Ushauri: Nimeitwa Polisi

Hapa nikubadili line tu, kule siendi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye simu yako huyo unayewasiliana naye mara kwa mara unajua mienendo yake?!

Tulia, tafakari kwanza! Usijipeleke kichwa kichwa! Wale wapo kazini wakikutia ndani mpaka uje uonekane huna hatia, ushapoteza muda wako mwingi sana pengine na hela pia!!

Wafanye kazi yao ipasavyo, wasirahisishe mambo kukuita tuu. Wakuje wakukamate wakakuhoji!!

Utii wa sheria bila shuruti...
 
Hapa nikubadili line tu, kule siendi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja nikupe kisa kilichonitokea miaka kadhaa iliyopita...

Niliamka asubuhi, mara paaap simu inaita namba mpya nikaona nipoke!

"unaongea na afande .... kutoka kituo cha polisi, unatakiwa ufike hapa haraka sana...akakata simu.."

Ilinishtua sana, nikawaza nishawahi piga dili mahali? no sijawahi! Basi nikawajulisha ndugu na jamaa ina case likitokea la kutokea!

Kufika kituoni nikakuta viajana kama wanne hivi wako selo, then afande akawaita!

"Huyu ndiye aliyewapa huo mzigo?"

Wakasema HAPANA!...nikawapiga mkwara wale polisi... lakini nikaona isiwe shida!

Basi nikawaacha pale wanabishana na wafungwa wao! Mimi huyo nikasepa zangu!

USHAURI.

Mpaka wamepata namba yako jua kabisa wana jina lako! ILA Kama unajiamini HUNA MABAYA NENDA ILA KUNA RISK UNAEZA ENDA UKAUNGWA NA UNAWEZA USIENDE WAKAKUSAKA (na mpaka wakusake utakua na jibu wakikupata nini kitafwata...)
 
Kwanza huyo polisi anayetaka uende central kwa sababu ya namba ambayo anaona unawasiliana nayo nafikiri anakosea sana hasa ukizingatia kwamba teknolojia ya kumpata wanayemtaka wanayo.

Pili anatakiwa akwambia haki zako iwapo kesi inakuhusu.

Tatu kabla ya kwenda hakikisha mambo yako umeyaweka vizuri,kama una issue yoyte ya sasa au zamani ambayo imekaa vibaya basi inawezekana ushadakwa so jiandae kisaikolojia

Vile vile angali pia maandiko yako mtandaoni usije naswa kwenye Tundu Bovu.

Ni hayo.
 
Asante mkuu
Hapa nawaza kubadili na line asa sijui unanishauri vipi maana hii nchi kwa kweli polisi wake nawajua
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah ko hapa nichague njia ipi maana pale uwezekano wa kukutana na janga lolote ni kugusa hata kama huhusiki

Nasie wananchi wakawaida wengi ndo yanatukuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesho ikifika mpigie huyo afande aliyekupigia simu mwambie umepata dharura unamuomba uweze kufika hapo kituoni jumatatu asubhi...na jumatatu asubuhi ufike kweli...kwako jitahidi usikae maana kama una msala watakufuata hapo! Kama ni kutoa ushirikiano ukatoe hiyo jumatatu upo na mdhamini na mwanasheria wako standby
 
Asante mkuu
Hapa nawaza kubadili na line asa sijui unanishauri vipi maana hii nchi kwa kweli polisi wake nawajua

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini ubadili line, jiamini kama huna kosa na wao wapo kazini wakufuate wakukamate wakakuhoji!!

Ukibadili line kama ni mtu wako wa karibu si bado mtakuwa mnawasiliana?!
 
Sina msala kaka yani sijui hata nini shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…