Ushauri: Service road maeneo ya Kimara zitumike jioni kuondoa foleni

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Kwenu wahusika!

Tunakuwa na foleni zisizo na tija kabisa muda wa jioni kuanzia Kibo kwenda Kimara na muda mwingine hadi Stopover.

Mh mkuu wa kanda maalum, tunaomba njia mbadala kuondoa hizi foleni service road zitumike. Huzuni imekuwa ni sehemu ya watu kupigia faini zao.

Wanaokaa Kimara DAWASCO
Hivi sasa kuna njia imetengenezwa vizuri tu, mnaweza mkaona mtu anaekwenda Kimara DAWASCO badala ya kukaa foleni anatumia service road mpaka bucha. Anaingilia mataa ya Kibo pale anapandisha Korogwe inakwenda mpaka njia ya kuingilia DAWASCO Kimara hapo unaokoa magari mengi kukaa mainroad.

2) Wanaoishi Baruti na Bucha na Korogwe, kiuhalisia hawa watu wangeweza kusaidiwa na service road. Wakifika Kibo mataa wanaingia service road wanaokaa vinane wanaingilia pale Msikitini, wanaoenda Bucha wakifika kwa Thomas Lyimo waanaenda moja kwa moja makwao.

Wale wa Korogwe badala ya kusubiri foleni wanaambaa na service road mpaka Kanisani wanaingia makwao.

Inasikitisha hata sisi tunaowahi ibada za jioni kwa mastaha unakuta ibada ndio imeisha ama unakuta watu wamekaa pale mataa upande a service road inabidi sadaka ujigaie kwenye gari mwenyewe ama utafute nyama choma karibu

Naamini hata njia kuu itabaki na malori tu na baadhi ya magari ya Kimara Bonyokwa nk. Tunaomba msaada wenu kwa hili, hivi sasa ikifika saa kumi na moja hujapita unakaa foleni saa moja, Kibo kuiona Baruti ama Kimara
 
Upo sahihi ,me nahisi ni vizur kama kuna folen hizi service road zingekuwa sinaruhusiwa kwa wahusika wanaokwenda sehem husika wapite huko mfano ni mataa ya tabata ukiwa unatoka buguruni unaenda segerea unaruhusiwa kupita service road tu, hii imesaidia sana kupunguza folen ya pale matumbi ukitokea buguruni, sasa sijui hawa viongozi wetu hawa lioni hili, kwa mfano sisi tunaopita mandela road folen ya matumbi kwenda buguruni ni kero sana aisee, ingeruhusiwa wanaoenda kariakoo wakifika buguruni wapite service road tu maana unaweza tumia hata masaa mawili kwenye ile folen ya matumbi buguruni yaan ni kero sana, mbaya zaidi hapo kwenye hizo folen ndipo unakuta matrafiki wamejificha wanasubiria upite service road wakupige fine , yaan ni kero
 
Back
Top Bottom