Ushauri: Nimwachie au nimpambanie mtoto wangu

Ushauri: Nimwachie au nimpambanie mtoto wangu

Pole
Yamkini huyo babymama Ana stress na Hana wa kumsaidia
Ameona mtoto amekuja amependeza kwahiyo anataka amchukue ili aendelee kuwa karibu na wewe ili apate child support
Cha kufanya kamchukue mtoto hata kwa kutumia polisi...maana hapo anayeteseka ni mtoto kwa ajili ya matatizo yenu nyie wazazi
 
Aisee wee jamaa bwege kweli. Mwanamke alishakubwaga kisa huna ndalama...iweje umuamini kumpa mtoto wako ata kama ni likizo?

Huyo ni kumwambia mtoto mama yako ni mshenzi tena shetani kabisa usiwe karibu nae wee tulia hapa na dingi
 
Kosa lilianzia kwako kwa kujifanya muungwana kwamba unampa mtoto akasalimie mama yake wakati wa likizo.
Wanaume tunafanyaga hivi......
1. Chukua mtoto wako ili ukamlee mwenyewe.
2. Usikubali kulelewa mwanao na mwanaume mwingine, maana akikua mkubwa atakua mtoto wako lakini mwenye tabia za baba mwingine (hauto mfurahia).
3. Marufuku mtoto kwenda tena kwa mama yake wakati wa likizo maana mama wahivyo lazima ataanza kumjaza mwanao maneno mabaya na taratibu ujinga wa mama yake utahamia kwenye akili ya mtoto wako.
4. Achana na uzungu wa kusema sijui mtoto asalimiane na mama yake kwenye sim, ni marufuku hadi mtoto mwenyewe atakapo jitambua na ataanza kwenda kumsalimia mama yake kwa utashi wake mtoto mwenyewe.
Mwisho ingawa sio kwa ulazima ni kwamba.....Usiwasomeshe watoto wako ili wawe matajiri, bali wafundishe kumjua Mungu, kwa njia hiyo watakuwa na furaha ya kweli. Na kwa jinsi hiyo, watakapokuwa wakubwa watajua thamani ya vitu na sio bei.
 
Nilikua na mahusiano na mwanamke tukajaaliwa kupata mtoto mmoja saivi ana miaka 10. Nilitoa mahari na hatukufikia ndoa, ila mahusiano yakaishia njiani baada ya mimi kuyumba kiuchumi/kupoteza kazi. Mwanzoni mtoto alilelewa na mama yake na alimng'ang'ania kwani tulikua tunaishi mikoa tofauti.

Maisha yakaja kumpiga na mtoto akashindwa kumsomesha akampeleka mara boarding mara kwa wazazi wake mara kumrudisha darasa etc. na mtoto akakosa stability akiwa bado mdogo. Mimi nilitumia nguvu nyingi mtoto nikamchukua kwa nia ya kupata elimu nzuri kwani mambo yangu hayakua mabaya.

Nimemsomesha kwa miaka mitatu na likizo tulikubaliana amchukue akasalimie upande wa mama yake, nikakubali. Cha ajabu akanibadilikia na akakataa kumrudisha mtoto shule zilipofunguliwa mwezi July. Akamtafutia shule mkoa anapoishi bila kufanya uhamisho usio rasmi. Nimejaribu mbinu zote ikiwemo kuzuia uhamisho wa mtoto (ambao unafanyika kupitia system) ili mtoto amalizie mwaka huu naona mama yake wala hashtuki na amekomalia kumsomesha mkoa aliyoko na vitu vyote vya mtoto viko kwangu ameacha.

Jambo kubwa huyu mwanamke hajafanikwia kupata mtoto mwingine, na hata matumizi by then nlikua nikituma sidhani kama yalikua yanafika kwa mtoto. Ninasikitika kuwa tabia yake ya sasahivi sio kama nlivyomfahamu (kunywa pombe, kuvaa vibaya etc) na inawezekana ikamu affect mtoto wa kike ambaye japo ni mdogo.

Wakuu, Niendelee kumpambania nimsomeshe niweze kwa kukaa naye au nimwache akae na mama yake. Maana sina hakika kama atapata elimu nzuri na makuzi akiwa bado mdogo. Mimi now nina familia yangu na nadhani niko kwenye stability ya kum monitor mtoto vizuri kitabia, kielimu na katika ukuaji.

Nahitaji mawazo
Nenda ustawi wa jamii,watakupa maelekezo mazuri ya nini cha kufanya,inawezekana hata ikaamriwa umchukue mtoto...
 
Mimi siwezi kugombea mtoto na mama yake nitafanya sehem yangu ikishindikana namwachia tu mtoto akiwa mkubwa huwa hapotei baba yake
 
Ulisema huyo binti ulikua unakaa naye? Anhaaaa sawa!

Angalia namna ya kumsaidia mtoto pia uwe unamkumbuka mama mtu hata kias flan Cha pesa baada ya mda flan inaonekana kama yupo frustrated
 
Mimi siwezi kugombea mtoto na mama yake nitafanya sehem yangu ikishindikana namwachia tu mtoto akiwa mkubwa huwa hapotei baba yake
Samahani mkuu.....
Utajiskiaje wewe kama baba kwa kuto kuonyesha juhudi za kumchukua mwanao (sio kumgombea), then akaja akapata malezi ya baba mwingine.... na kisha akaja kurudi kwako akiwa na tabia zingine kabisa na mitazamo hata mawazo tofauti kabisa na yakwako...??
 
Ulisema huyo binti ulikua unakaa naye? Anhaaaa sawa!

Angalia namna ya kumsaidia mtoto pia uwe unamkumbuka mama mtu hata kias flan Cha pesa baada ya mda flan inaonekana kama yupo frustrated
Hivi inawezekana vipi kumbadilisha mtu mlie kutana nae ukubwani tena alie lelewa tofauti kabisa na wewe..!!
Huyo kama hakufundishwa na wazazi wake na kisha jamaa akajaribu kwa sehem yake akashindwa, basi amteme akafundishwe na dunia.
By the way, kumsaidia kwa viposho mzazi mweza mlie achana kwa ubaya nisawa na kujisogoza karibu na matatizo.
Binafsi iliwahi kunitokea, tena hua wanajua kutegesha na kulipua bila huruma maana tayari wanakua wanaona hawana cha kupoteza.
 
Aisee wee jamaa bwege kweli. Mwanamke alishakubwaga kisa huna ndalama...iweje umuamini kumpa mtoto wako ata kama ni likizo?

Huyo ni kumwambia mtoto mama yako ni mshenzi tena shetani kabisa usiwe karibu nae wee tulia hapa na dingi
wewe ndo lipumbavu likubwa...ugomvi na mzazi mwenzako unakimbilia kulialia kwa mtoto....ugomvi wa wazazi usipeleke kwa watoto, mjinga mkubwa ww.....munakua visogo tu, huku akili mmezidumaza..... stupid
 
ila pia upande mwingine je huyo mtoto unaishije naye? huenda anateseka kwa njia moja au nyingine, huenda mwenza uliyenaye anamtesa mtoto umejaribu kuchunguza?
ila pia hawa watoto wanakuwaga na kasumba moja ya kuongelea vibaya upande wa pili hata kama hateseki mf anaweza kuwa anafundishwa kazi yeye akaona anateseka akienda kwa mama yake anaenda kuongea vitu negative

fanya uchunguzi mkuu
 
Ni ngumu sana kushauri jambo kwa kuskiliza upande moja
 
Back
Top Bottom