Ushauri: Nadhulumiwa na mjomba bila sababu?

Ushauri: Nadhulumiwa na mjomba bila sababu?

kissambivi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
218
Reaction score
119
Mimi ni kijana wa miaka 28 nimeoa Nina mtoto mmoja wa mwaka mmoja,

Bahati nzuri nimelewa na kusoma kwa Babu yangu na Bibi yangu upande wa kike maana ndio walezi wangu ;Kwa bahati mbaya Babu na Bibi yangu wamefariki Nikiwa nasoma form two;

Babu yangu alinifundisha kuwekeza baadhi ya rasilimali kwa kupanda miti kwenye baadhi ya maeneo ukiunganisha unapata kama ekari saba(7) .Mjomba ni mtoto pekee wa kiume kati ya watoto watano wa Babu yangu imefikia kipindi mjomba amefuta kabisa Mali na maeneo aliyonipa Babu,Moja ya eneo langu amesha vuna Miti yangu, Nashindwa kuelewa kwanini anifanyie hivyo,Yeye anadai kwa anataifisha Mali zangu kisa Ada aliyonilipia Nikiwa chuoni .

Naombeni ushauri amenipandikisha chuki kwa Dada zake imefikia kipindi Mimi na familia yangu tunanyoshewa vidole eti Mimi Nina kiburi na Sina pakuanzia .
 
mzeee umri huo bado unaweza ukajipanga bila kutegemea chochote wala yyt, usitake kufikaaa nilipofikaga mm, nilimpiga ndugu yng tofali la usooo, tangu siku hioooo n mtu mzima ila siku nyingne tukikutana kwa ghafla anaweza anisalimiee
 
Huyo ni mjomba wako kabisa,yaani kaka au mdogo wa mama.Mi navyojua wajomba hua hawanaga shida ya mirathi,wenye shida na mali Mara nyingi ni ndugu wa baba.
 
Nadhani wewe hujitambui kabisa na una matatizo kisaikolojia kama walivyo vijana wengi wapinzani wa siasa za Tanzania. Shukuru sana umesomeshwa mpaka chuo!

Ni hivi, kama umesoma mpaka chuo na ile miti uliipanda wewe mwenyewe, achana na hivyo vi mali haviwezi kukufikisha popote zaidi ya migogoro.

Wewe shukuru tu hiyo hali na wala huna haja ya kuwa na ugomvi na mjomba wako kwa sababu utajri wako hautatokana na hiyo miti bali ni akili yako wewe mwenyewe unavyoweza kuichanga and you are not late for that.

Hivyo miti na huyo mjomba wako ni vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wako ktk kuvicontrol ila your attitude ya kufanikiwa ktk maisha au kutafuta mishemishe zingine it is under your control and you can make it na unaweza kufanikiwa zaidi ya hiyo miti.
 
Ili uweze kufanikiwa katika maisha huko mbeleni, potezea hiyo miti... ipo siku mjomba atakutafuta kwa aibu
 
Mjomba Mungu anakuona jnc unavyo-mtetemesha mtoa mada.
 
Kama babu yako hakuacha maandiko yeyote ya kukukabidhi hilo shamba ulilo panda miti kwa sheria ya mirathi huna haki, hivyo chukulia mjomba alikukopesha pesa ukasoma chuo na umemlipa kwa hiyo miti. USISAHAU KUMSHUKURU KWA KUKUWEZESHA KUHITIMU CHUO SI KITU KIDOGO.
 
Mjomba wako yuko sahihi hapo sio kwenu wala huna haki yoyote hapo cha kufanya katafute haki kwenu kwa baba yako. kama ulizaliwa nyumbani kwao mama yako huna jinsi mlaumu mama yako Kisha upambane na hali yako.
Niende kwa baba wa kambo ananikataa
 
Kama babu yako hakuacha maandiko yeyote ya kukukabidhi hilo shamba ulilo panda miti kwa sheria ya mirathi huna haki, hivyo chukulia mjomba alikukopesha pesa ukasoma chuo na umemlipa kwa hiyo miti. USISAHAU KUMSHUKURU KWA KUKUWEZESHA KUHITIMU CHUO SI KITU KIDOGO.
Sema ndio hicho daa
 
Mkuu kama umesoma na una kazi ingia bank chukua mkopo anza mishe mishe utapiga hela nyingi then nunua eneo hapo hapo kijijini tena itakua sio hela nyingi kwa mbwinde anza upya.kumbuka kuna msema respect is earned hakuna mtu atakuja kukupa respect you must earn it
Sema ndio hicho daa
 
Hii mpya msomi mzima unategemea kutoka kwa urithi wa babu? Haiwezekani Ndalichako lazima ajiuzulu
 
Back
Top Bottom