Ushauri: Sidumu katika mapenzi

Ushauri: Sidumu katika mapenzi

Mleta mada umepoteza taste ya kupenda ndo maana.pole
 
Wakuu habarini za mida hii,

Poleni kwa majukumu ya kila siku ya kukabiliana na changamoto za maisha. Nina hoja nataka mnipe ushauri ndugu zangu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27. Kwa muda sasa nimekuwa na wapenzi tofauti tofauti.Mpenzi pekee niliyeweza kudumu naye kwa muda mrefu ilikuwa ni miaka miwili(Japo nilikua ninamsaliti kwa tamaa zangu lakini tuliweza kudumu),baada ya kuachana naye sasa miaka kadhaa imepita na sijawahi kuwa katika mahusiano ya maana yaliyodumu zaidi ya miezi walau mitatu.Na hata inapotokea tumeachana huwa ni kimyakimya na wala sina hisia zozote za kujutia zaidi tu ya kuwaonea wivu wenzangu walio katika mahusiano mazuri.Ni kweli nina tamaa na huenda ndiyo sababu ya kutojutia pale ninapoachana na mpenzi mmoja kwa kuwa nionapo wengine ninapata ashiki kama binadamu wengine,lakini ninapoingia katika mahusiano (kwa kudhamiria na kujitoa kimwili na kiroho/yaani ninaamua kabisa kuwa huyu ninampenda kwa dhati na sitomfanyia baya lolote) mambo huishia katikati kimyakimya na bila sababu ya msingi,mpaka sasa nahisi nina mkosi na kiukweli roho inaniuma kuona wenzangu wakifaidi matunda ya mahusiano yao na wakiwa wenye furaha huku mimi nikiwa na wasiwasi wa kupata magonjwa kwa kutokuwa katika mahusiano yenye msimamo.


Naombeni ushauri wenu.
karibu kwenye chama pendwa la UMALAYA
 
Ni tabia ya kutokujali jambo/kitu fulani,..sasa si kitu kizuri inaweza kukugharimu kwenye maisha na unaweza usione impact yake kwa wakati huu...jaribu kutulia,tambua unahitaji nini kwenye mahusiano yako,.yape thamani mahusiano yako nayo yatakuthamini.
nashukuru kwa ushauri.nitaufanyia kazi
 
Hatua ya kwanza ni kujitambua, wewe umeshajitambua, next ni kutengeneza plan then third unatakiwa kusimamia
 
Jaribu penzi na mabeki 3...wale ndio wa kujifunzia mkuu kama upo kilimanjaro driving school vile
 
Wakuu habarini za mida hii,

Poleni kwa majukumu ya kila siku ya kukabiliana na changamoto za maisha. Nina hoja nataka mnipe ushauri ndugu zangu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27. Kwa muda sasa nimekuwa na wapenzi tofauti tofauti.Mpenzi pekee niliyeweza kudumu naye kwa muda mrefu ilikuwa ni miaka miwili(Japo nilikua ninamsaliti kwa tamaa zangu lakini tuliweza kudumu),baada ya kuachana naye sasa miaka kadhaa imepita na sijawahi kuwa katika mahusiano ya maana yaliyodumu zaidi ya miezi walau mitatu.Na hata inapotokea tumeachana huwa ni kimyakimya na wala sina hisia zozote za kujutia zaidi tu ya kuwaonea wivu wenzangu walio katika mahusiano mazuri.Ni kweli nina tamaa na huenda ndiyo sababu ya kutojutia pale ninapoachana na mpenzi mmoja kwa kuwa nionapo wengine ninapata ashiki kama binadamu wengine,lakini ninapoingia katika mahusiano (kwa kudhamiria na kujitoa kimwili na kiroho/yaani ninaamua kabisa kuwa huyu ninampenda kwa dhati na sitomfanyia baya lolote) mambo huishia katikati kimyakimya na bila sababu ya msingi,mpaka sasa nahisi nina mkosi na kiukweli roho inaniuma kuona wenzangu wakifaidi matunda ya mahusiano yao na wakiwa wenye furaha huku mimi nikiwa na wasiwasi wa kupata magonjwa kwa kutokuwa katika mahusiano yenye msimamo.


Naombeni ushauri wenu.
Ni lazima ufahamu kweli hizi;

1. Mwanadamu anapenda mara moja tu, zingine zote ni ashiki majinuni ikiambatana na kuvumilia kuwa kwenye mapenzi au mahusiano ili siku ziende.

2. Mahusiano sio kufanya ngono, ukiingia katika mahusiano na mtazamo huo, jua kuwa safari yako itakuwa na milima zaidi badala ya tambalale za mahusiano yanayopelekea ndoa.

3. Kabla ya kuanza mahusiano na mtu, mchunguze kwanza wewe binafsi kuhusu tabia yake, mienendo yake, pamoja na familia yake ili utakapoanzisha move za mahusiano yawe yanayokupelekea kwenye kuoa na sio kufanya ngono tu.

Mwisho: Hakuna katika maandiko matakatifu sehemu inayosema kuwa kuna mtu alichumbia akakaa miaka miwili ndio akaoa, walipeleka posa na kuoa mara moja. Unless unakitabu chako tofauti na changu.

Kwahiyo ndugu badili mtazamo kuhusu mahusiano ili usiendelee kukosea zaidi, maana hata mimi ninaekushauri nilishabugi sana na mpaka sasa najutia ila nasonga mbele kibingwa.
 
Huenda ikawa ni kweli kutokana na historia yangu hapo nyuma lakini kama ni kweli mbona wakati mwingine natamani kupenda haswaa!?
Huwa inatokea huna habar na binti hasa baada ya kumla.Ni kupoteza hali ya upendo ndani yako.Itakuchukua muda mrefu kuanza kupenda tena.Pole sn
 
Nna tatizo kama lako ila siwaonei wivu jamaa zangu zaidi wananifanya kuonekama muhuni flani kwa familia zao.

maana kuna jamaa zangu wawili kila wakinitambulisha kwa wake zao wanakazia huyu ni zipompa umemuona lakini yaani wananitambulisha kama kutoa tahadhari flani. huwa inaniuma balaa

ukizingatia sinaga nia ovu nao. yaani kuna wakati huna najicheka kwa umri huu 25+ sina mahusiano ya kudumu/maana.
 
Ni lazima ufahamu kweli hizi;

1. Mwanadamu anapenda mara moja tu, zingine zote ni ashiki majinuni ikiambatana na kuvumilia kuwa kwenye mapenzi au mahusiano ili siku ziende.

2. Mahusiano sio kufanya ngono, ukiingia katika mahusiano na mtazamo huo, jua kuwa safari yako itakuwa na milima zaidi badala ya tambalale za mahusiano yanayopelekea ndoa.

3. Kabla ya kuanza mahusiano na mtu, mchunguze kwanza wewe binafsi kuhusu tabia yake, mienendo yake, pamoja na familia yake ili utakapoanzisha move za mahusiano yawe yanayokupelekea kwenye kuoa na sio kufanya ngono tu.

Mwisho: Hakuna katika maandiko matakatifu sehemu inayosema kuwa kuna mtu alichumbia akakaa miaka miwili ndio akaoa, walipeleka posa na kuoa mara moja. Unless unakitabu chako tofauti na changu.

Kwahiyo ndugu badili mtazamo kuhusu mahusiano ili usiendelee kukosea zaidi, maana hata mimi ninaekushauri nilishabugi sana na mpaka sasa najutia ila nasonga mbele kibingwa.
shukrani mkuu,kuna kitu nimejifunza hasa kuhusu mtazamo.Nitaufanyia kazi ushauri wako
 
Back
Top Bottom