Mdogo wangu alikuwa ananionea sana sababu I always walked away.Hehe polee.. lkn ni hivyo uwa kipindi kinafika na ngumi zinaisha. Kwani wewe umezaliwa pekeako? Maana kama una dada au kaka kupigana lazima
πππMmmh Karucee wa kwangu nao wameanza vita
Kuna muda inabidi nitafute sehemu twende angalau waone aibu.
Mvulana anampiga sana dada yake hadi huruma.
Dada naye akipata chance anamdunda na chochote.
Yaani nyumba imekuwa uwanja wa masumbwi
Hadi leo mna pigana?Mdogo wangu alikuwa ananionea sana sababu I always walked away.
Mpaka na mimi nilipoanza kumdunda hasa. Mpaka ukubwani. Na hiki ndo kinanipa wasiwasi.
Wa kwangu wanadundana nimeona waende shule wakirudi wamechokaπππ
Unanikumbusha kitambo sana na dada angu alikua mgomvi sana kisa mzee alikua anampenda na kumtetea sana, mambo ya watoto wa mwisho.
Siku moja akalianzisha nikampiga hadi akaanza kutapika, wacha huruma inijue, toka siku hiyo nikaapa sitokuja pigana nae tena na hadi leo hii sijawahi pigana, nampenda sana lito sisπ
Kudundana ni afya bwana em muwaache.Wa kwangu wanadundana nimeona waende shule wakirudi wamechoka
Ila haijasaidia ikifika muda wa kula ni ngumi, ukimtuma mmoja na mwingine anataka.
Nafikiri kuna siku nao wataacha
πππππhahaaa. Hamna bana. Mpaka sekondari tu.
Now Tupo nchi tofauti na tunapendana sana.
mpaka wanafika sekondari nishachizi kabisa.ππDaaah umenikumbusha mbali sana mimi na mdogo wangu wa kiume tunaefuatana yaani tulikuwa hivyo hivyo ni mwendo wa kudundana sana aisee hahahahah
Ila bahati nzuri shule ilituweka mbali sana hasa tulipofika sekondari (tulipishana darasa moja tu na nilimzidi miaka 2 na miezi 7 ) kila mtu anasoma mkoa wake mimi mbeya yeye tanga hahahah
Leo hii huyu jamaa ndio bestfriend wangu namba moja .
Dawa yao wakifika sekondari kila mtu akasome bweni wakija kukua watakuwa marafiki hatari