nyaggad
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 1,160
- 694
Habari wana jamii forums
Wandugu sio siri nahisi na matatizo ya kisaikolojia naombeni ushauri wenu,mimi huwa nikimpenda msichana mpaka huwa nahisi kuchanganyikiwa maana huwa napenda sana kupita mfano,sasa hivi kuna binti mmoja ndo nipo nae kwenye relation yani nampenda mpaka watu wananishangaa.
Nikiwa natembea mda wote yupo kichwani mwangu,nikiwa nafanya kazi mda mwingi yupo kwenye akili zangu,nikiona kitu kizuri kinauzwa kinachomfaa lazima nimnunulie,pesa huwa namtumia mara kwa mara bila yeye kuniomba,nampigia simu kwa siku kama si chini ya mara kumi,nikilala usiku mara nyingi huwa namuota.
Mwenzenu nimechizika kwa penzi la huyu dada,yani tunapokutana wawili huwa najihisi nimekaa na kiumbe kizuri ajabu mapigo yangu ya moyo huenda kwa kasi ajabu utafikiri nilikuwa nakimbizwa na mnyama mkali,nimemuomba mautamu ameniambia atanipa mpaka tufunge ndoa,hapa nilipo nafanya mahesabu nimuoe mapema kabla hajabadilisha nia.Hivi jamani huu ni upendo wa kawaida au na matatizo ya kisaikolojia.
Napenda kuwasilisha