ushauri please

mamkindi

Member
Mar 14, 2012
61
5
Nina mahusiano na mtu ambaye tumekutana kwenye mtandao na hatujawahi kuonana, mwanzo tulikuwa tunawasiliana vizuri sana kwa skype, cha ajabu imefika kipindi mawasiliano yamekata na visa vya hapa na pale. hapa ninapofanyia kazi kuna kijana amekuwa akinifuatilia na sasa ni miezi mitatu na ninamuona ana mwelekeo. nimeshindwa kuamua ni mwache huyu ambaye hatujawahi kuonana hata siku moja sababu yeye ni mtanzania na yupo marekani. ushauri wenu wanajamvi
 
yani unataka kuacha moja la mkononi kwa ajili ya 99 ya mwituni?mpe nafasi kijana wa ofisini ni rahisi kumjua sio hayo ya mtandaoni!
 
unatisha, wa mtandaoni!

Bora umeweka wazi. maana kuna waliosbiri kuja kuolewa mpaka wakazeeka kisa kijana wa mtandaoni toka marekani!
 
uliza watu wa UPanga watakwambia mume wa mtandaoni
nimesahau, subiri wajuzi watakujuza ndio utasoma namba
 
mapenzi ya bluetooth ya nini bi dada, charge inaweza isha bure ukashindwa kulipata file lote....mpe nafasi huyo wa ofisini bhanaa
 
Unatema .....kwa karanga za kuonjeshwa? Maswali mengine bhana?
 
achana na wa online, cheki na huyo wa hapo ofisini kwako...!!!
Nina mahusiano na mtu ambaye tumekutana kwenye mtandao na hatujawahi kuonana, mwanzo tulikuwa tunawasiliana vizuri sana kwa skype, cha ajabu imefika kipindi mawasiliano yamekata na visa vya hapa na pale. hapa ninapofanyia kazi kuna kijana amekuwa akinifuatilia na sasa ni miezi mitatu na ninamuona ana mwelekeo. nimeshindwa kuamua ni mwache huyu ambaye hatujawahi kuonana hata siku moja sababu yeye ni mtanzania na yupo marekani. ushauri wenu wanajamvi
 
Naona ushauri ushatosha. Kila la kheri na angalia usiharibu kazi. Utushirikishe vicheni pate, Zinduna kesharudi.
 
mi naona aendelee na wa mtandaoni.....huwezi jua ni lini utamtembelea Obama.....huyo wa ofisini atakuzengua kudadadeki.....
 
wa mtandaon anaweza akawa jike, linaigiza sauti ya kibesi.

chukua kitu cha ofc mama.

hapa najipigia pande naweza nikawa mimi, si unajua humu hatujuani?
 
mi naona aendelee na wa mtandaoni.....huwezi jua ni lini utamtembelea Obama.....huyo wa ofisini atakuzengua kudadadeki.....

Ha ha ha haaah!! Preta acha kumuingiza mwenzako chaka.
 
Last edited by a moderator:
Tahadhari...mahusiano kazini yamekuwa yana matokeo mabaya, ikiwa mnafanya kazi eneo moja please do not enter tain that kind pf relationship, kwani huwezi jua wengine pembeni watapokeaje...na huyu anakufuatilia kwa vile anakuona kila siku, subiri ukichukua likizo itakuwaje
 
yani unataka kuacha moja la mkononi kwa ajili ya 99 ya mwituni?mpe nafasi kijana wa ofisini ni rahisi kumjua sio hayo ya mtandaoni!
asante sana maana huyo wa mtandaoni sijawahi hata kumwona na pia mpaka 2014 ndio arudi
 
Tahadhari...mahusiano kazini yamekuwa yana matokeo mabaya, ikiwa mnafanya kazi eneo moja please do not enter tain that kind pf relationship, kwani huwezi jua wengine pembeni watapokeaje...na huyu anakufuatilia kwa vile anakuona kila siku, subiri ukichukua likizo itakuwaje
naelewa ila huyu hatupo ofisi moja bali huwa tunaonana maeneo haya na pia yeye yupo company tofauti na mimi
 
Back
Top Bottom