Ushauri:Nina shamba la eka 3 msata

fungi

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,539
4,671
Habari wakuu,
Mimi ni kijana niliye chuo kikuu,baba yangu amenikatia eneo la eka 3 maeneo ya msata 100m kutok barabaran
Naomba ushauri wenu ni kilimo gani kinafaa maeneo hayo na ushauri wowote una ona unafaa kwangu.
Natanguliza shukurani.
 
natafuta eneo sehemu hiyo nianzishe intensive commercial goat and sheep farming ..... nifuge mbuzi na kondoo kama 2,000 plus
 
natafuta eneo sehemu hiyo nianzishe intensive commercial goat and sheep farming ..... nifuge mbuzi na kondoo kama 2,000 plus
HV mbuzi wanalipa mie nami Nina ndoto za ufugaji kama huo. Ila naambiwa wezi, mbuzi wasumbufu. Nachoka ila najpa muda nasubiri mwaka uanze na kauli yangu itakuwa ... hapa mbuzi tu..
 
HV mbuzi wanalipa mie nami Nina ndoto za ufugaji kama huo. Ila naambiwa wezi, mbuzi wasumbufu. Nachoka ila najpa muda nasubiri mwaka uanze na kauli yangu itakuwa ... hapa mbuzi tu..

LuisMkinga .... hakuna kusichoibiwa dunia hii .... kunachotakiwa ni control ... ukifuga kama hobby utaibiwa na usijue ..... ukifuga kibiashara utafanikiwa

Mbuzi wanalipa sana .... haswa wanapopata matunzo bora kama chanjo za mgonjwa dawaza minyoo na lishe yenye virutubisho kama vile pumba za mahindi, pollard na mashudu ya alizeti .... na kuwaogesha mara kwa mara kuondoa parasites kama vile kupe ..... mbuzi huzaa mara mbilikwa mwaka na uikiwana breed ya mapacha iinatoa wawili wawili ..... kuna aina mbili nzuri za mbuzi kwa ajili ya nyama .... hizi ni Boer and Angora goats

soko la mbuzi wazuri dar ni Tsh 120,000 - 180,000 per head kutoka na na body weight
 
Last edited by a moderator:
natafuta eneo sehemu hiyo nianzishe intensive commercial goat and sheep farming ..... nifuge mbuzi na kondoo kama 2,000 plus

bei iko juu sana maeneo yale kwa sasa, nenda Mkoka au Madesa kuna maeneo mazuri. Changamoto ya Mkoka ni wanyama pori, changamoto ya Madesa ni wakulima wadogo na maji, japo maji ya bomba yapo. Madesa ni hapo hapo Msata ( kijiji cha Kihangaiko, kitongoji ndio Madesa, kinapakana na IFM compound), kuna mwenzio ana mbuzi balaa mitaa ile.

Kama uko serious, nenda Buyuni kata ya Vigwaza, maeneo yako vizuri kwa ufugaji na makubwa, na bei iko vizuri, udongo wake unaruhusu lambo na kilimo, ni eneo la wafugaji wa mifugo mbali mbali.
 
Mkuu unaonekana unataharifa muhimu lakini unazitoa kwa kifupi. Mimi nipo interested na maeneo ya kufugia yenye maji. Nimesha jaribu kufanya hii shughuli especial maeneo ya Handeni lakini changamoto yangu ni maji. Mifugo bila maji ya huhakika ni shida. Nimejitahidi na bado naendelea lakini maji ni shida. sasa nikipata maeneo yenye maji nahisi mambo yatakuwa mazuri. Naomba mkuu nikupm unipe mwanga zaidi.
 
Back
Top Bottom