Ushauri: Nataka nikaishi Ulaya

Ingia you tube andika suprising europe utapata majibu yote nna uhakika

Mkuu Mwanaume akiamua kufanya kitu hakuna wa kuzuia, suprising europe inategemeana na mtu na mtu kila mtu ana njia yake, wale jamaa wanapata PESA sema zinaishia kwenye pombe then hawakubali kazi mbovu

kama kuna mTZ amekumbwa na hilo basi ni uvivu, ukienda kwa mategemeo makubwa utaumia
 
Nina diploma ya IT pia lakin naona sasa mambo yangu mazur kabsa... Komaa hapahapa usichagua kazi
 
haya diaspora mtarajiwa nenda germany hutojutia........
Kwanini Germany mkuu, na sio uk, USA, Canada n. K. halafu Germany si kuna kibarua cha kujifunza lugha kwanza maana kiingereza hakitumiki...
 
Tangu nisome thread hapa JF kwamba matikiti maji ya siku hizi ni matamu kupitiliza basi na mawazo ya kwenda kwa Wazungu nayo nishayafutilia mbali!
 
Nimebase sana katika Masuala ya Networking na maintenance.
 
Dah hayo maneno bro
Acjisumbue saaana kufikiria ulaya
Asome zaidi ili aende hizo nchi za ulaya kama expart lakini azamie 2 na shahada ya diploma mwisho atasafisha barabara ulaya
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] kazi yoyote upo tayari ata ushoga !!?
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]

#Ni mtazamo tuu
 

Kijana, mimi nakushauri kwamba suala ya kwenda Ulaya na Diploma ya IT usahau.

Ungekuwa una degree ya IT (tena baadhi ya maeneo kama software engineering au software development) basi ungepata scholarship kupitia wafadhili kama wale wa jumuiya ya madola, na ukaenda kusoma masters na ambayo labda ingekusaidia kuona maisha ya huko.

Pili, suala la kwenda Ulaya kwa minajili ya kuzamia nalo kwa sasa ni gumu sana na hata ukitaka kwenda kupitia njia ya Mediterranean, pia unaweza kuishia Libya.

Halafu, kila kitu siku hizi ni bahati ya mtu pia inasaidia, kama una bahati unaweza kupata tu namna na ukajikuta unakwenda Afrika Kusini, Botswana au Ulaya, lakini si sasa hivi wala miaka hii.

Ulaya ya leo si Ulaya ya miaka 20 ilopita, na mimi nakwambia hivyo kutokana na uzoefu wangu wa kutembelea na kuishi nchi kadhaa ulimwenguni zikiwemo zile za barani Ulaya (mimi niliwahi kuwa Boy Scout)

Kila njia siku hizi imesilibwa na sheria na taratibu za uhamiaji hivyo kufanya situation kuwa tata sana.

Tatizo la vijana wengi ukiwapa ushauri kama huu watakwambia unawawekea kauzibe, ila ushauri nao lazima uwe updated kulingana na mazingira na matukio.

Nchi nyingi kama Afrika Kusini sasa nao wana matatizo na wahamiaji wa kutoka Zimbabwe na kwingine, pia nchi za Ulaya bila shaka umeona na kusikia yanayotkea sasa hivi.

Nchi pekee ambayo kidogo ipo wazi ni Canada lakini ni lazima uwe na angalau degree ya kwanza kama hiyo ya IT na uwe umebobea maeneo fulani ambayo yanakufanya uwe juu ya watafutaji wengine.

Canada khasa jimbo la Quebec, wanahitaji wataalam wa ujenzi kwenye ujenzi wa majengo, wataalam wa IT na afya- nenda kwenye link hii na uisome kwa makini na uelewe kuhusu kuhamia Canada - Immigrate to Canada na hapa kuhusu Quebec Determine your eligibility: Quebec-selected skilled workers na kuomba kuingia Quebec yenyewe hapa: Immigration-Québec - Home Page

Ila jitahidi hapohapo ulipo ongeza degree, pigana na maisha na utafanikiwa tu ipo siku milango itafunguliwa, lakini fanya hivyo kabla hutafika miaka 30 - hivyo una miaka 8 tu kuanzia sasa.

😉
 
Dah hayo maneno bro
Acjisumbue saaana kufikiria ulaya
Asome zaidi ili aende hizo nchi za ulaya kama expart lakini azamie 2 na shahada ya diploma mwisho atasafisha barabara ulaya
Kwi kwi makubwaa...
 
Dah hayo maneno bro
Acjisumbue saaana kufikiria ulaya
Asome zaidi ili aende hizo nchi za ulaya kama expart lakini azamie 2 na shahada ya diploma mwisho atasafisha barabara ulaya

Teh-teh-teh

Siku hizi barabara zinasafishwa na wazungu wenyewe wale wasokwenda shule na wanalipwa hata zaidi ya wale wanaobeba boksi.
 
miaka 22 maana yake umezaliwa 1994,,form4 umehitimu2012,,diploma ya it umehitimu 2015.
Nashindwa kuelewa umeangaika lini tena kwa sana(kama ulivyosema) kutafuta maisha.
Ni bora useme unataka kwenda ulaya kutafuta maisha,,,lakini si kwa kigezo ya kwamba umeshahangaika sana uku Tanzania kutafuta maisha(umri wako unapingana na hilo)
 
Nashukuru sana mkuu,
hakika msaada wako umenifungua njia na wengi wamefaidika nao..
CANADA COMING SOOOOON 🙂
 
form 4 2011,diploma 2014.
 
nashukuru mkuu,ingekua vizuri pia kama ungenipa njia ya kufikia huko.
Jilipue kwa mtalii wa kitasha..., ukifumba macho na kufungua utajikuta ktk mojawapo ya nchi zilizotajwa hapo juu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…