ni nini unachoona utakifaidi zaidi ukiwa kwako kwa wakati huu,,,,kama utaweza kuyajibu haya maswali,ninaweza nikawa na straight solution nikusaidiaje kimawazo....naendelea kuufwatilia huu uzi
 
hapana sio uhuru wa private life, naomba nikuulize madame x we ulivyo anza life ulianza kujijenga au uliaza kuboresha familia yenu?

Unamaanisha kuboresha family au nyumba maana ni vitu viwili tofauti. Kama ni family please kaa kidogo kama ni nyumba unaweza fanya hata ukiwa haupo. Mimi niliondoka nyumba baada ya kuona nina kitita 🙂 cha kuweza kuanzisha maisha yangu, naweza sema kuishi nyumbani niliweza kusave ili niweze kukabiliana zaidi na maisha yangu.
 
nikijana wa kiume, nimekaa mbali na wazazi zaidi ya miaka 7 nikiwa nasoma,wazazi wangu wote wana kipato,hakuna mdogo wangu anae nitegemea,sina mda maalum wa kurudi nyumban ila natakiwa nitoe taarifa kama nitachelewa au km sirudi,faida inazoziona nikiondoka home ni kuacha kuwategemea wazazi,kupata changamoto za maisha
 
Unamaanisha kuboresha family au nyumba maana ni vitu viwili tofauti. Kama ni family please kaa kidogo kama ni nyumba unaweza fanya hata ukiwa haupo. Mimi niliondoka nyumba baada ya kuona nina kitita 🙂 cha kuweza kuanzisha maisha yangu, naweza sema kuishi nyumbani niliweza kusave ili niweze kukabiliana zaidi na maisha yangu.

kuboresha nyumba na nina uwezo wa kujitegemea kwani nimeajiriwa ktk kampun moja hapa mjin na nalipwa mshahara si mbaya sana
 
ndugu inaonekana wazazi wamekutengenezea pasonality ya utegemezi,,
unaenda kupata hizo changamoto za maisha wapi wazazi lazima wawe curious,
umri wako pia ni wa kawaida ila unahitaji kuprove kwa wazazi kwamba unapoondoka hawatabaki na wasi mh
pia una nini cha kwenda kuanzia maisha waoneshe ni zaidi ya elimu ulopata
unachofanya ukiwa nyumbani kitaakisi uwezo wako wa kujitegemea
 
jitegemee bana we shoka, utajuwaje majukumu yako pale utakapo itaji kubeba jiko. komaa kiume bana
 
hakuna mzazi anakubali ukajitegemee kirahisi.
 
Nakupa pongezi sana kwa kupata wazo la kuanza kujitegemea,hii ni hatua moja katika kujitambua,nakupongeza maana
::
Yeyote anaedhani kuwa bila baba,mama kaka au dada maisha hayawezekani,kila kitu kitaisha,labda atakufa kesho yake n.k Basi mtu huyo hajafikia ukomavu wa kiakili.
::
Kujitegemea unakotaka hakuna maana,utafute uhuru wa kufanya unayotaka mema kwa mabaya,la! Kuna maana uzingatie misingi ya maadili uliyofunzwa,linda maisha yako usisahau Kila mchuma janga hula na wa kwao.
::
Mambo ya msingi yatakayo kupa kibali cha kujitegemea au kuishi mbali na wazazi wako ni pamoja na KAZI HALALI inayojulikana,USALAMA wa maisha yako na MAWASILIANO ya uhakika kwa familia yako.Nadhani ukiwahakikishia kwa vitendo wazazi wako mambo hayo watakuwa radhi kukubalia.
::
Mwisho,usiogope maisha,wapo vijana wengi ambao unawazidi umri na maisha yao yana dira nzuri,wengine hawakupata bahati ya kuchungwa au kulelewa na wazazi wao(ni yatima) lakini wana maisha mazuri.Usiogope shida,,shida huleta maarifa..wakati ndio sasa,AMUA NI MAISHA YAKO.
=
 
hakuna radhi wala laana ya hivyo.
Je baba yako yupo,na amekwambia nini?
Kama hayupo kaa utunze mama yako.
 
hiyo hela ya kodi utakayoenda kulipa si bora ununue kiwanja????
 
ndugu zangu naomben busara zenu hapa.Mi bado ni kijana miaka 24 ndo naanza kujenga maisha yangu ila bado nipo kwa wazazi,nili mweleza mama yangu kuwa naomba niondoke nyumban nikajitegemee ila mama yangu kanikatalia na kaniambia nikiondoka ananiachia radhi yeye anachoitaji ni tuiboreshe nyumba na niendelee kukaa nyumban,kitu ambacho mi nakipinga kwan naona nikikaa home sipati changamoto za maisha.najua humu ndan wamo wapo baba zangu,mama,kaka na dada ni uamuzi gan mnao ona ni sahihi na wa busara niufanye

mueleze kuwa huwezi kuishi nae milele,unahitaji kuanza kujitegemea na kuface challenges directly.
 
Waulize wazazi wako wote, walianza kujitegemea au kuoa/olewa wakiwa na umri gani? Kama unauwezo wa kujitegemea na unajiamini, ondoka kwa nguvu kajitegemee, wazazi wako wanamaisha yao na wewe unamaisha yako, hilo swala la kukuzuia limepitwa na wakati ila ni hali tu ya wazazi kuwa too protective kwako. Umri wako ndiyo umri wa kuweka msingi imara wa maisha yako ya baadaye. Usipohama sasa baadaye utajuta.
 
hiyo hela ya kodi utakayoenda kulipa si bora ununue kiwanja????

eeeh! Kwa hiyo akiposa ndo anasaka nyumba wanahamia na mkewe kila mmoja katoka kwa mzazi? Hivi ulishaona mkaka akiudhiana na mkewe anachukua kibegi huyooooo kwa mamake? Nilishaona hii kituko aisee, kama comedy
 
ndugu zangu naomben busara zenu hapa.Mi bado ni kijana miaka 24 ndo naanza kujenga maisha yangu ila bado nipo kwa wazazi,nili mweleza mama yangu kuwa naomba niondoke nyumban nikajitegemee ila mama yangu kanikatalia na kaniambia nikiondoka ananiachia radhi yeye anachoitaji ni tuiboreshe nyumba na niendelee kukaa nyumban,kitu ambacho mi nakipinga kwan naona nikikaa home sipati changamoto za maisha.najua humu ndan wamo wapo baba zangu,mama,kaka na dada ni uamuzi gan mnao ona ni sahihi na wa busara niufanye
Your mother is a narcistic ,very controlling .Anza mbele
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom