Ushauri: Siyaelewi haya maisha ya ndoa

Kijana mbona wewe ndio una shida, huyo binti anataka utoe mahari anaishi kwa stress kwasababu yako, wazazi wamemtenga anahisi hata wewe hutakuja kumwacha, peleka mahari au posa utamwona anavyobadirika na kurudi hali yake ya awali.
 
Hela ya mahali nilipata million kadhaa nilipomwambia nikalipe mahari alikuwa mbogo na akanishauri nikafanye kitu kingine.

Kiuhalisia mimi hata nisingeweza kuishi nae nilitaka akakae kwao ila wamemkataa hawamtaki
 
Kijana mbona wewe ndio una shida, huyo binti anataka utoe mahari anaishi kwa stress kwasababu yako, wazazi wamemtenga anahisi hata wewe hutakuja kumwacha, peleka mahari au posa utamwona anavyobadirika na kurudi hali yake ya awali.
Posa nilishapeleka mahari ndo sina hela kwa sasa uchumi wangu umekuwa mbovu..

Mpaka juzi nimemwambia nataka niuze eneo nikalipe mahari kwao anakataa?
 
Mwanzoni anaondoka kiukweli alikuwa potential sana ndo maana nikamtafuta tena ila kwa sasa amerudi naona amekuwa mbogo na kuanza kunionesha makucha yake live hapa najiuliza siku akipata hela atakuaje ?

Ukimwambia issue za kuachana anakwambia poa tu.
 
In short huyo mwanamke hana afya kwa maisha ya ndoa no matter what! Utajuta sana maishani kuwa na mke km huyo. On the other hand kuishi na mtoto wa mtu bila kutoa chochote ni hatari kuliko hatari yenyewe, haiko direct ila utaona ugumu wake ukopatwa na tatizo upande wa mkeo, utaona nyota zote. Fanya maamuzi km unataka awe mkeo lipa mahari, km humtaki acha kikaa nae kabisa
 
Kwao wamemkataa hawamtaki yeye wala watoto wangu na hapo ndipo nilipoamua kuanza kuishi nae.
 
Tatizo lako ni hapo kwenye umri wa miaka 30 ila bado unajiona ni kijana mdogo,

Huwezi kupata mwanamke ambae yupo perfect 100% hata wewe hapo una mapungufu yako,

Uamuzi ni wako,hapa utapata kila aina ya ushauri ila at the end uamuzi ni wako,

Fanya kile ambacho nafsi yako inacho kitaka,

Good luck.
 
Kwao wamemkataa hawamtaki yeye wala watoto wangu na hapo ndipo nilipoamua kuanza kuishi nae.
Kwao wamemkataa coz inaonekana kabisa hakusikia ushauri wa wazazi wake na akaja kwako kwa mapenzi yake kwako,

Wazazi wake sio kwamba wanataka mahari coz ya hela bali mahari maana yake ni kua binti yao anaolewa na sio kuishi na mwanaume bila ndoa,

Familia ya huyo Mwanamke inaonekana wanajitambua sana na walimlea binti yao kwenye maadili mema ila mapenzi yake kwako yakamtia upofu.
 
Na jamaa anataka kumkacha.

Jamaa ajiangalie na yeye ni kipi anakosea, asimkosoe binti tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…