Ushauri Tafadhali

Mimi sijaoa lakini nimesikitishwa na kitendo cha rafiki yangu mmoja ambae ana mchumba wake na wamekua ktk uchumba kwa karibia mwaka sasa, huyu rafiki yangu alishauriwa na mtu wake wa karibu ili amwoe huyo binti kwa sababu ni mchapa kazi na ni mwenye tabia nzuri piani mzuri wa sura (kwa mujibu wa jamaa) lakini jamaa anakuwa na mashaka kwani yule binti ni mfupi (short chasis lady) naye jamaa ni mfupi so anaona km wakioana wote wafupi haitakuwa imekaa vizuri na amefikia hatua ya kutaka kuuvunja uchumba huo ili atafute msichana mrefu kidogo wa kuoa. Ni kweli walikuwa na mgogoro kidogo ktk ucumba wao ila wamemaliza tofauti zao ila jamaa anasema tatizo ni UFUPI tu. Mie kwa ufahamu wangu nimemshauri asimwache huyo binti bali waoane lakini naona jamaa yangu anakuwa mgumu kunielewa....... Km ungekua wewe ungemshauri nini huyu kijana ambae anataka kuingia kwenye ndoa lakini ufupi unamfanya amwache mchumba wake?
Thanks


Siri ya mtungi aijuae kata.

Nadhani uchapakazi, tabia (unaijua ya nje yeye anajua ya ndani, vile vile tabia nzuri kwako si lazima nae aione nzuri) si vigezo ambavyo kila anayetaka kuoa lazima avizingatie. Tunatofautiana na tukubali kutofautiana.
 
Back
Top Bottom