Ushauri: Nimeshindwa kuvumilia hii dhuluma

Miss chagga pesa na rafiki ni vitu vi 2 tofauti kabisa!!!usimwamini mtu yeyeto hata awe ndugu yako pesa pesa zinauwa undugu na urafiki!!!mi namwa mini mama yangu tu!!! Cha msingi we mlipe mdogo wako hiyo pesa yake!!!then kata mazoea na huyo!!!kulikuwa na ushahidi ulipo mpa hiyo pesa au mlienda kupeana chumbani mdogo wangu!!!?
Wengi sijui wanawekaje u rafiki na pesa aisee... Kama unampa mpe na usahahu . amlipe tu Mdogo wake
 
Nina rafiki zangu wawili huwa tunakopeshana hela for years na hatujawahi kudhulumiana hata thumni. Any time one of them akiwa na shida, kama ninayo Natoa tu fasta na me nikiwa na shida wananisaidia fasta. Ila kilichonishinda kabisa ni kwenda kumkopea mtu hela kwa mtu wangu mwingine, yani hata awe na shida ya vipi, kama mimi binafsi sina, namwambia tu ma "I'm broke". Bora ipotee hela yangu kuliko hela ya mtu mwingine kwa dhamana yangu, hapana mwee. Utamkopea mtu hela kubwa ambayo hata wewe uwezo nayo huna, nina allergy na pressure akhaaa
 
Ki ukweli pesa na ubinadamu ni kitu kingine!! Mi the wey nilivyo na uchungu na maisha halafu mtu adhulum hata elfu 1,tutapambana mbaya!!!fanya utani na mimi ila usifanye utani na pesa yangu,
 
Quote "Ilipotimia miezi mitatu nikamuuliza ndugu vipi hela ya watu ulisema utarejesha baada ya miezi mitatu na muda umeshafika,inakuaje bado?Akanijibu biashara aliyoibuni ilimpatia hasara hivyo sehemu kubwa ya mtaji ikawa imekata,Dahhh!'

Wala mwanzoni hakuwa na nia ya kukudhulumu. Elewa biashara ina uncertainty nyingi sana hasa ikichangiwa na ukosefu wa uzoefu. Alivyotarajia imekuwa sivyo na cha kukulipa hana ndio maana anapiga chenga. hata ukimchukulia hatua hawezi kukulipa maana hana. Wewe mlipe kidogo kidogo mdogo wako na huyo jamaa akipata huko mbeleni aje kukulipa lakini ni ngumu sana kuweza kupata faida ya milioni mbili baada ya kutoa gharama katika shughuli nyingine atakayofanya labda aajiliwe.

Biashara halali Tanzania faida yake ni ndogo sana.

Ulikosea sana kumkopea hizo pesa.
 
Jamani tapeli utamjua oh!!biashara haikuenda vizuri mara mtaji umekata hapo ni shetani alikuwa anamwingia taratibu ili arushe pesa za watu!!kwanza nimeshikwa na hasira utadhani ni yangu hiyo pesa!!!sijui kwa nn hatui waungwana kwenye huu ulimwengu wa kutafuta
 
Imeniumiza sana maana ni mtu ambaye hata wazazi wanamfahamu, na kitendo hiki kimeshanipotezea imani kwa wadau/wawezeshaji...
 
Mana yaweza ikawa mdogo wangu kuna kitu kingine ulikuwa unategemea ndo mana akasepa na hiyo 2 milion
Sikuhitaji reward yoyote dada, ilikuwa sehemu ya kumsaidia shida yake na ndiyo maana hakupewa riba ya marejesho...
 
Kusaidia!!!!! au ww ni UNHCR!!! Unasaidia hadi 2 milion!!jamani ningutana na wewe ningekopa 20 milion nisepe zangu mana unaonekana ww ni mtu wa huruma sana!
 
Tatizo nilimuamini na sikuyategemea yote haya dada yangu, kinachonisikitisha zaidi hata kulipa kwa installments kashindwa na kafikia hatua ya kutopokea simu yangu na hapatikani hewani.....
 
Kabla ya Yote Niwatakie Heri ya Sikuu ya PASAKA wanaJF.

Nipo hapa kwa ombi la kuhitaji ushauri kutokana na kisa kifuatacho ambacho kimenisibu mimi mwenzenu.

Nina rafiki yangu wa kiume ambaye nimesoma naye shule moja ya sekondari, A-Level.

Katika miaka yote ya masomo ya a level tumekuwa tukisaidiana katika kila hali,kuanzia masomoni mpaka katika maisha ya kawaida mathalan masuala ya kiuchumi, amekuwa rafiki ambaye tumekuwa tukishirikishana siri zetu nyingi na changamoto mbalimbali hata baada ya kumaliza masomo yetu ya sekondari na baada ya kila mtu kuingia mtaani kuyasaka maishana kujiunga na elimu ya chuo kikuu.

Katika wakati wa masomo ya chuo kikuu tumekuwa tukisoma mikoa miwili tofauti kwa hiyo tulikuwa tukikutana nyakati za likizo pekee au kama kuna matukio ya dharura ambayo yananilazimu kuja Dar wakatimimi nikiwa chuo mkoani.

Ilifikia kipindi rafiki yangu alitembeleamkoani kwetu na kwa sababu alikuwa mtu wangu wa karibu sana na nilimuamini, hivyo nilimchukulia kama ndugu hivyo sikusita kumtambulisha kwa wazazi ili wamtambue na nikawaeleza wazazi huyu ndiye rafiki pekee tunayeshirikiana kwa kila jambo tunapokuwa mjini.

Sasa miezi michache iliyopita aliniazima kiasi cha fedha, Milioni 2 kuna shughuli ameipata na tatizo limekuwa mtaji, bila kusita kwa sababu ni mtu wangu wa karibu sikupata mashaka naye maana hajawahi kuniangusha, kwa sababu wakati huo nilikuwa masomoni nikamuambia kwa wakati huo nisingeweza kuwa na fedha hizo ila nikamuahidi kumuazimia kwa mtu mwingine kwa wakati, hazikupita sikumbili nikapata hizo Milioni mbili taslim kutoka kwa ndugu yangu wa damu ambaye aliniuliza fedha za nini hizi wakati unasoma au ni ada? nikamjibu hapana bali kuna rafiki yangu ana shida nazo nami namuamini atazirejesha kwa wakati utakaonipa, alijaribu kusita nikamtoa wasiwasi na nikamuahidi fedha zake zitakuwa salama.

Aliponikubalia basi nikampatia namba za M-PESA akamtumia huyu rafiki yangu moja kwa moja na muda si mrefu jamaa akanihajikishia amezipokea na akashukuru sana.

Huyu rafiki yangu alinihakikishia ndani ya miezi mitatu pesa yote itakuwa imerejeshwa, nikamuuliza ana uhakika? akanijibu nisiwe na wasiwasi na miezi mitatu akasema nimingi sana.

Nikamuambia atimize ahadi yake ili niendelee kulinda uaminifu na heshima yangu kwa mdogo wangu.

Ilipotimia miezi mitatu nikamuuliza ndugu vipi hela ya watu ulisema utarejesha baada ya miezi mitatu na muda umeshafika,inakuaje bado?Akanijibu biashara aliyoibuni ilimpatia hasara hivyo sehemu kubwa ya mtaji ikawa imekata,Dahhh!

Nikamuuliza sasa inakuwaje na muhusika anahitaji pesa yake kuna mambo yake anataka afanye na ukizingatia alitupatia bila riba yoyote?Akaniomba aongezewe muda, nilipozungumza na mdogo wangu alinielewa ila akanisihi sana isikute pesa nimetoa kwa matapeli, nikamueleza hapana kwani muhusikahata nyumbani alishafika na wazazi wanamfahamu.

Akanijibu sawa kishingo upande.Jamaa akaongezewa miezi miwili zaidi bado akashindwa kutoa pesa.

Akawa bado analia mtaji umekata wote lakini nikajaribu kudodosa kwa watu aliokuwa anashirikiana nao wakanijibu ni kweli jamaa kapata hasara lakini siyo kwamba hana kitu cha kutoa hata kupunguza deni.

Baada ya kuona Kuna harufu ya ujanja ujanja nikamsihi mdogo wangu anipe muda niweze kumshughulikia huyu jamaa hela irudi baada ya kuchoka kupokea ahadi hewa kila siku.

Nilimsihi awe anapunguza deni kwa awamu mpaka liishe, akanikubalia naakasema kwa hapo nitakuwa nimemsaidia sana na ataanza kurejesha muda siyo mrefu, wakati huo nafanya mawasiliano naye nikiwa bado chuoni.

Sasa nimemaliza chuo narudi mtaanikumfuatilia baada ya kushindwa kupunguza hata shilingi mia kwenye Milioni mbili alizopokea.

Picha anazonichezea ni kwamba yupo safarini mikoani kila siku na chuo alishaacha, wakati mwingine hata simu yangu hapokei na hapatikani hewani mara nyingine.

Nimejaribu kufuatilia kwanini ananifanyia huu uhuni wakati sijawahi kumfanyia dhuluma yoyote nakosa majibu.

Nimepata taarifa pia kuna rafiki zake wengine wanalia wamedhulumiwa pesa pia.Ilifikia wakati nikamwambia nitalifikisha hili suala kwa ndugu zake aliokuwa akiishi nao lakini haonekani kutingishika na wala hajalikwani nasikia hata ndugu zake ameshawatapeli pia.

Sasa kero zaidi ni kutoka kwa mdogo wangu ambaye ndiye mwenye pesa imefikia wakati kapoteza imani kabisa na mimi na ananiona kama nimeshirikiana na rafiki yangu kumtapeli, kafika mbali zaidi kwani kasema anataka alifikishe suala hili kwa wazazi ili wazungumze na mimi jambo ambalo naona litaleta shida zaidi na litaleta mgogoro katika familia yetu.

Wakuu naombeni niishie hapo nisiwachoshe,naomba mnisaidie mkakati wa namna ya kumkabili huyujamaa na hatimaye pesa alizoazimwaaweze kuzirejesha kwani umeshapitamwaka na nusu sasa hajarejesha hata shilingi kumi.

Natanguliza shukrani.
 
Pole sana kwa majanga,nakushauri utumie njia za kisheria zaidi kama umehisi anataka kukutapeli hususan unaweza kwenda kumfungulia kesi ya wizi wa kuaminiwa(false pretence), lakini kabla hujafungua kesi hiyo ukumbuke kuwa lazima uwe na ushahidi/vielelezo vya kutosha vya kuthibitisha kuwa kulikuwa na makubaliano ya kumkopesha fedha hizo(mfano barua au nakala zozote za makubaliano) la sivyo jamaa itakuwa rahisi kukukana popote pale kwan atakubana kwa kutaka ushahidi ili akushinde vile vile mahakama itataka utoe vielelezo kama hivyo ili kuthibitisha.Tahadhari yangu kwako ni kwamba kama ulimkopesha pesa hizo tu bila maandishi au uwepo wa mashahidi wowote utapoteza haki yako kiurahisi.Pia nakushauri kuwa usije muamini tena mtu hata awe rafiki ako vipi kwan wapo ndugu wa damu wanadhulumiana sembuse wewe na yeye rafiki ako pia naamin utakuwa umejifunza kuwa makini na marafiki na umetupa somo sisi sote wana JF kwa ujumla.
 
Kabla ya Yote Niwatakie Heri ya Sikuu ya PASAKA wanaJF.

Nipo hapa kwa ombi la kuhitaji ushauri kutokana na kisa kifuatacho ambacho kimenisibu mimi mwenzenu.

Nina rafiki yangu wa kiume ambaye nimesoma naye shule moja ya sekondari, A-Level.

Katika miaka yote ya masomo ya a level tumekuwa tukisaidiana katika kila hali,kuanzia masomoni mpaka katika maisha ya kawaida mathalan masuala ya kiuchumi, amekuwa rafiki ambaye tumekuwa tukishirikishana siri zetu nyingi na changamoto mbalimbali hata baada ya kumaliza masomo yetu ya sekondari na baada ya kila mtu kuingia mtaani kuyasaka maishana kujiunga na elimu ya chuo kikuu.

Katika wakati wa masomo ya chuo kikuu tumekuwa tukisoma mikoa miwili tofauti kwa hiyo tulikuwa tukikutana nyakati za likizo pekee au kama kuna matukio ya dharura ambayo yananilazimu kuja Dar wakatimimi nikiwa chuo mkoani.

Ilifikia kipindi rafiki yangu alitembeleamkoani kwetu na kwa sababu alikuwa mtu wangu wa karibu sana na nilimuamini, hivyo nilimchukulia kama ndugu hivyo sikusita kumtambulisha kwa wazazi ili wamtambue na nikawaeleza wazazi huyu ndiye rafiki pekee tunayeshirikiana kwa kila jambo tunapokuwa mjini.

Sasa miezi michache iliyopita aliniazima kiasi cha fedha, Milioni 2 kuna shughuli ameipata na tatizo limekuwa mtaji, bila kusita kwa sababu ni mtu wangu wa karibu sikupata mashaka naye maana hajawahi kuniangusha, kwa sababu wakati huo nilikuwa masomoni nikamuambia kwa wakati huo nisingeweza kuwa na fedha hizo ila nikamuahidi kumuazimia kwa mtu mwingine kwa wakati, hazikupita sikumbili nikapata hizo Milioni mbili taslim kutoka kwa ndugu yangu wa damu ambaye aliniuliza fedha za nini hizi wakati unasoma au ni ada? nikamjibu hapana bali kuna rafiki yangu ana shida nazo nami namuamini atazirejesha kwa wakati utakaonipa, alijaribu kusita nikamtoa wasiwasi na nikamuahidi fedha zake zitakuwa salama.

Aliponikubalia basi nikampatia namba za M-PESA akamtumia huyu rafiki yangu moja kwa moja na muda si mrefu jamaa akanihajikishia amezipokea na akashukuru sana.

Huyu rafiki yangu alinihakikishia ndani ya miezi mitatu pesa yote itakuwa imerejeshwa, nikamuuliza ana uhakika? akanijibu nisiwe na wasiwasi na miezi mitatu akasema nimingi sana.

Nikamuambia atimize ahadi yake ili niendelee kulinda uaminifu na heshima yangu kwa mdogo wangu.

Ilipotimia miezi mitatu nikamuuliza ndugu vipi hela ya watu ulisema utarejesha baada ya miezi mitatu na muda umeshafika,inakuaje bado?Akanijibu biashara aliyoibuni ilimpatia hasara hivyo sehemu kubwa ya mtaji ikawa imekata,Dahhh!

Nikamuuliza sasa inakuwaje na muhusika anahitaji pesa yake kuna mambo yake anataka afanye na ukizingatia alitupatia bila riba yoyote?Akaniomba aongezewe muda, nilipozungumza na mdogo wangu alinielewa ila akanisihi sana isikute pesa nimetoa kwa matapeli, nikamueleza hapana kwani muhusikahata nyumbani alishafika na wazazi wanamfahamu.

Akanijibu sawa kishingo upande.Jamaa akaongezewa miezi miwili zaidi bado akashindwa kutoa pesa.

Akawa bado analia mtaji umekata wote lakini nikajaribu kudodosa kwa watu aliokuwa anashirikiana nao wakanijibu ni kweli jamaa kapata hasara lakini siyo kwamba hana kitu cha kutoa hata kupunguza deni.

Baada ya kuona Kuna harufu ya ujanja ujanja nikamsihi mdogo wangu anipe muda niweze kumshughulikia huyu jamaa hela irudi baada ya kuchoka kupokea ahadi hewa kila siku.

Nilimsihi awe anapunguza deni kwa awamu mpaka liishe, akanikubalia naakasema kwa hapo nitakuwa nimemsaidia sana na ataanza kurejesha muda siyo mrefu, wakati huo nafanya mawasiliano naye nikiwa bado chuoni.

Sasa nimemaliza chuo narudi mtaanikumfuatilia baada ya kushindwa kupunguza hata shilingi mia kwenye Milioni mbili alizopokea.

Picha anazonichezea ni kwamba yupo safarini mikoani kila siku na chuo alishaacha, wakati mwingine hata simu yangu hapokei na hapatikani hewani mara nyingine.

Nimejaribu kufuatilia kwanini ananifanyia huu uhuni wakati sijawahi kumfanyia dhuluma yoyote nakosa majibu.

Nimepata taarifa pia kuna rafiki zake wengine wanalia wamedhulumiwa pesa pia.Ilifikia wakati nikamwambia nitalifikisha hili suala kwa ndugu zake aliokuwa akiishi nao lakini haonekani kutingishika na wala hajalikwani nasikia hata ndugu zake ameshawatapeli pia.

Sasa kero zaidi ni kutoka kwa mdogo wangu ambaye ndiye mwenye pesa imefikia wakati kapoteza imani kabisa na mimi na ananiona kama nimeshirikiana na rafiki yangu kumtapeli, kafika mbali zaidi kwani kasema anataka alifikishe suala hili kwa wazazi ili wazungumze na mimi jambo ambalo naona litaleta shida zaidi na litaleta mgogoro katika familia yetu.

Wakuu naombeni niishie hapo nisiwachoshe,naomba mnisaidie mkakati wa namna ya kumkabili huyujamaa na hatimaye pesa alizoazimwaaweze kuzirejesha kwani umeshapitamwaka na nusu sasa hajarejesha hata shilingi kumi.

Natanguliza shukrani.

Pole sana ndugu!

Ukweli ni kwamba ulifanya kosa na usijelirudia kumwamini mtu yeyote juu ya pesa, kosa ulilolifanya ni kumwamini rafiki yako 100% hadi inafika point unamwazimia pesa kubwa namna hiyo kwa ndugu.

ushauri:
1. Nenda ulipoti polisi juu ya utapeli huo, hii itakusaidia kuweka ushahidi wa kimaandishi coz makubaliano yenu ni ya mdomo tu.
 
Itakuwa ushadhulumiwa, tafuta namna ya kumlipa ndugu yako hela yake hata ukimpeleka polisi/mahakamani haisaidii kitu maana mdaiwa hafungwi badala yake ataambiwa akulipe taratibu kulingana na kipato chako kwa waweza jikuta jamaa anakulipa elf 5 kwa mwenzi endapo km kipato alichonacho ni mgogoro.
 
Duuh,pole sana mkuu....usimwamini kila mtu especcially katika suala la kupeana/kukopeshana pesa.

Namimi kwa kupitia mada hii nimejifunza
 
Back
Top Bottom