Ushauri Tafadhali

Fmewa

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
292
81
Mimi sijaoa lakini nimesikitishwa na kitendo cha rafiki yangu mmoja ambae ana mchumba wake na wamekua ktk uchumba kwa karibia mwaka sasa, huyu rafiki yangu alishauriwa na mtu wake wa karibu ili amwoe huyo binti kwa sababu ni mchapa kazi na ni mwenye tabia nzuri piani mzuri wa sura (kwa mujibu wa jamaa) lakini jamaa anakuwa na mashaka kwani yule binti ni mfupi (short chasis lady) naye jamaa ni mfupi so anaona km wakioana wote wafupi haitakuwa imekaa vizuri na amefikia hatua ya kutaka kuuvunja uchumba huo ili atafute msichana mrefu kidogo wa kuoa. Ni kweli walikuwa na mgogoro kidogo ktk ucumba wao ila wamemaliza tofauti zao ila jamaa anasema tatizo ni UFUPI tu. Mie kwa ufahamu wangu nimemshauri asimwache huyo binti bali waoane lakini naona jamaa yangu anakuwa mgumu kunielewa....... Km ungekua wewe ungemshauri nini huyu kijana ambae anataka kuingia kwenye ndoa lakini ufupi unamfanya amwache mchumba wake?
Thanks
 
Hana akili jamaa! Looks kwake ndio kigezo kikubwa anaacha kuangalia vitu vya msingi??!! Akipata mke mzuri na mrefu kama PPF Tower halafu heshima=0,nidhamu=0,utulivu=0..hata akili ya kujenga maisha hana...atakuwa ndo kafanya nini..#Nonsense..
 
Duu hii kali.Kama mimi naoa tu mbona kuna dawa ya kumrefusha mtoto kipindi anabarehe.Bora mfupi mwenye akili ya maisha kuliko mrefu zezeta.
 
huyo zuzu labda kuna jambo anaficha kwa huyo binti sidhani kama ufupi ni sababu ya msingi
 
Siku zote hakuuona huo ufupi?
Mwambie arefuke yeye maana hata yeye atajamwagwa hivyo hivyo kwa ufupi wake.
 
Mpe pole coz akae akijua ni ngumu kwa mwanaume mfupi kupata mwanamke mrefu!zaidi ya hapo hajajitambua kwan uzuri wa mke ni inner luk na co out luk!nataman huyo dada ajue hiyo kitu amwage huyo jamaa ili apate mwanaume wa kumfaa maishan!vivulan vingine cjui vikoje,mbona huyo dada hakujali ufupi wa hicho kivulana!
 
Siku zote hakuuona huo ufupi?
Mwambie arefuke yeye maana hata yeye atajamwagwa hivyo hivyo kwa ufupi wake.
Hapa ndipo nimegunduwa uselfish wa wanaume, yaani yeye kauona ufupi wa mwenzanke, lakini ufupi wake yeye mwenyewe hauoni!! huu ni upumbavu wa kupindukia.
 
Hapa ndipo nimegunduwa uselfish wa wanaume, yaani yeye kauona ufupi wa mwenzanke, lakini ufupi wake yeye mwenyewe hauoni!! huu ni upumbavu wa kupindukia.
Kiujumla binadamu sie ni wabinafsi, sema wengine wamezidi kama huyu jamaa.Hana tofauti na wale wanaosema "nataka msichana mzuri, mwembamba" wakati yeye hana huo uzuri na mwili ni kama pipa.Wako tayari kutaka vitu ambavyo wao hawawezi kutoa. . .
 
Yeah guess na kina dada nao wangekuwa wanaweka masharti yao kwa wakaka si ingekuwa balaa? maana mdada angeanza na sifa za mwanaum
1. Awe na misuli
2. Awe na umbo sex
3. Awe mrefu wa wastani
4. Awe na usafiri
5. Asiwe na financial arrasment.
Imagine wadada nao wakikomaa na vigenzo hivi kutakuwa na mahusiano kweli?
 
Mbona wapo?
Sema bahati nzuri mdada akisema vigezo muhimu ni pesa, umbo na sura , ukiwa na pesa tu hayo mengine anajifanya haoni. Mi nadhani mtu akitaka kitu kwa mwenzie nae awe kwenye position ya kumpa mwenzie hicho kitu.Kama ni pesa nae awe nazo, kama ni sura na yake ilipe, kama ni umbo na lake liwe linaeleweka sio yeye kiuno hakijulikani kilipo alafu anataka dada mwenye umbo namba 8/kaka mwenye six pack.
 
Yeah guess na kina dada nao wangekuwa wanaweka masharti yao kwa wakaka si ingekuwa balaa? maana mdada angeanza na sifa za mwanaum
1. Awe na misuli
2. Awe na umbo sex
3. Awe mrefu wa wastani
4. Awe na usafiri
5. Asiwe na financial arrasment.
Imagine wadada nao wakikomaa na vigenzo hivi kutakuwa na mahusiano kweli?
wa2 siku iz wana vigezo vyao lol.
unioi 2 et ndoa , marriage with purpose ndio mpango mzima.
vigezo na masharti lazima vizingatiwe.
 
wa2 siku iz wana vigezo vyao lol.
unioi 2 et ndoa , marriage with purpose ndio mpango mzima.
vigezo na masharti lazima vizingatiwe.
Jidanganye tu kwenye huo umri ulionao, ngoja ukaribie 40 yrs tuone kama utaongea huo upuuzi wa marriage with purpose.
 
Mh ina maana huyu rafikio anatafuta mwanamke mrefu kumzidi yeye au mrefu kulinganisha na huyu alomwacha? Its unussual!
 
Natoa shukurani zangu kwenu nyote ndugu zangu ambao mmetoa maoni yenu. kwa kweli hatua ya huyu jamaa mimi mwenyewe imenishangaza na ni mtu wangu wa karibu ila naona kwa ameanza kunikwepa eti kwa sababu sijakubaliana nae ktk jambo hili yaani amebadilika. mimi nilihisi labda amepata binti mwingine nikamwambia kama amempata mwingine ambae anampenda zaidi ya huyu basi ni bora aseme kuliko kusema kuwa tatizo ni ufupi lakini akasema bado hajampata mwingine ila kila ninaposisitiza kuwa sababu ya ufupi si ya msingi jamaa anakasirika. Ila ninashukuru kwani hata ninyi ndugu zangu mmeliona hilo namimi nitaendelea kumwambia ukweli kwani yeye anadai kua binti ana sifa zote ila tatizo ni ufupi tu.............. duh. ukistaajabu ya Musa utayaona ya Moses.
Asanteni nyote ndugu zangu
 
Back
Top Bottom