Wenzangu mnadili navyo vipi? uzoefu tafadhali
Mkuu kwanza hongera kwa kuwa na watoto wa umri huo na pia pole kwa changamoto za malezi. Watoto huwa wasiri mno kwa asili na mara nyingi wanatabia za aina mbili yaani mbele ya wazazi wapo tofauti na wanapokua mbali na wazazi wanonyesha tabia tofauti. Mkuu nami ni mzazi na kwa bahati nzuri nimeanza kulea wadogo zangu na sasa wanangu zipo changamoto nyingi. Nakumbuka niliamini sana malezi niliyokua nawapa na mbinu nilizokua natumia kugundua tabia zao lkn kumbe kuna ambayo yalikua nje ya uwezo wangu kuyagundua. Kipindi hiki cha maendeleo ya teknojia ndio usiseme, Unaweza ukawakataza kumiliki simu lkn bado haisaidii kwani kuna wenzao watakua na simu watatumia au wao wenyewe watakuficha kama wanamiliki simu, hapo hujazungumzia vitu kama facebook na mengineyo.
Unachotakiwa kufanya ni kukaa nao na kuwaeleza athari za mitandao na za kuweka picha zisizo na staha kwenye mitandao hii waeleze kwa kina ili waelewe unamaanisha nini. Usiache kuwa wazi machoni pao jadilini kila kitu kwa uwazi ikiwezekana wape nafac watoe mawazo yao . Zungumza nao faida za mitandao hasa inapotumiwa vizuri na hasara zake . Waelimishe pia athari za kujiingiza kwenye mapenzi ktk umri mdogo na hasa ukikazia imani yenu bila kuacha kuzungumzia magonjwa, Ktk hili la mahusiano tumia muda wa mwingi kuongea nao .
Kuhusu nguo za ajabu hapo mkuu itakua ngumu mno kuwazuia ila usiache kuwakanya isipokua tegemea watafanya tu wakiwa mbali na nyumbani. Nakumbuka kijana wangu hapa huwa kila nikimbamba ananipa kiswahili na kuniweka sawa kama kwamba mie kipofu sioni. Usiwe mkali kupita kiasi au usiover restrict kila kitu kiwe kwa kiasi naamini kwa njia ya majadiliano mtakua sawa.
wapi hujaelewa mkuu? uliza nifafanue
maneno kama malavidavi, kusepa bana, hayo ni maneno ambayo hao unaoita wanao ndiyo wanapaswa kusema. inaonyesha wamefata nyayo zako mito
Karucee ushauri plz!! siyo unacheka tu na kusepa bana
maneno kama malavidavi, kusepa bana, hayo ni maneno ambayo hao unaoita wanao ndiyo wanapaswa kusema. inaonyesha wamefata nyayo zako mito
Mbona unaandika kama kijana wa leo huonekani kama ni mtu mzima ambaye anawatoto wakubwa Wa A level
Sina imani na 'Mshua' huyu.
Yeye ameomba watu wawe siriasi wakati mwenyewe hayupo hivyo.
Lugha uliyoitumia ina harufu na rangi ya Kijana, Sio mtu mwenye watoto wa kuwa ngazi uliyosema,
Pili, Umeulizwa umri wa watoto unasema mtu akadirie,
Kwani ingekugharimu kiasi gani kusema?
-Stop pretending.
Wakuu nina vijana wangu wawili, wa kike na wa kiume. Wote wako high school sasa. Kimasomo naona kama wanaenda vizuri ila kimaadili napata shaka kidogo hadi nimeamua kuomba muongozo kwa wadau wenzangu hapa.Wako shule tofauti na huwa nawasiliana nao kwa simu, call na texts.
Sasa mimi baba yao nilikuwa nyuma kidogo na hii technology ya whatsApp, simu yangu ilikuwa haisupport hii huduma halafu pia nilikuwa sina munkari nayo kivile. Sasa majuzi hapa nimenunua simu ya kisasa kuliko niliyokuwa nayo mwanzo ni hizi smartphone.
Sasa na mimi ndo sasa nikaamua kujiunga na haya ma-whatsApp. Katika kupekenyua huku na kule si nikaingia kwenye profile zao, daah. Vilivyoko huko sikutegemea kabisa, hayo maneno sasa ya malavidavi kwenye status zao, na yanavyobadilishwa kila siku, khaa nimechoka mwili na roho na hizo picha hivyo vivazi sasa ndo mimeishiwa nguvu kabisa, hata sijawahi waona wakivivaa nyumbani na hata sijui wanavipata wapi.
Kama mzazi najitahidi sana kuongea na wanangu, hadi huwa najipa imani kuwa wananielewa ila haya mambo yao ya kwenye mitandao ndo yamenipa mashaka sasa. Sijawauliza chochote hao watoto na wala hata wife sijamshirikisha. Nimeona nije kwanza kupata ushauri wenu kwa kunijibu mambo yafuatayo.
Je na wewe kama mzazi ulishawahi ona mambo kama hayo kwa vijana wako we uliyachukuliaje.Je haya ni mambo ya kawaida tu katika ulimwengu wa sasa hivyo niyapuuze,je nifanyeje mimi kama mzazi.
NB: Team kuponda tafadhali piteni tu huko pembeni, nitawashukuruni sana.
Pole ila naomba ku share na wewe Mimi kama mzazi huwa naongeaga ukweli na watoto wangu na wasifichi kitu kabisa na kitu kingine ni kwamba nimewaambia what I expect from them in terms Ya kuvaa kuongea na mambo Mengineyo nimeenda mbele zaidi na kuwapa masharti yangu kama mzazi mfano Kupata mimba au HATA kutoa mimba au kumpa msichana mimba na mambo mengine kama kutumia madawa Ya kulevya na MENGINEYO yaani wasitegemee kwamba eti atapata mimba Halafu Mie ntalea mjukuu au hata nikisikia ametoa mimba au eti katumia bangi au madawa Halafu Mie nianze hangaika Naye aache nimewaambia vyote nnavyotaka na nsivyotaka na adhabu zake. Kuongea na watoto ni muhimu ila naona kuna umuhimu sana wa kiset standards ntakuwa firm Kwenye adhabu
Aisee pole sana na changamoto za malezi. Hapa katikati nimepitia changamoto kibao na bado naendelea nazo. Kikubwa wewe mwenyewe kuwa karibu sana na Mungu halafu mkabidhi familia yako "mimi na nyumba yangu yutamtumikia Mungu". Pili waintroduce na wao kwenye kumtafuta Mungu sana. Tatu ukiweza zuia matumizi ya simu au wabadilishie wape nokia torch kwa ajili ya kupiga na texts tu. Lakini vyote hivyo vifanyike kwa dialogue ya hali ya juu nao ukiwaeleza faida na asala za utandawazi wa kidot com.Kaunga leo nimekuona hapa jukwaani, i want to hear something from you. Of course from others as well
Aisee pole sana na changamoto za malezi. Hapa katikati nimepitia changamoto kibao na bado naendelea nazo. Kikubwa wewe mwenyewe kuwa karibu sana na Mungu halafu mkabidhi familia yako "mimi na nyumba yangu yutamtumikia Mungu". Pili waintroduce na wao kwenye kumtafuta Mungu sana. Tatu ukiweza zuia matumizi ya simu au wabadilishie wape nokia torch kwa ajili ya kupiga na texts tu. Lakini vyote hivyo vifanyike kwa dialogue ya hali ya juu nao ukiwaeleza faida na asala za utandawazi wa kidot com.
Ni ngumu sana lkn lazima tu keep on trying bila kuchoka.
maendeleo yao shuleni yakoje.
Kama wanajitambua umshukuru Mungu wako.
actually hiki ndo huwa kinanipumbaza hata nachukulia na mambo mengine ya kimaadili yanaenda sana. Manake maendeleo yao shuleni yanaridhisha, na tabia zao nyumbani au machoni mwetu ni njema, ila kumbe huko nyuma ya pazia kuna vituko vinaendelea