Ushauri: Ni jinsi gani kijana aliyemaliza chuo anaweza toka bila kupitia kuajiriwa?

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
21,532
34,912
Wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema!
Je ni jinsi gani kijana aliyemaliza chuo anaweza toka bila kutegemea ajira?? maana kila sehemu mambo yanabana (ila sio kisingizio)!!

Na kiuhalisia siwezi kutegemea ajira maana naamini haitaweza nifikisha sehemu ninayotaka kama kijana!!

Je nyie mliojiajiri mmefikaje huko?? Embu wekeni njia hapa nasi tujifunze maana tunangoja ajira ila kiuhalisia ajira ni mfumo ule ule wa kumnyenyekea mtu na ningumu sana kutoka!!

Naombeni mawazo waungwana!!
NB: Sihitaji njia ambayo sio legal pia sihitaji mambo ya forever products and the alike!!

Asanteni!
 
Kwa mawazo yangu ni kwamba kujiajiri bila kuajiriwa kwanza ni ngumu, labda kama una ndugu zako wenye hela wakugawie mtaji ufanye biashara, kinyume na hapo inabidi utafute mahali pakuajiriwa kwanza kusudi upate mtaji wa kuanzia, hapo tayari unatakiwa uwe na wazo la biashara utakayofanya endapo utapata mtaji, mwenzio nimemaliza chuo nikafanya kibarua ambayo anastaili afanye hata form four leaver, lakini kusudi langu lilikuwa nipate mtaji na nimefanikisha lengo langu namshukuru mungu. Changamka Jomba vyeti vya chuo visikuzuie kujichanganya kitaani.
 
Nashukuru kwa mawazo yako mkuu!
 
Cha kwanza ni kuwa na MTAJI.

Kama mtaji tayari unao, omba ushauri juu ya biashara gani ya kufanya kwa mtaji ulionao.
Mawazo mengi yanapatikana kwenye jukwaa la Biashara
 
Kwanza uwe na wazo unataka ufanye nini!? Biashara au Kilimo au ishu gani unaweza kuimudu vizuri lakini wakati unaendelea kutafakari juu ya hayo pia lazima uwe na mtaji sasa hapo kwenye mtaji lazima utafute kazi ambayo ulipwe kipato chako,au la sivyo uwe na ndugu basi wakuwezeshe ila ushauri wangu kuhusu kilimo aisee inatakiwa uwe na mtaji mzuri eebwana afadhali biashara.....Mimi ndugu yako najuta hapa nilipata kimtaji kidogo nikapata ushauri wa kilimo sina hamu.....nimeanza kutafuta mtaji upya tena nifanye biashara tu ila sasa kazi ndo hazipatikani maisha ni Fumbo kubwa.
 
Wakuu ni mara chache sana wazo la kibiashara linaweza kuwa jipya kabisa, mara nyingi tunapata mawazo ya biashara kutoka katika biashara zinazofanyika. Ni rahisi sana kujenga biashara kwenye mawazo ambayo yameshafanyika kuliko kwenye wazo jipya. Na kama ni wazo jipya inabidi uwe na nguvu ya kutosha kutengeneza soko kitu ambacho ni kigumu kwa wale wanaoanza kwa mara ya kwanza, sema una mtaji wa shilingi ngapi?
 
Mkuu kufanya biashara mpya inayo tofautiana na iliyo zoeleka ni rahisi ila lazima uwe na akili ya ziada
 
Mkuu siwezi kupinga mawazo yako, ila nitakubali zaidi endapo umefanyika utafiti wa kutosha kabla na baada ya kuanza hiyo biashara! Watanzania wengi wa leo tumekuwa wagumu sana kujifunza kupitia kwa wale waliofanikiwa jambo ambalo mimi siliafiki hata kidogo!
 
Wakuu ni mara chache sana wazo la kibiashara linaweza kuwa jipya kabisa, mara nyingi tunapata mawazo ya biashara kutoka katika biashara zinazofanyika. Ni rahisi sana kujenga biashara kwenye mawazo ambayo yameshafanyika kuliko kwenye wazo jipya. Na kama ni wazo jipya inabidi uwe na nguvu ya kutosha kutengeneza soko kitu ambacho ni kigumu kwa wale wanaoanza kwa mara ya kwanza, sema una mtaji wa shilingi ngapi?
Kiukweli sina mtaji wa pesa! Na mtaji nilio nao ni...

1. Uhai na afya

2. Kauli kwa wateja (customer care)

3. Passion ya kufika mbali kimaisha

Naomba mawazo yako ndugu
 
Mkuu siwezi kupinga mawazo yako, ila nitakubali zaidi endapo umefanyika utafiti wa kutosha kabla na baada ya kuanza hiyo biashara! Watanzania wengi wa leo tumekuwa wagumu sana kujifunza kupitia kwa wale waliofanikiwa jambo ambalo mimi siliafiki hata kidogo!
Mkuu kuna vitu vichache tunavyo kosa katika ubunifu na hii ndo hutufanya tuone biashara mpya ni ngumu kuanzisha
 
Shahada ya Uhandisi wa umwagiliaji na vyanzo maji (2016)!
so kuitumia hiyo elimu kujiajiri ni ngumu sababu ya mtaji, vipi mkijikusanya watu mliomaliza kisha mkatengeneza proposal mpewe capital kisha mfanye miradi? maana ukame ndio huo hadi tuna upungufu wa chakula sasa na kilimo cha umwagiliaji ndio sustainable solution...
elimu yako kukosa matumizi kwa changamoto za hapa tanzania ni kitu cha kusikitisha sana, sana, sana...ni kama afrika elimu haitusaidii bali kutupotezea muda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom