Ushauri: Nimeshindwa kuvumilia hii dhuluma

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,691
22,712
Kabla ya yote niwatakie heri ya sikuu ya pasaka wanaJF.

Nipo hapa kwa ombi la kuhitaji ushauri kutokana na kisa kifuatacho ambacho kimenisibu mimi mwenzenu.

Nina rafiki yangu wa kiume ambaye nimesoma naye shule moja ya sekondari, A-Level.Katika miaka yote ya masomo ya a level tumekuwa tukisaidiana katika kila hali,kuanzia masomoni mpaka katika maisha ya kawaida mathalani masuala ya kiuchumi, amekuwa rafiki ambaye tumekuwa tukishirikishana siri zetu nyingi na changamoto mbalimbali hata baada ya kumaliza masomo yetu ya sekondari na baada ya kila mtu kuingia mtaani kuyasaka maishana kujiunga na elimu ya chuo kikuu.

Katika wakati wa masomo ya chuo kikuu tumekuwa tukisoma mikoa miwili tofauti kwa hiyo tulikuwa tukikutana nyakati za likizo pekee au kama kuna matukio ya dharura ambayo yananilazimu kuja Dar wakatimimi nikiwa chuo mkoani.

Ilifikia kipindi rafiki yangu alitembeleamkoani kwetu na kwa sababu alikuwa mtu wangu wa karibu sana na nilimuamini, hivyo nilimchukulia kama ndugu hivyo sikusita kumtambulisha kwa wazazi ili wamtambue na nikawaeleza wazazi huyu ndiye rafiki pekee tunayeshirikiana kwa kila jambo tunapokuwa mjini.

Sasa miezi michache iliyopita aliniazima kiasi cha fedha, Milioni 2 kuna shughuli ameipata na tatizo limekuwa mtaji, bila kusita kwa sababu ni mtu wangu wa karibu sikupata mashaka naye maana hajawahi kuniangusha, kwa sababu wakati huo nilikuwa masomoni nikamuambia kwa wakati huo nisingeweza kuwa na fedha hizo ila nikamuahidi kumuazimia kwa mtu mwingine kwa wakati, hazikupita sikumbili nikapata hizo Milioni mbili taslim kutoka kwa ndugu yangu wa damu ambaye aliniuliza fedha za nini hizi wakati unasoma au ni ada? nikamjibu hapana bali kuna rafiki yangu ana shida nazo nami namuamini atazirejesha kwa wakati utakaonipa, alijaribu kusita nikamtoa wasiwasi na nikamuahidi fedha zake zitakuwa salama.

Aliponikubalia basi nikampatia namba za M-PESA akamtumia huyu rafiki yangu moja kwa moja na muda si mrefu jamaa akanihajikishia amezipokea na akashukuru sana.

Huyu rafiki yangu alinihakikishia ndani ya miezi mitatu pesa yote itakuwa imerejeshwa, nikamuuliza ana uhakika? akanijibu nisiwe na wasiwasi na miezi mitatu akasema nimingi sana.

Nikamuambia atimize ahadi yake ili niendelee kulinda uaminifu na heshima yangu kwa mdogo wangu.Ilipotimia miezi mitatu nikamuuliza ndugu vipi hela ya watu ulisema utarejesha baada ya miezi mitatu na muda umeshafika,inakuaje bado?Akanijibu biashara aliyoibuni ilimpatia hasara hivyo sehemu kubwa ya mtaji ikawa imekata,Dahhh!

Nikamuuliza sasa inakuwaje na muhusika anahitaji pesa yake kuna mambo yake anataka afanye na ukizingatia alitupatia bila riba yoyote?Akaniomba aongezewe muda, nilipozungumza na mdogo wangu alinielewa ila akanisihi sana isikute pesa nimetoa kwa matapeli, nikamueleza hapana kwani muhusikahata nyumbani alishafika na wazazi wanamfahamu.

Akanijibu sawa kishingo upande.Jamaa akaongezewa miezi miwili zaidi bado akashindwa kutoa pesa.Akawa bado analia mtaji umekata wote lakini nikajaribu kudodosa kwa watu aliokuwa anashirikiana nao wakanijibu ni kweli jamaa kapata hasara lakini siyo kwamba hana kitu cha kutoa hata kupunguza deni.

Baada ya kuona kuna harufu ya ujanja ujanja nikamsihi mdogo wangu anipe muda niweze kumshughulikia huyu jamaa hela irudi baada ya kuchoka kupokea ahadi hewa kila siku.Nilimsihi awe anapunguza deni kwa awamu mpaka liishe, akanikubalia na akasema kwa hapo nitakuwa nimemsaidia sana na ataanza kurejesha muda siyo mrefu, wakati huo nafanya mawasiliano naye nikiwa bado chuoni.Sasa nimemaliza chuo narudi mtaanikumfuatilia baada ya kushindwa kupunguza hata shilingi mia kwenye Milioni mbili alizopokea.

Picha anazonichezea ni kwamba yupo safarini mikoani kila siku na chuo alishaacha, wakati mwingine hata simu yangu hapokei na hapatikani hewani mara nyingine.Nimejaribu kufuatilia kwanini ananifanyia huu uhuni wakati sijawahi kumfanyia dhuluma yoyote nakosa majibu.

Nimepata taarifa pia kuna rafiki zake wengine wanalia wamedhulumiwa pesa pia.Ilifikia wakati nikamwambia nitalifikisha hili suala kwa ndugu zake aliokuwa akiishi nao lakini haonekani kutingishika na wala hajalikwani nasikia hata ndugu zake ameshawatapeli pia.

Sasa kero zaidi ni kutoka kwa mdogo wangu ambaye ndiye mwenye pesa imefikia wakati kapoteza imani kabisa na mimi na ananiona kama nimeshirikiana na rafiki yangu kumtapeli, kafika mbali zaidi kwani kasema anataka alifikishe suala hili kwa wazazi ili wazungumze na mimi jambo ambalo naona litaleta shida zaidi na litaleta mgogoro katika familia yetu.

Wakuu naombeni niishie hapo nisiwachoshe,naomba mnisaidie mkakati wa namna ya kumkabili huyu jamaa na hatimaye pesa alizoazimwa aweze kuzirejesha kwani umeshapitamwaka na nusu sasa hajarejesha hata shilingi kumi.

Natanguliza shukrani.
 
Kwa ulimwengu huu ulovaa bikini soma khitma kabsaa ila pole siku hizi hata misikitini na makanisani kuna wapigaji sembuse kitaa?
 
Unatoa pesa kwa rafiki ? Kweli hujui ramani inaendaje.. Sasa kuipata sina uhakika ila kama unaweza we rudiaha kwa Mdogo wako pesa huku ukiendelea kumfuatilia rafiki yako kipenzi..
Acha tu mkuu, kuamini mtu kupita kiasi ni tatizo..
 
Nenda Police Dawati la Jinsiaaa Kama Upo Dar nenda Kimara karibu na stand kuu ya kimara mpya ya mabus..Huyoo jimama Afande Mariam Ni kibokoo wa njiaaa ila kama upoo mkoani Nenda Kituo chochotee cha police Funguaa Jalada WIZI WA KUAMINIWA..nakwambia Mi ilinitokea MTU kanitapeli Pesa tena nilimpa tukiwa 2...mbona Alizirudisha!!!!!!!;
 
Miss chagga pesa na rafiki ni vitu vi 2 tofauti kabisa!!!usimwamini mtu yeyeto hata awe ndugu yako pesa pesa zinauwa undugu na urafiki!!!mi namwa mini mama yangu tu!!! Cha msingi we mlipe mdogo wako hiyo pesa yake!!!then kata mazoea na huyo!!!kulikuwa na ushahidi ulipo mpa hiyo pesa au mlienda kupeana chumbani mdogo wangu!!!?
 
Miss chagga pesa na rafiki ni vitu vi 2 tofauti kabisa!!!usimwamini mtu yeyeto hata awe ndugu yako pesa pesa zinauwa undugu na urafiki!!!mi namwa mini mama yangu tu!!! Cha msingi we mlipe mdogo wako hiyo pesa yake!!!then kata mazoea na huyo!!!kulikuwa na ushahidi ulipo mpa hiyo pesa au mlienda kupeana chumbani mdogo wangu!!!?
Hatukuweza kuonana, tuliwasiliana kwa simu tu kisha akatumiwa via M-PESA.
 
Ile sms ya M-pesa bado unayo we unaweza ukampeleka mbele ya sheria!!!kama bado iko kwa am yako
Kwa bahati mbaya aliyetuma anasema haioni tena ila kwenye System hiyo transaction inaweza kuonekana na ikawa printed tukapata hard copy bila shaka
 
Back
Top Bottom