[USHAURI] Nina milion 80. Naomba msaada. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

[USHAURI] Nina milion 80. Naomba msaada.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mutta, Jun 1, 2012.

 1. Mutta

  Mutta Senior Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana Jf,nimebahatika kupata million 80.Naomba msaada wa biashara gani nifanye ili nisiwe tena Maskini.
   
 2. C

  Criss Alex Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Dah! Fungua duka la vifaa vya ujenzi. Au kampuni ya kimtandao.
   
 3. H

  HAKUNA Senior Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Utaendelea kuwa maskini, kwasababu wewe ni maskini wa mawazo; haingii akili eti mpaka unapata milioni 80 hujui cha kufanya, labda umekwapua mahali;siwezi kushiriki kumwendeleza mwizi (fisadi). Kanuni ya biashara, huwa linaanza WAZO, halafu MPANGO, baadae MTAJI. Sasa wewe uliwezaje kutafuta pesa kabla ya kuwa na mpango. Mahitaji ya watu katika eneo husika ndio hugeuzwa kuwa fursa ya biashara.
   
 4. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu nadhani huja mtendea haki mtoa mada. Je kama amezipata kwa kuuza nyumba au shamba la urithi baado ni mwizi (fisadi)? Mimi nadhani wewe ndio umekurupuka bila kufikiria.
   
 5. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  mdau mbona unatoka mapovu kwa kuilalia wazi bahati ya mwenzio hujui watu wanauza nyumba kkoo huko.........kaka mi ningekishauri ungeenda kwe wataalamu wa biashara huwa wanatoa ushauri wa kibiashara kwa ujira kidogo koz kwa pesa hiyo siyo wa kushauriwa kufungua sijui uwakala au duka la pamba...maoni tu
   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,101
  Likes Received: 7,351
  Trophy Points: 280
  Kaka unaua namna hiyo.
  Hizo kanuni za kuanza Na Wazo ilishapitwa Na wakati,
  Unaweza ukaanza na Mtaji uje Mipango.
  Halafu una uhakika gani kua kaiba??
   
 7. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Duka la vifaa vya ujenzi linalipa, duka la vitu vya watoto pia linalipa sana.
   
 8. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  uza urembo,
   
 9. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Duh, Mwanangu umeiba wapi hiyo ela maana tofauti na hapo ni ya mirathi au umeipata ktk bahati nasibu. Kama alivyosema mchangiaji hapo juu haiwezekani uwe na hela yote hiyo hivi hivi, bila kutoka ktk biashara au kazi fulani.
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nunua kiwanja kwa sh. mil 15 sehemu ambayo iko accessible vizuri na gari Dar es Salaam (I suppose uko Dar). Jenga ghala la kuhifadhi nafaka kwa sh. mil 30. Chukua mil 20, ingia shamba, nunua mchele wakati wa msimu uhifadhi kwenye ghala. Msimu ukiisha anza kuuza whole sale and retail.
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Alternatively, kodisha nyumba kwa mkataba kuwa unaimodify kuwa guest house au hotel.Ukipata maeneo mazuri kama karibu na stand etc. utaingiza faida nzuri sana chini ya utawala mzuri.
   
 12. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  GOOD IDEA! Thanx.
   
 13. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  tungejua uko wapi, namaanisha mkoa au hata wilaya, au una access na maeneo gani ingekuwa rahisi zaidi kukushauri kwani fursa zinatofautiana kulingana na mahali ulipo

  lakini kama ndo kwanza umezipata, nakushauri uzitafutiea fixed account ya hata mwaka mmoja ili akili itulie kwanza, maana kiukweli ukipata hela kama hiyo bila kuwa na wazo au kutegemea, kwanza unaweweseka, na ukija kukaa sawa imebaki m10, hapo unapata frustration, ukija kujipanga zimekata na hapo ndo utakuwa maskini milele maana wansema opportunity never come twice
  lakini kama uko dar, angalia biashara ambayo unaweza kuwa na uzoefu nayo, au unaweza kuimudu kwa muda mfupi, na usijaribu kuwaamini watu au mtu yeyote katika biashara, na usijaribu kumuagiza mtu sijui dubai, au china wala singapore itakula kwako mkubwa (nina wafahamu watu zaidi ya 7 ambao wameachwa njiani kwa kuagiza au kuamini watu kwa hela nyingi)
  kwa sasa mkuu nakushauri uchukue m70 weka kabisa fixed account ya mwaka, na hiyo m10 tumia kufanya test za biashara, au kutafutia ujuzi wa biashara kama kuwaona wataalamu wa biashara, kufanya kozi fupi za ujasiriamali na kupata exposure ya biashara tofauti tofauti
  Kama utakuwa tayari unaweza kuni PM pia naweza kukusaidia kwa njia moja au nyingine (ingawa kwa sasa sipo nchini - niko Uholanzi kwa masomo ya mda mfupi - narudi mwezi wa saba, na pia ni mwl wa masomo ya biahsara katika moja ya vyuo vikuu hapo bongo) so sitahitaji ujira, wala kujua hela yako ilipo wala taarifa zako za kibenki, uwe na amani kuwa utakuwa na mtu mpenda maendeleo.
  Hongera pia kwa kupata mtaji mkuu, komaa uuzalishe maana bongo ni ngumu, na kwa kweli ni dunia nzima, maana hata huku si shwari sana
   
 14. Micha

  Micha JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wekeza kwenye Ardhi. Kama uko Dar es salaam tafute viwanja vizuri vilivyopimwa (vina hati) na ambavyo viko maeneo mazuri kama Boko, Mbweni, nk. Asume utapata kila kiwanja kwa Shs 15m, utanunua viwanja 5 na utabaki na mil 5 ya kuzungushia bar. Ukisubri kwa mwaka mmoja tu viwanja hivyo hvyo utaviuza kwa kati ya Shs 25m mpaka 30m; maana yake kwa mwaka mmoja utakuwa ume double hela yako. That is close to 100% return ukizingatia hautakuwa na running cost yoyote zaidi ya mwenyewe kwenda kuviangalia angalau mara moja kwa mwezi na kuvisafisha pale inapobidi.
   
 15. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  mkuu, hongera kwa kubahatika, pili naomba ungejieleza upo wapi? una shughuli gani? una uzoefu gani? ulishawahi kufanya biashara yoyote? binafsi ulishawahi kuwa na mawazo gani ya biashara? unapenda nini? umeoa/ kuolewa? ....... amini kuwa BIASHARA YA KUFANYA INATEGEMEA MTU NA MTU NA MAZINGIRA ALIYONAYO, SI KILA ANACHOKIFANYA MWINGINE NA WEWE UTAWEZA AMA SI KILA ANACHOSHINDWA MWINGINE NA WEWE KITAKUSHINDA.
   
 16. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Inabidi utuweke wazi kidogo ili ushauri uwe effective....kwanza wewe unaelimu/exposure ya level gani? unafanya shughuli nyingine kama ajira nk, unauzoefu na biashara gani? unapenda kufanya nini? je wewe ndio utakuwa msimamizi full time au unatarajia kumuweka mtu? unahitaji quick cash au hata longterm investment???

  Kimsingi biashara utakayo ifanya kwa mafanikio inategemea zaidi uelewa wako katika hiyo biashara na mambo mengine kama usimamizi, muda unaotumia, malengo n.k.

  Kama ni pesa tu unataka kufanya investment unaweza kuanza na hayo mambo ya ardhi ambayo hayatahitaji muda wako na pia risk ni ndogo.......kidogo kidogo unakuja kuwa guru wa real estate........

  pia kuna mambo ya kilimo na uuzaji wa vyakula, kutegemea na location yako na ujuzi na muda wako, masuala ya ku-import bidhaa in bulky kutoka uchina/hongkong/mumbai.......kimsingi inategemea upo kwenye field gani na nini unaujuzi nacho???
   
 17. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Samahani naingilia mada ya mtu hapa, lakini ningelipenda kuelewa umekusudia nini unaposema kampuni ya kimtandao? unaweza kuweka wazi zaidi, umenigusa kidogo lakini nimeshindwa kujua unakusudia nini hasa.
   
 18. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  inatosha kuingia kwenye business ya real estate.Fanya hili hutajutia hakika.
   
 19. chash

  chash JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Idea ya fixed deposit ili uweze kufikiria ni nzuri sana. Pia kuna biashara ya mpesa-tigo-airtel-zantel ambazo unaweza kuwa unazungusha hela yako na kupata faida wakati unajipanga ufanye nini. Hela yako itabaki in cash form hadi utakapo tafiti long term investment.
   
 20. c

  chakarikamkopo Member

  #20
  Jun 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ili uwe na uhakika na return nzuri, hebu nikopesha hizo pesa kwa riba nzuri nzuri tu....15%- 17% mimi nitakuwa nakulipa kila mwezi. Biashara yangu mimi nikutoa mikopo midogo midogo.
   
Loading...