Ushauri: Nilizaa nae akaolewa ila ananirudia ananiomba matumizi

masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
15,539
2,000
Mi si kijana mudogo lakini katika ngano za mapenzi nimo!

Nina mpenzi wangu na imezaa naye mtoto, ila familia yangu katu haifahamu isipokuwa wachache sana. Na kwa kweli huyu bibie si tu nampenda , ila ni musweet sana, umbo poa sura nzuri sana na hata (wo)3 ni poa kabisa.

Sasa huyu sumolu hausi akaamua kuolewa vile vile na ikawa afadhali kwangu maana iliniondolea majukumu mengi iidogo.

Lakini cha kushangaza huyu bibie ananirudia rudia kwa kila kitu kuanzia kodi ya nyumba hadi matumizi ya nyumbani.

Kijana mwenziwe wanagombana kwa vile mshiko hautoshi. Sasa hii imenikera maana nakuwa kama natunza bado familia mbili.

Nashindwa kumtolea nje kwa sababu ya mtoto wangu, lakini cha moto nakiona bulungutu linavyonitoka.

Wanawake hasa, hebu nishaurini!
 

Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,327
2,000
Sasa tukushauri nini mkuu????lea mwanao ndo ushauri tunaoweza kukupa,kwani kumnaniliu...mdada wa watu hadi kumzalisha na wakati unajua una familia tayari uliomba ushauri???

Pambana na hali yako usitingishe ya mchepuko wako na motto wako acha maneno lea mtoto
 

charty

JF-Expert Member
Oct 28, 2013
7,414
2,000
Sasa si umuwezeshe huyo small house atafute kitu cha kufanya ili aingize kipato aache kukuchomoa mkwanja! ila ukome kwa niaba ya wanaume wenzio mmezidi kufungua zipu mno...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom