Ushauri: Nataka nikaishi Ulaya

Watanzania wengi ni malofa..% kubwa ya wachangiaji hawajawah toka nje ya Tz ukiacha Afrika..ujuaji sasa mmmh
Wewe umewahi kwenda nchi zipi mbali na za Africa?
Tupatie uzoefu wa life ya nje ili wengi tujifunze toka kwako!
 
Umri unakurusu nenda, usiogope umri ndio huo unaruhusu kwanini nasema hivi

Kama ni kweli umri huo ndio wako naimani
Raha ujui, wanawake wazuri ujui, matumizi ya pesa ujui kwani umri wako kibongo bongo Kijana bado yupo kwa wazazi

Hivyo basi ukienda ulaya kitu unachoweza kumis pengine kupewa pesa na walezi ila ukikomaa unaanza shika pesa yako nakuanza itafuta raha nakujua raha ulaya katu uwezi kumis tz so nenda umri ndio huo foolish age utumie
 


Kazi gani dada, kwa europe hata kama una degree haina faida kwako. labda kama kusafisha barabara,vyoo,kuzoa zile takataka pembeni mwa barabara na kadhalika.

Chagua hapo ipi unataka?
 
Nakubaliana na Richard. Ningependa kuchimba kidogo. Unaweza kwenda nchi yeyote iwapo tu una ujuzi wanaouhitaji. Ningekuwa wewe ningegoogle "what coutries are short of IT stuff/skills" na kuendelea hapo. Kwa sasa nchi zinazohitaji watu kwa sana ni Australia na Canada; hawa wameweka ''express entry programs' hili kurahisisha uhamiaji. Ukiachana na hizo nchi mbili New zealand na Dernmark ni nchi nzuri kwa mtazamo wangu. Hivyo basi jipe uwanja mpana wa nchi za kwenda ili husipate jazba pale changamoto zinapojitokeza. Vitu muhimu utakavyohitaji kwa nchi tajwa; 1. IELTS tests; hii ni mitihani ya kiingereza, inafanyika British council na vituo kadhaa mara 2/3 kila mwezi. Gharama kwa sasa Tsh 465,000. 2. Kutegemeana na nchi utakayotaka kwenda itabidi uwatumia nakala za vyeti vyako ili walinganishe kiwango na elimu ya kwao na yako yaani educational equivalence. Kwenye website za uhamiaji utaona orodha ya vyombo wanavyovitambua. Hapa pia utalipia (sijui bei lakini angalia tovuti husika). Ukishapata hivyo viwili (kwa kawaida) utaruhusiwa kuomba kazi (Makampuni ya ndani huwa yanatafuta wafanyakazi wahamiaji kwa kupitia balozi zao) Hizo ndo kazi utakazoweza kuomba. Unavyoapply watataka viambatanisho vya IELTS tests na educational equivalence reports, medical reports, n.k. Ukipata kazi utapewa muda maarumu wa kureport nchi husika. Mara nyingi Kampuni inayokuajiri (kujua kuwa wewe ni mgeni) watakuandalia mazingira ya kufika ila hili siyo lazima na inategemea na makubaliano yenu wakati wanakupa kazi. Kwa kuwa umeonyesha kujituma na kutochagua kazi ni vema ujue utakutana na waajiri watakaotaka kukupa kazi za kuosha vyo mwenye migahawa, n.k. Yaani kazi ambazo utaona haziendani na wewe mi nathan hautachagua kazi. Hata hivyo ukifika huko unaweza kubadili kazi. Pia ni vyema utafiti kama utahitaji kibali cha taaluma husika ili kuruhusiwa kufanya kazi nchi husika. Mfano; Fundi bomba Tanzania hawezifanya hiyo shughuli Canada bila kibali cha ufundi bomba. Hilo liaathiri uwezekano wa kupata kazi kupitia balozi husika. Lakini isikukatishe tamaa, unaweza apply kazi yeyote alafu ukifika huko ukaenda kozi ya kupata kibali cha taaluma yako (mara nyingi haizidi miezi 12) na kisha kufanya kazi uliyosomea. Kwa sasa jitahidi upate experience ya taaluma yako, itakusaidia mbeleni, na jipe mda usiopungua miezi 6 kufuatilia jambo hili. Kila la kheri!
 

MWOMBE MUNGU AKUSAIDIE, HATA UKIENDA WAPI IT CAN JUST BE THE SAME!
 
Kwa diploma ya IT labda ukabebe maboksi, ila sasa visa hawawezi kukupa, kupata visa ungekua unaomba kama mwanafunzi ungepata kirahisi, au kama mtu mwenye pesa ndefu anajua anaenda kufanya nini, wewe umesema umefanya kazi bila mafanikio, nauli utatoa wapi aisee? na hela ya kuanzia maisha angalau emergency money ya kukuwezesha kukaa ulaya miezi angalau mitatu ili kuhakikisha umepata kazi hata ya chini. Inshort inabidi uweke kama Tshs. 10Million hivi just in case.
 
mkuu umeandika point sana
 
nashukuru sana mkuu kwa kuniongezea maarifa,hakika nitajitahidi kufuata ushauri wako.
 
Kazi gani dada, kwa europe hata kama una degree haina faida kwako. labda kama kusafisha barabara,vyoo,kuzoa zile takataka pembeni mwa barabara na kadhalika.

Chagua hapo ipi unataka?
niko tayari kufanya kazi yoyote mkuu.
 
'Upo tayari kufanya kazi yoyote?' Angalia kijana aiseee wengine wakienda huko wanarudi sio riziki.
 
niko tayari kufanya kazi yoyote mkuu.

Pole sana mkuu. inaonesha unashida sana,kuwa mvumilivu Mungu yupo nawe utapata kazi hapahapa. achana na ulaya gharama mno huko,hutobakiwa na akiba yeyote.
 
Safi sana mkuu tunanufaika wengi kwakweli
 
Inspector Harun..babuuuuu..hujawahi kusikia mtu kalala na njaa ndani ya Paris Ufaransaaa au sababu ni jiji la maraha ndo watu hawalambi garasaaa!!?

Paris kuna machinga wanauza maji ya chupa kwenye ndoo kama wale wanaouza barabarani kwenye mataa ya Jangwani pale. Machinga kibao huko Ulaya. Kama mtu anataka status ya kuonekana anaishi Ulaya haya ila kule hali si hali. Maisha magumu balaa
 
Kumbe diploma tu?
Unatakiwa uwe na sifa kama za yule mwenyekiti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…