Jamani mwenzenu niko njia panda,yapata Mwaka sasa niko kwenye mahusiano na mdada fulani jina nitasema badae, jamani nampenda sana nae pia kiukweli ananipenda mno si kidogo, ila sasa amekuwa na tabia fulani ya kusema uongo wa vitu vidogo vidogo mfano amaweza kuwa yuko nyumbani akadanganya yuko kwenye Daladala huku unasikia mazingira yanaonesha siyo kwenye Gari ila yapo matukio mengi anakuwa anadanya ila ukimbana kidogo anakueleza ukweli na kuomba msamaha.
Shida imeanza leo baada ya kuwa amedanganya kaenda mahali afu akawa amerudi Nyumbani nilipompigia Simu kaanza uongo wake mara nipo kwenye Daladala sasa shisa ni kwamba mazingira ya kwao nayaelewa sana, nikaa nambishia baada ya kama dakika tatu za mabishano akaadimit na kukubali yupo home na kumuuliza anafanya hivyo akadai hana jibu.
Kwakweli nilichukia nikaamua kumtolea uvivu nilimpa masharti kadhaa na ili ayalidhi moja ilikuwa aniambie sababu ya kuwa muongo kwa vitu vya kijinga. Baada ya kuona yamekuwa makubwa akaamua kufunguka na sababu zake ni hizi:
1) Kwanza ili mchukua muda ila mwisho kasema kwa huzuni sana kuwa yeye ni mgonjwa( Sickle cell), unamfanya apende kudanganya ili kwasababu watu wa namna hii wanatabia ya kuogopa kutokubaliwa au kutojiamini muda wote.
2) Sababu ya pili kasema huwa ajui anachosema kama kitanikwaza sana, kwahiyo yeye anavyona hakuna tatizo, mimi nachukia.
Sasa waungwana wanajamvi embu nielezeni kuna uhusiano kati ya kuongopa na Sickle cell? Pili hii habari imenichanganya sana, nawaza nimwache maana huu ugonjwa ni mkubwa na si wakiza kimoja na pia nimesoma kwenye mtandao matunzo ya mtu wa sickle cell ni ghali sana! lakini hata muda wake wa kuishi ni akibahatika kuvuka 18 ni limit 50yrs.
Hapa nilipo nimechanganyikiwa sijui ata nifanyeje yeye kwasasa yupo 21, kama kuna mtu uelewa nisaidieni ameniambia hii siri baada yakuwa amelia sana. Na amevunja agano la mama yake alimwambia asije mweleza mtu ambaye ajui hili tatizo naona hofu ya mama yake ni kwamba mwanae atakosa mwanaume wa kumuoa na kanitishia nikimwacha anakunywa sumu. Nimeanza naye mapenzi alikuwa bado ajajua mwanaume nampenda Avemaria nifanyaje.