USHAURI: Rais Samia Suluhu amteue Joseph Magufuli kuwa Mbunge na Waziri

Huyo kijana amtafutie permanent job kwenye taasisi moja safi inatosha (like BOT, TRA & TCRA)

Apate uwezo/uhakika wa kumtunza Mama yake na Bibi yake
Aende akasimamie miradi ya baba yake si ana kiwanda cha maziwa na mayanga contraction na ile kampuni yao ya clearing and forward ambayo ina tawi hadi Rwanda aende akazisimamie
 
Nikiri kuwa binafsi nilikuwa simfahamu Joseph Magufuli kwa undani hadi nilipomuona juzi akiongea kwenye kongamano la kidini kule Chamwino, Dodoma.

Kijana huyu jasiri alipokaribishwa kutoa shukrani za familia mbele ya Rais na viongozi wa dini, alionesha ukomavu mkubwa sana. Kwa wale mliofuatilia kongamano hili mtakubaliana nami kuwa hata mama Samia alionyesha kumkubali.

Bila kuwachosha na maneno mengi, naomba niingie kwenye hoja moja kwa moja. Umekuwa ni utaratibu wa kawaida kiongozi anapofariki, hasa mbunge, mtoto wake huchukua usukani wa jimbo alilokuwa akiliongoza marehemu baba au mama yake. Mifano ipo mingi sina haja ya kuitaja.

Sasa kwa kuwa Rais Magufuli kipenzi cha wana wa Tanzania, Afrika na dunia nzima ametutoka ghafla pasipo kutarajia, namuomba sana Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu amteue ndugu Joseph John Pombe Magufuli kuwa mbunge na hata kama itampendeza amteue kuwa waziri katika wizara yoyote atakayoona inafaa.

Ninazo sababu zilizonipelekea kutuma ombi langu hili kwa mama Samia na nitazieleza kwa ufupi sana kama ifuatavyo:

Marehemu Rais John Pombe Joseph Magufuli alikuwa kipenzi cha watanzania wote na dunia nzima kwa ujumla. Kitendo cha kumteua Joseph Magufuli kuwa mbunge kitawafuta machozi watanzania, hasa pale watakapokuwa wakisikia jina la Magufuli likitajwa kupitia kwa mtoto wake.

Tukumbuke kuwa Magufuli alikuwa anapendwa na watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kidini, kisiasa, kikabila, kikanda na kijamii. Hivyo basi, uwepo wa mtoto wa Magufuli ndani ya serikali utawafariji watanzania wote na watu wenye mapenzi na maendeleo ya taifa letu.

Kama ilivyo kawaida kwa watoto wa wabunge waliofariki kufutwa machozi kwa kupewa ubunge kwenye majimbo waliyokuwa wakiyaongoza wazazi wao, kitendo cha Joseph Magufuli kuteuliwa kuwa mbunge na waziri kitasaidia kuifuta machozi familia kwa kuwa nina imani mshahara atakaokuwa anaupata kutokana na uwaziri utasaidia sana kuboresha hali za kiuchumi za wanafamilia.

Ingekuwa baba yake alikuwa mbunge ingekuwa rahisi sana kuteuliwa kugombea ubunge na kukalia kiti cha jimbo la baba yake. Lakini kwa kuwa baba alikuwa Rais, na kwa mujibu sheria anayepaswa kukalia kiti hicho ni makamu wa Rais, hatuwezi kusema mama Samia ampishe akalie usukani kwa kuwa tukifanya hivyo tutakuwa tunavunja katiba ya nchi. Hivyo, njia pekee ya Joseph Magufuli kupenya kwenye siasa ni kupitia ubunge na uwaziri wa kuteuliwa.

Joseph Magufuli ni kijana msomi na mwenye uwezo wa kuongoza wizara yoyote ijapokuwa hajawahi kuingia kwenye siasa. Hivyo, nina imani kuwa anaweza kuwa waziri mzuri kama alivyokuwa baba yake. Na ningependekeza mama Samia amteue kuwa waziri wa ujenzi ili kumuenzi marehemu baba yake aliyewahi kuongoza wizara hiyo kwa ufanisi mkubwa. Ikiwa watoto wa wabunge waliowahi kuziba nafasi za baba/mama zao huko nyuma hawakushindwa, iweje Joseph yeye ashindwe?

Kwa sababu hizi nilizozitaja hapo juu, namuomba sana mama yetu na Rais wetu mpendwa H.E Samia Suluhu Hassan amteue Joseph Magufuli kuwa mbunge na kama itampendeza amteue kuwa waziri wa ujenzi.

Nawasilisha.​

Kmlammko !!
 
Familia ya Kikwete si ndio hao akina Ridhiwani na Salma Kikwete (mke mtu)
First lady kama mama.salma ilitakiwa akae nyumbani.amlee mzee jk lakini kwa tamaa zao.sasa anaenda kumkosoa mmeo aliyokuwa akifanya!kustaafu ni heshima angemwachia mwanae ridhiwan tu. Hawa watu bwanaaaaaa
 
Mkuu nadhani hujanielewa vizuri. Mimi nimezaliwa katika familia ya kinyonge ndio maana nimependekeza Joseph aliyezaliwa katika familia ya kitawala ateuliwe. Babu yangu alikuwa mnyonge, baba yangu alikuwa mnyonge pia na amenirithisha unyonge ambao pia nitaurithisha kwa wanangu. So, ni vizuri kila mtu arithike na kipaji alichorithishwa na wazazi wake.
Ha ha ha hata Mungu hapendi mtu anaekata tamaa wewe ni binadamu sawa na huyo Joseph,narudia tena usikubali unyonge tena kwa kiwango hicho chako ni dhambi!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nikiri kuwa binafsi nilikuwa simfahamu Joseph Magufuli kwa undani hadi nilipomuona juzi akiongea kwenye kongamano la kidini kule Chamwino, Dodoma.

Kijana huyu jasiri alipokaribishwa kutoa shukrani za familia mbele ya Rais na viongozi wa dini, alionesha ukomavu mkubwa sana. Kwa wale mliofuatilia kongamano hili mtakubaliana nami kuwa hata mama Samia alionyesha kumkubali.

Bila kuwachosha na maneno mengi, naomba niingie kwenye hoja moja kwa moja. Umekuwa ni utaratibu wa kawaida kiongozi anapofariki, hasa mbunge, mtoto wake huchukua usukani wa jimbo alilokuwa akiliongoza marehemu baba au mama yake. Mifano ipo mingi sina haja ya kuitaja.

Sasa kwa kuwa Rais Magufuli kipenzi cha wana wa Tanzania, Afrika na dunia nzima ametutoka ghafla pasipo kutarajia, namuomba sana Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu amteue ndugu Joseph John Pombe Magufuli kuwa mbunge na hata kama itampendeza amteue kuwa waziri katika wizara yoyote atakayoona inafaa.

Ninazo sababu zilizonipelekea kutuma ombi langu hili kwa mama Samia na nitazieleza kwa ufupi sana kama ifuatavyo:

Marehemu Rais John Pombe Joseph Magufuli alikuwa kipenzi cha watanzania wote na dunia nzima kwa ujumla. Kitendo cha kumteua Joseph Magufuli kuwa mbunge kitawafuta machozi watanzania, hasa pale watakapokuwa wakisikia jina la Magufuli likitajwa kupitia kwa mtoto wake.

Tukumbuke kuwa Magufuli alikuwa anapendwa na watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kidini, kisiasa, kikabila, kikanda na kijamii. Hivyo basi, uwepo wa mtoto wa Magufuli ndani ya serikali utawafariji watanzania wote na watu wenye mapenzi na maendeleo ya taifa letu.

Kama ilivyo kawaida kwa watoto wa wabunge waliofariki kufutwa machozi kwa kupewa ubunge kwenye majimbo waliyokuwa wakiyaongoza wazazi wao, kitendo cha Joseph Magufuli kuteuliwa kuwa mbunge na waziri kitasaidia kuifuta machozi familia kwa kuwa nina imani mshahara atakaokuwa anaupata kutokana na uwaziri utasaidia sana kuboresha hali za kiuchumi za wanafamilia.

Ingekuwa baba yake alikuwa mbunge ingekuwa rahisi sana kuteuliwa kugombea ubunge na kukalia kiti cha jimbo la baba yake. Lakini kwa kuwa baba alikuwa Rais, na kwa mujibu sheria anayepaswa kukalia kiti hicho ni makamu wa Rais, hatuwezi kusema mama Samia ampishe akalie usukani kwa kuwa tukifanya hivyo tutakuwa tunavunja katiba ya nchi. Hivyo, njia pekee ya Joseph Magufuli kupenya kwenye siasa ni kupitia ubunge na uwaziri wa kuteuliwa.

Joseph Magufuli ni kijana msomi na mwenye uwezo wa kuongoza wizara yoyote ijapokuwa hajawahi kuingia kwenye siasa. Hivyo, nina imani kuwa anaweza kuwa waziri mzuri kama alivyokuwa baba yake. Na ningependekeza mama Samia amteue kuwa waziri wa ujenzi ili kumuenzi marehemu baba yake aliyewahi kuongoza wizara hiyo kwa ufanisi mkubwa. Ikiwa watoto wa wabunge waliowahi kuziba nafasi za baba/mama zao huko nyuma hawakushindwa, iweje Joseph yeye ashindwe?

Kwa sababu hizi nilizozitaja hapo juu, namuomba sana mama yetu na Rais wetu mpendwa H.E Samia Suluhu Hassan amteue Joseph Magufuli kuwa mbunge na kama itampendeza amteue kuwa waziri wa ujenzi.

Nawasilisha.​
Sawasawa Joseph jiwe tumekusikia

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Aisee Yan watoto ambao baba alishawaachia urithi mkubwa Bado unawapambania.na wakat vijana mtaan no ajira
 
Back
Top Bottom