Watu wa ukumbi huu natumai muko poa sana.
Mwanzo wangu wa kuingia katika mapenzi nilikuwa na mpenzi wangu 1 tu ambaye tulipendana sana na ukweli sikupenda kufanya naye kwa sababu nilimtegemea kwa 100% kuja kuwa mke wangu sikupenda kuwa na haraka kula lile tunda.
Wakati tumo katika mahusinao ya urafiki wa mapenzi kikawaida kwao kupitia wazee wake alitokea mume kuja kumposa., lakini lazima niseme huyu aliyekuja ni maji marefu anaishi mamtoni kule kule kwao Trump (U.S.A). wazee wa huyu mtoto wakapata tamaa sana wakamforce yule mtoto na kumkimbiza dar es salaam na kumfanyia safari bila kujijuwa kumbe anaenda kuolewa., akaolewa.
Niliumia na kuteseka sana kwa mawazo lakini rafki zangu wakanipa moyo sana nikarud hali ya kawaida baada ya mda., Nikakaa nikapata shori jengine kuliko lile la Trump, tukapanga maisha tukakubaliana tuoane lakini baada mda mdogo ikatokezea na yeye akaolewa., Nikaendelea kuvuta subra.
Nikaja nikapata mtoto mkali tena lakini huyu alikuwa mtoto wa chuo (msomi) sasa uzalendo ukawa unanishinda nikaanza kula lile tunda ili nisije kukosa kama wale wa mwanzo., lakini naye pia nikaja nikagundua ana matatizo siko peke yangu si mnajuwa tena mtoto yuko chuo mbali na mimi niko mbali mpaka likizo akija au nikienda ndio tunakuwa pamoja. Nikaachana naye kumpa fursa zaidi mwenzangu.
kutoka hapo nikaja nikapata tena shori la maana tena lakini huyu tulikaa kama mwezi tu naye akaolewa kwa kweli sasa nikaanza kuchanganyikiwa.
Akili yangu sasa ikanipa bora kuanzia sasa nisiwe na mmoja tu bora nitengeneze kama 3 ivi or 4 ili mmoja au wawili wakichopoka mmoja niko naye au wawili niko nao mapaka maisha yangu yanakuwa sawa naowa 1 tu.
Sasa Mtihani ulipo ndugu wa ukumbi huu ni kwamba muda wa KUOA umefika yaani hivi sasa na ukweli ni kwamba wapo 4 jumla yao na wote ni mapenzi motomoto hakuna anayepepesa macho wote wananipenda sana na mimi nawapenda ingawa kwa ufundi wangu hakuna ata mmoja anayejuana na mwenzake kila mmoja anajiona yuko peke yake.
Ukweli ni kwamba uwezo wangu kwa sasa ni kuoa mmoja tu. Na nimejaribu kufanya mbinu wale wengine nigombane nao ata kwa sababu nduchu tu ili iwe sabab niachane nao lakini hawakasiriki wala chochote bado wameniganda kama rubaa.
Nimeleta hapa naomba ushauri nini nifanye wadau wa mtandao huu. Nataka nioe mmoja tu lakini pia nahofia je hawa wengine wakijuwa nimeoa salama itakuwepo? utulivu utakuwepo? nina hofu sana.
Natanguliza shukurani.