Ushauri: Nahitaji kununua TV Flat Screen

Shelus Jr

JF-Expert Member
Jun 2, 2016
270
166
Habari za muda huu wana jamvi,

Natumaini humu jukwaani wapo wajuzi wengi kwa nyanja tofauti tofauti, kwa wale wataalam wa vifaa vya electronic hususani TV za kisasa naomba wanishauri ni ipi iliyo Kampuni nzuri.

Nahitaji kuanzia 47" 52" ni kwa matumizi ya nyumbani tu.

Mimi sio mwandishi mzuri sana naomba kuwasilisha kama ilivyo.
 
Kuna vitu vya kuzingatia inapaswa ukavifahamu kabla ya kununua flat tv.

Angalau vitakusaidia kununua tv yenye ubora hasa upande wa picha na matumizi mengine ya ziada utakayoyahitaji baadae.

Baadhi ya mambo ya kuzingatia ununuapo tv.
1. Resolution - tv nzuri ni zenye 4k kama itakuwa gharama basi ni bora uchukue yenye 1900x1080.

2. TV iwe na HDR walau HDR10. High dynamic range inaipa tv uwezo wa kutofautisha rangi za objects kwa usahihi, kwa mfano video ambayo imechukuliwa kwenye mwanga hafifu rangi ya nyeusi inatawala mpaka hata vitu ambavyo si vieusi vinakuwa kama veusi.

Angalia utofauti wa tv yenye hdr na isio na hdr
HDR.jpg

Ukiangalia picha kushoto paka yuko exposed sana scene na mwanga wa taa ambao ni hafifu haunokani vizuri tofauti na picha ya kulia yenye hdr.

Kujua tv hdr ni vizuri muuzaji akawa nakiwekea video zenye scene za usiku na sio za mchana pekee unaweza usione tofauti.

3. TV iwe na PVR- Personal Video Recorder inasaidia kurekodi tv program unayoitaka na kuihifadhi kwenye usb flash drive.

4. Contrast ratio iwe kubwa angalau zaidi ya 3000:1. Contrast ratio ni utofauti kati rangi nyeupe(bright) na nyeusi (dark)

Kama video imepchuliwa usiku basi sehemu ambayo ni dark basi iwe dark hivyohivyo na sehemu ambayo ipo bright basi itokee ikiwa bright.
Angalia hii link imefafanuliwa kwa mifano.
What is contrast ratio?
images.jpeg

Hiyo picha ina picha mbili, ya kushoto ina contrast ratio kubwa na inaonyesha pure dark upande wa juu wenye giza.

Wakati ya kulia contrast ratio ni ndogo brightness imetapakaa picha nzima mpaka kwenye giza.


4. Viewing angle pia la kuzingatia

5. Display technology inamatter kama mpunga utakuwa nao Oled au qled.

6. USB ports ziwe nyingi hata hdmi

7. TV iwe na dvb tech kama dvb-s/t/c ili uweze kuangalia baadhi ya tv bila king'amuzi cha nje.

8. TV iwe na uwezo wa kuplay aina nyingi za video formats kama mkv,mp4,avi, ogg, webm nk

9. Refresh rate ni vizruri pia ikawa 120 kama utakuwa mpenzi wa kucheza games kwenye tv.

Kwangu mimi ningekushauri uchukue tcl zinazotumia OS ya androidtv.
1. TCL 43S6500
Specification zake zipo hapa.
43" S6500 Series.

2. TCL 43P8M

https://www.tclelectronics.com.au/products/series-p-43-inch-p8m-quhd-tv-ai-in/
 
Back
Top Bottom