Doto Dotto
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 4,046
- 3,049
Wana jukwaa amani iwe kwenu,
Ni juzi tu nilikuwa na mpenzi wangu sehemu fulani hivi tulivu, tukipiga story na ku-refresh.
Sasa wakati tukiendelea kupata good time, mimi simu yangu ikawa imeishiwa charge mnaotumia samsung mtakuwa mnajua hilo, na kwa wallet pesa ilikuwa imebaki kidogo ikabidi huyu manzi anipe simu yake nikaweka laini yangu then nikaenda kutoa tigo pesa karibu tu na hapo tulikuwa tumeketi.
Sasa nilipomaliza kutoa pesa moyo ukanituma kupita pita kwa haraka haraka kwenye chats zake kwenye simu yake.
Daaaah! Ghafla! Niliishiwa pozi baada ya kuona hii SMS "ile lodge tulioenda siku zile hapana tafuta lodge nyingine bhana ile mimi siitaki tena.
Nilirudi kwenye kiti huku nimefura kama mbogo nusura nimtembezee kichapo lakini nikapiga moyo konde, nilivombana kwa ule ushahidi wa SMS alikataa kataa eti kuna rafiki yake wa Mbezi alimuomba simu ndo akawa anachat na mpenzi wake.
Kesho yake asubuhi asubuhi mimi nikampiga kibuti bila kukawia. Lakini baada ye amekubali ni kweli amefanya mapenzi na jamaa, na anaomba nimsamehe jana kaniibukia usiku analia bado tuu anaomba nimsamehe.
Sasa wadau ushauri wenu ni muhimu kwangu. Je nitengue kauli au nikomae tuu.