Ushauri: Nataka kununua home theatre!!

Je hi fi music system inapatikana wapi kwa Tanzania? Mimi sipendi bass kubwa sana, napenda music system unaochuja vizuri (stereo) na kusikika vyombo vyote
 
Aahaaa kaka acha kumtishia bure,mm nimenunua home theater pale samsung agent mwanza pale nata kwa bei ya 250,000 ina deck,spika 5 na woofer moja.
Wapi apo nikachukue kesho asubuhi ya laki mbili ya Samsung,, au ni vile vyenye spika kama kikombe cha chai vinaungua kama taa za umeme
 
Je hi fi music system inapatikana wapi kwa Tanzania? Mimi sipendi bass kubwa sana, napenda music system unaochuja vizuri (stereo) na kusikika vyombo vyote
cheki kwa dealers wa miziki mjini, mbona zipo nyingi tu ingawa watu hawazipendelei sana siku hizi
 
cheki kwa dealers wa miziki mjini, mbona zipo nyingi tu ingawa watu hawazipendelei sana siku hizi
Yale yale ya bendera kufuata upepo, unadhani kuna jipya basi???.

Na bei ya hizi hi-fi ni juu kuliko. nadhanu pia yaweza kuwa sababu.
 
Bose ina bei gani?
 
home theatre ni nzuri kwa wapenda movies kwani yenyewe inatoa sound inayoongezwa manjonjo hata kama hayakurekodiwa kama mwangwi,base sana zinakuwa na spika nyingi n.k. na hizi Ilitengenezwa maalum kwa movies ndo maana zikaitwa home theatre.... lakini kwa wapenda muziki sana wanunue radio zenye mfumo wa hi-fi ( high fidelity) hii inakuwa na speaker mbili tu lakini zinachambua na kuchuja music na kukufanya kusikia kila kifaa kilichopigwa humo.
 
Bei gani hii mkuu?
 
Hizi ndo best brands kwa audio systems kwa sasa. Speaker ndogo mziki mkubwa
1. Sonos
2. Bose
3. Denon
Hizo zingine za kawaida tu

Google hizo brands ujiridhishe
Hapo ni denon tu wengine uzushi. Halafu brand hizi sijui kama zinapatikana mkuu.
 

Acha maneno weka music.

Mbona hujatupia picha?
 
Hivi wakuu duka Gan hasa kwa hapa bongo naweza pata home theater ya bajet ya laki sita hivi maanake Jana nimezunguka kariakoo kila nayoiona siiamin nataka Sony
Sony wana duka lao mitaa ya Nkurumah street, mkabala na Jengo la NHC au TTCL

Au unweza enda Mlimani City kuna duka pia na ndani kule Nakumatt au Game
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…