Ushauri please !!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri please !!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sagna, Mar 27, 2012.

 1. s

  sagna New Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa yangu leo amegunduwa kuwa mkeo huwa anatabia ya wizi pesa anazotoa za matumizi anapeleka kwao. Na gharama za nyumbani zimepanda lakini huduma na chakula ni kile kile leo katika pekua pekua zake kakuta laki moja chini ya meza na jana tu mkewe alikuwa analalamkika kuwa pesa haitoshe anayo acha aongeze kila akifika stori ni pesa pesa. Yeye ameamuwa ampe talaka arudi kwao mimi nimemshauri ampe nafasi nyingine ya kujirekebisha, jee nyie mnamshauri nini??????
   
 2. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Sasa pesa zote anapeleka wapi jamani?
  Labda anashida kubwa na mume wake si muelewa?
  Na huyo mume asiwe mwepesi kumtishia mkewe talaka!
   
 3. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Huu uzi unanikumbusha mbali sana, kuna ile nyimbo ilikuwa inaimbwa hivi.

  Huyu niliyeoa, sina la kusema
  Mshahara nikipata
  Bajeti apange yeye
  Anajenga nyumba kwao
  Mimi kwangu midabwada

  Mimi naona ampe muda wa kujirekebisha, yawezekana mume hampi hata pocket money ndio akaamua kuiba.
   
 4. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Du! kumbe na wewe umekula age kama mimi? mmmhh!
   
 5. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  He just need to judge if he has been a good husband, Kama ni mbahili sana kwa mkewe na mke Hana kipato unategemea niño? He can only be a judge by himself, ukimwambie ampe naFasi Kama lijamaa lenyewe Lina matatizo itasaidia niñi?

  Halafu achana na mapenzi ya watu, hujui wamekutana wapi na kwa mistake gani!

   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  anamuachia kiasi gani mpaka aseme anaiba pesa za matumizi?

  mke haruhusiwi kuwa na pesa?

  hana kazi wa kibiashara wala hachezi upatu au hayumo kwenye vikoba?

  huyo rafiki yako kamchoka mkewe/ au ni aina ya wanaume wasiotaka wake zao wawe na kitu aka wafujaji
   
 7. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Uwazi na mawasiliano ndani y mahusiano ni kitu kizuri sana,

  Huyo mwanamme inawezekana ana kipato kikubwa tu lkn ndio hivo hajampa nafasi mkewe kuwa muwazi na kujieleza shida zake especial km ni mama wa nyumban ndio maana inampelekea kufanya ivo au kutafuta njia ya kumaliza shida za kwao,

  Tena anatakiwa amshukuru mkewe kwan hiyo njia nayotumia kubana hiyo hela ni nzuri kuliko angetafuta bwana wa nje wa kummalizia matatizo yake,

  Na huyo mwanamke naye namlaum kwann asifunguke kwa mumewe japo akamsaidia hata kuwa na kijimradi cha kumwingizia chochote ili ajibane yeye na kumaliza shida za nyumban kwao?

  Cha kufanya huyo mwanaume aache akili za kitoto hawezi acha mke anayempenda kwa kosa km hilo,hapo tatizo ni uelewa,uwazi na mawasiliano yako kuwa madogo,

  Anatakiwa kumuonya mkewe kwa kumuelewesha na sio kumgombeza,na ampe mtaji ili ajishuhukishe na kupata japo kipato kidogo kwa ajili ya mambo yake binafsi na kuwasaidia ndunguze!!!
   
 8. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nadhani kuna mapugufu kwa wote wawili mume na mke wanatakiwa wakae waeleweshae hasa suala la kipato
   
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Inawezekana huyu mumewe huwa hana muda mzuri wa kukaa na mkewe na kudiscuss matatizo/mahitaji ya pande zote mbili. Na pia inawezekana mkewe huyo hana ajira na hana namna yoyote ya kumuingizia kipato nje na hela ya mboga anayoachiwa. Hivyo yumkini mkewe kaamua kutumia utaratibu huo ili kusaidia wazazi na ndugu wa upande wake. Ushauri: Mwambie jamaa awe karibu na mkewe na kumhoji kwa nini anachukua pesa na kupeleka kwao bila taarifa, na kuyasolve mambo haya kwa hekima zaidi kuliko kukimbilia talaka. Nani aliyewaambia talaka ndiyo suluhisho pekee la matatizo ya ndoa??
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Awe anamdakisha mkewe fungu lake la macarolite, mapowder na mazagazaga ili aache udokozi.
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Ukiona mwanamme anauliza chenji ya nyanya, si mwanamme timamu.

  Hivi unamwacha mkeo kila siku, unataka hadi hela ya pedi akuombe?
  kama mnakula kama kawaida na anasaidia kwao kunashida gani?

  Uchoyo wa aina gani huo?
  Hivi unadhani unioe uniweke mama wa nyumbani sina hata genge la nyanya, nitaacha kupiga panga niwasaidie kwetu?
  Hivi unadhani umenikuta mtu mzima, nimetokea shimoni?
  Sina uchungu na wazazi wangu? Niwaone wanalala njaa mie najichana, nitakuw MWEHU WA KARNE.

  Tatizo baadhi ya wanamme wana uchoyo wa chakula sana, hii ni aibu ya mwaka na wala si ya kuongea mabele za watu.
  Kama chakula tu ni tatizo, kusomesha watoto je?

  Mpe mkeo kahela ka matumizi yake binafsi kama utaona anakata panga hela ya nyumbani kwako.

  Big up sana kwa huyo dada, ndo maana nasema ukizaa binti umezaa asset hatakuacha ulale njaa, wana akili ya kujiongeza. Mwanamme aah anajali kwake na mkewe tu.
   
 12. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sasa mke wake akipeleka pesa kwa wazazi wake kosa gani.


  Mimi ndo ningezidisha kumpenda mke wa namna hio, mana ana wajali wazazi wake.

  Afu huyo mwanaume kama ana adabu hata kusema hi issue asinge sema, ange nyamaza tu...mana wale wazee wamempa mtoto wao yani mke, lazima uwafanyie heshima.
   
 13. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na wewe, km kuna mawasiliano mazuri na mwanamke anapata mahitaji yake hawezi kuficha fedha, kubali kataa hatuwezi kuziacha hizi familia mtambuka(extended families) hivyo mnapokuwa katika ndoa ni vema kuangalia na mahitaji ya wanandugu wengine. Jadili talaka siyo suluhisho aangalie kosa liko wapi warekebishe.
   
 14. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  laki si pesa jamani?
  hadi talaka kisa laki?
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ukute analisha mume mwenza. . . . Kaaaazi kweli kweli.
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  Kongosho nimekupenda buuuuuuure bila senti tano,


   
 17. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu hao wote wanaonekana kwanza hawaaminiani pili wote wanatamaa ya mkwanja kwa kuwa hilo limetokea basi kama wameachana watajijua wenyewe kwani wakati wanakubaliana hawakukushirikisha..

  let them go praaaa.....
   
 18. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  muulize huyo rafiki yako huwa anawakumbuka ukweni kwake au ndo dada huyo kashaolewa mahari keshatolewa ndo kwao basi tena kama huwa anawapa fungu hapo ndo tatizo lakini kama ndo bahili ni halali yake huyo mwanamama lol.Chezea uchungu wa mzazi:attention:
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  umeona enheeee...
   
Loading...