Ushauri: Rais awe na ajenda moja ya kutekeleza kwa kipindi atachokuwa madarakani

Kazanazo

JF-Expert Member
Aug 16, 2023
686
1,360
Katika kubadirisha viongozi wa nchi kila baada ya miaka mitano au kumi, ni bora kila Rais aje na Ajenda Kuu moja ya kutekeleza kwa miaka kumi zingine zikiwa ajenda ndogondogo.

Mfano kwa mwaka 2025-2035 Ajenda Kuu ya Rais ajae iwe ni sekta ya umeme, kwahiyo miaka yake yote kumi afumue na aweke mifumo ya kisasa ya kusambaza umeme reliable nchi nzima na kutafuta solution ya kudumu ili umeme usikatike tena kwa miaka kumi inawezekana.

Vivo hivyo kwenye sekta nyingine kama miundo mbinu (kama alivyofanya mzee Magufuli), madini, afya, elimu na nyinginezo. Hii itatusaidia kama nchi baada ya miongo mitano au kumi tutakuwa tuko mbali sana.

Nawasilisha.
 
Nilikuw nawaza hvo,ila nikaja kuona kutakuwa na unprogressive za mirad mingi.kodi,malipo kwa serikali ila unachosema pia ne4yo kinafanyiwa kazi now ni mda wa ujenzi tu kwenye afya,elimu na barabara kwa wingi.
 
Nilikuw nawaza hvo,ila nikaja kuona kutakuwa na unprogressive za mirad mingi.kodi,malipo kwa serikali ila unachosema pia ne4yo kinafanyiwa kazi now ni mda wa ujenzi tu kwenye afya,elimu na barabara kwa wingi..
Miaka kumi ni mingi sana kwa kuangalia zaidi secta moja tungefanikiwa pakubwa kuliko ivi tunavyoenda
 
Back
Top Bottom