Ushauri tafadhali, nataka kuacha kazi Serikalini nitimkie ughaibuni

colin_morgan

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,443
2,896
Habari wakuu

Bila kupoteza muda niende kwenye point husika kama kichwa cha habar hapo juu

Mimi ni mtumishi wa Serikali ila kwa muda sasa nimekuwa nikiwaza juu ya kuacha hii kazi na kutimkia ughaibuni kuanza maisha mapya

Najua si jambo la kujiamulia tu ukiangalia hali ilivyo ngumu nyakati hizi kupata ajira....ndo nimeamua kuja kwenu wadau munipe a..b..c

Nchi ambazo nataka nizamie ni canada au Uk moja wapo hapo so naomba wale wa tz wenzangu ambao wapo huko waje kunishauri na kunipa expirience pia za hizo nchi husika

Nasubiri ushauri wenu wadau nitashukuru sana

Mnakaribishwaaaa.
 
Unachotaka kushauriwa ni kipi ?

Kuacha Kazi au kuendelea ?

Namna ya kuzamia ?

Fursa huko Canada/UK ?
 
Hapa tanzania unalipwa/ unakilato cha Tsh. Ngapi kwa mwezi???? Na huko Canada/ USA unategemea kuwa na kipato cha Tsh. Ngapi kwa mwezi

Unategemea kuenda kufanya kazi zipi? Skilled au Unskilled?

Una historia yoyote ya kusafiri/ Kuishi nchi za kigeni???

Kwa hili janga la Korona, nakushauri utulie nyumbani. Hata huko nchi za dunia ya kwanza Uchumi sio mzuri na kazi hakuna.

Au mnasemaje mods wa JF
 
Ndugu hayo ni maisha yako fanya kile moyo wako unataka, niongozee nyama tu kidogo kwa kushauri.

Kwa vile ni mwajiriwa tumia likizo yako moja kwenda kutembea na kusoma mazingira kwenye hiyo nchi unayotaka kwenda mpaka unamaliza likizo yako unarudi bongo utaweza kufanya maamuzi sahihi juu ya mustakabali wa maisha yako. Lakini kuwa makini kwa kila hatua unayofanya.

Hayo ni maisha yako pambana unavyoweza kuyawin
 
Nje sio kwamba unaomba visa tu ya kufanya kazi unapewa. Unless umepata kampuni tayari ambayo ipo tayari kukusponsor visa au kama una 200 million ya kwenda nje kuinvest kuingia sio kirahisi, ndiyo maana wengi wanapitia njia za shule kwanza. Ukienda kuomba visa ukafanye kazi nje hivihivi tu watakunyima.

Maisha UK, Canada, US ni bora sana kuliko Tz, nimeishi nchi zote hizi na huwezi kabisa kulinganisha na Tz ni kama usiku na mchana. Kuna advantage na disadvantages zake. Ila panaishika vizuri tu, ukifika jitahidi usigawe tu contact, waliobaki bongo watakua wanakuomba hela kila siku utadhani kuishi nje tayari ushageuka milionea.
 
Siku nikipata nafasi nitakuja kuwaelekeza vijana madhara ya kufanya kazi/kuishi abroad, nitawapa mfano wa mimi mwenyewe.
Kwakifupi niliacha kazi nje, wakati nikiwa nalipwa mshahara mzuri na kisha nikarudi back home Tz, nikajiajiri kwa kipato kiduchu.
Leo nimekuwa mwenye furaha, amani tele na kipato kimeongezeka raha burdani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea na aina ya utumishi ulionao nchini mwako, kuna baadhi ya kada hata ukiacha hauna cha kupoteza
 
Hapa tanzania unalipwa/ unakilato cha Tsh. Ngapi kwa mwezi???? Na huko Canada/ USA unategemea kuwa na kipato cha Tsh. Ngapi kwa mwezi

Unategemea kuenda kufanya kazi zipi? Skilled au Unskilled?

Una historia yoyote ya kusafiri/ Kuishi nchi za kigeni???

Kwa hili janga la Korona, nakushauri utulie nyumbani. Hata huko nchi za dunia ya kwanza Uchumi sio mzuri na kazi hakuna.

Au mnasemaje mods wa JF
kipato changu monthly kinafika 1m
huko nje kazi yeyote tu....kama skilled or unskilled nitafanya muhimu maslahi tu

kama nitapata chance nimepanga kupiga short course

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa jinsi corona ilivyo-colonize uchumi wa dunia, nakushauri kwa sasa hivi usubirie kidogo hadi hali iwe shwari, maana duniani kote kuna watu wamepoteza ajira zao kipindi hiki na kuna kundi kubwa la jobless, so ni vema ungevuta subira.
 
Ndugu hayo ni maisha yako fanya kile moyo wako unataka, niongozee nyama tu kidogo kwa kushauri.

Kwa vile ni mwajiriwa tumia likizo yako moja kwenda kutembea na kusoma mazingira kwenye hiyo nchi unayotaka kwenda mpaka unamaliza likizo yako unarudi bongo utaweza kufanya maamuzi sahihi juu ya mustakabali wa maisha yako. Lakini kuwa makini kwa kila hatua unayofanya.

Hayo ni maisha yako pambana unavyoweza kuyawin
asante mkuu kwa ushauri wenye busara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku nikipata nafasi nitakuja kuwaelekeza vijana madhara ya kufanya kazi/kuishi abroad, nitawapa mfano wa mimi mwenyewe.
Kwakifupi niliacha kazi nje, wakati nikiwa nalipwa mshahara mzuri na kisha nikarudi back home Tz, nikajiajiri kwa kipato kiduchu.
Leo nimekuwa mwenye furaha, amani tele na kipato kimeongezeka raha burdani.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu kwanini usinieleze kidg leo....au japo pm kama unahis haupo comfortable hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom