Sijui wenzangu mnaonaje. Kama watu wamefungia mamilioni majumbani na kusababisha pesa isiwe kwenye mzunguko kwa kuogopa majipu yanayotumbuliwa, bora pesa ibadilishwe at short notice ili zilazimike kwenda kwenye ma bank na kisha kwenye mzunguko. Mimi si mchumi ila naona itasaidia uchumi maana kuna tetesi watu wamefungia mabilioni nyumbani hawataki yaende bank kwa uoga. Kama ni kweli lazima mapesa haya yatakwamisha juhudi za president wetu na uchumi utaathirika. Unaunga mkono hoja? Tujadili kwa uzalendo kwani kutumbua majipu sugu ni kazi ngumu.