Hance Mbuya
Member
- Apr 11, 2012
- 45
- 12
Kama unampenda kweli utamsaidia lakini kama una mpango wa kumchezea we chapa lapa. Inawezekana huyo binti maisha ya nyuma alipitia maisha magumu sana inawezekana wazaz au walezi wake walikuwa wakali sana kwahiyo akajikuta anaishi maisha ya kutojiamini,embu jitahid kujua background yake,ukikuta kuna tatizo anza kumchangamsha na kumsaidia kukutana na watu mbalimbali ukimjengea tabia ya kujiamini,pendelea kuzungumzia zile stori anazopenda unamshirikisha kwa upendo,unampa macare ya kufa mtu penda kujua kila wakat anafanya nini,viutan vizur vya kimapenz huku ukimthamini mbona ataanza kufunguka mwenyewe halafu atakuja kuwa talkative kuliko ww,pia inawezekana ikawa shule lakini nayo si kigezo tumia ndondoo hizo hizo hapo juu,zaid msaidie kumjengea tabia ya kujiamini kwmb mawazo yake ni mazur na unayathamin hata kama kaongea kisicho ww unapotezea unamrekebisha kiaina kwa upendo.
Tuko pamoja nilishakumbana nalo hilo kwa ndugu yangu na baada ya kufanya hivyo yaan mkewe amekuwa the best woman,pia jitahidi usiwe mkali sana na mwenye hasira kupitiliza,mfanye kuwa rafiki zaidi nakwambia atafunguka na ataueleza yanayomsifu,make her to feel like woman. Jembe hilo baba siku hizi kupata mwanamke mwenye sifa za mke ni adimu sana.Ebana shukran kwa advise ulioutoa big up.Ni hivi nampenda sana natamani awe mke wangu.Ana kila sifa ya kuwa mke bora.Ila tatizo ndo hilo.Shukran kwa ushauri nitaufanyia kazi.
kwani hajasoma kabisa au? infact wanawake wenye hawaongei wanaboa saana,
pia kama mnatofautiana sana kielimu anaweza akajiona mawazo yake infirior fulani hivi
ni psychologia tu ila mambo flani kwa 6/6 nini freshi,,
\ukiona wasi sasa fanya maamuzi ya mwaka
gud luck
sasa wewe unataka kusimuliwa hadi movie si uangalie mwenyewe , ushajua binti ni mkimya hujiulizi labda maswali yako yanam-bore? au labda interest zenu tofauti ndo maana mnashindwa kupiga stori?
Ilikuwa tar 24/01/2012 ndipo nilipoanzisha uhusiano wa kimapenzi na kadadaa(sio jina halisi)ana 23yrs.Kilichonifanya nianzishe uhusiano nae ni muonekano wake jinsi alivyo,usafi,pia tabia.Kadadaa alikuwa ni mkimya sana si mtu wa story kama walivyo wanawake wengine hii ilinipa shida sana kujua kama ananipenda au napoteza muda wangu kumfuatilia,ilichukua kama miezi miwili baadae akaja kunikubalia,sikuamini moyoni kama ni kweli au anatania lakini mwisho wa siku ilikuwa kweli.Mara kwa mara huwa anapenda kukaa peke yake peke yake.Sikumfahamu kiundani mwanzo ila kadri muda ulivyozidi niliweza kugundua kitu.Kadadaa na vyote alivyokuwa navyo vizuri lakini anashindwa kutoa ushauri,kuamua jambo peke yake,Wakati mwingine anaweza akawa anaangalia muvi.Badae ukampigia na kumuuliza vip ile muvi uliipenda,anakujibu yah niliipenda sana tena sana ilikuwa nzuri we acha tu,Kazi inakuja pale utakapomwambia aielezee kidogo jinsi ilivyokuwa au sehemu aliyoipenda,hapa anaweza kukata simu au akakaa kimya mpaka ubadili story.Nafahamu kila binadamu ana mapungufu yake,lakini mapungufu aliyo nayo sijui ni yanaitwaje.Kabla nilijua anafanya kusudi kumbe ndivyo alivyo.Hapa vip elimu inaweza ikachangia au maisha aliyoishi hapo awali?Naombeni ushauri kwani love inashuka siku hadi siku kama ni asilimia zimebaki 10% tu.
wife material huyo komaa mpaka umfunge paka kengele.
poa fazaa!
sasa wewe unataka kusimuliwa hadi movie si uangalie mwenyewe , ushajua binti ni mkimya hujiulizi labda maswali yako yanam-bore? au labda interest zenu tofauti ndo maana mnashindwa kupiga stori?