minda
JF-Expert Member
- Oct 2, 2009
- 1,068
- 67
Wakuu, kupitia jukwaa hili napenda kumshauri komredi mwiru ang'atuke siasa.
Nimekuwa nikifuatilia mchango wa komredi kingunge ngombale mwiru kwenye medani ya siasa hapa nchini tangu nilipokuwa mdogo miaka ya 1990s.
Ama kwa hakika, huyu mwanasiasa ni miongoni mwa wanasiasa wanaojulikana kwenye historia ya nchi hii; hasa kwa upande wa ujenzi wa siasa ya ujamaa wakati wa utawala wa mwl nyerere.
Nakumbuka sana miaka hiyo ya 1990s, huyo mwanasiasa alisifika kuwa miongoni mwa vinara wa siasa ya ujamaa; mzalendo asiyepingika katika ujenzi wa ujamaa wa kweli na yasemekana alisomea kwa mara ya kwanza, mambo ya siasa ya ujamaa huko algeria kwa ben bella, nchi maarufu ya kijamaa.
Ikaelezwa ya kwamba kutokana na ukereketwa wa siasa za ujamaa, hasa za ulaya mashariki na soviet, huyu mwanasiasa akaamua hata kuacha dini yake ya ukristo na akaamua kuwa mpagani, kama kanuni za kijamaa za kisovieti zinavyoelekeza.
Tunaambiwa hata leo hii, huyu babu ni mpagani na kama mtu atamuulizia dini, basi dini yake ni ccm.
Hata hivyo, bahati mbaya ccm aliyoiasisi sasa siyo hiyo tena, kwani ilishaondoka na mwalimu.
Pengine mkuu yeyote anaweza kujiuliza ni kwa nini nashauri mzee kingunge ang'atuke siasa.
Ule wasifu alionao kama mjamaa sasa haupo tena kwa huyu mwanasiasa, kiasi kwamba naona kama kosa kumuita 'komredi', heshima apewayo mjamaa halisi kama akina castro, che guevara, mugabe, chriss hani nk
Zifuatazo ni sababu zilizopelekea mimi kushauri 'komredi 'mwiru ang'atuke siasa:
updates;
1. novemba 25, 2010:
hatimaye jk amemtupilia mbali huyu mzee kwa kumnyima ubunge wa kuteuliwa na hatimaye uwaziri kama jk alivyoteua baraza lake la mawaziri jana 24 novemba, 2010. ni wazi sio jk tu bali watanzania wengi tungependa kumuona huyu mzee aking'atuka siasa na kama tatizo lake ni ulaji basi apewe kitengo ndani ya chama chake ambacho ni tajiri sana kimapato.
wakuu mnasemaje?

- Ameishiwa haiba ya kijamaa na sasa kilichobaki kama mjamaa ni upagani wake ambao hauna nguvu na huenda akabaki peke yake duniani kwani hata wale wajamaa wa mashariki ni wafuasi wazuri wa dini mfano urusi (orthodox), poland (rc), algeria (islam) nk
- Amevunja ile kanuni ya 'wazee ni dawa' katika kushauri watanzania juu ya uzalendo na badala yake amekuwa akijikita katika ugomvi usio na msingi na viongozi wa dini mfano hivi karibuni amekaririwa akipondea viongozi wa dini kuhubiri elimu ya urai; aidha miezi michache iliyopita alijiingiza katika ugomvi 'usio wa lazima' na kanisa katoliki baada ya kanisa hilo kupitia idara yake ya haki na amani kutoa waraka unaolenga kuelimisha watanzania juu ya elimu ya uraia, kiasi cha kupelekea chama chake kumpa karipio la 'siri' na kumshauri kupitia nec, aachane na viongozi wa dini..
- Amehusishwa na kupendelea wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya chama chake na kukandamiza wale wanaotetea maslahi ya umma.
- Amehusishwa na kung'ang'ania kwenye siasa kwa sababu za kufaidika kiuchumi kwani anahusishwa na biashara kubwa kubwa kupitia familia yake, mfano suala la ubungo terminal na machinga complex.
- Amekuwa mfadhili na muasisi wa dhana ya maslahi ya chama kama dhana kinzani na kinyume cha maslahi ya taifa na kufanikiwa kwa kuona kama maadui wa chama chake wale watakaotetea maslahi ya umma.
- Alishang'atuka ubunge wa jimbo (kilwa) lakini jk akamteua kuwa mbunge wa kuteuliwa. Alitakiwa 'kumsihi' jk asifanye hivyo kama kweli alikuwa na lengo zuri la kung'atuka, badala yake alikubali haraka uteuzi japo jk 'alimjaribu' ili akatae ili jk aondokane na lawama ya kuacha wazee ambao ni 'dawa'.
- Wenzake kama akina mzindakaya, kimiti, askofu desmond tutu, mandela nk wameamua kung'atuka kwa heshima. Asisubiri kuja kuumbuliwa kama akina malecela, mungai, kaunda, mporogonyi nk
- Amekuwa mpinzani wa taasisi yoyote inayojitokeza kutoa elimu ya uraia kama nilivyoeleza hapo juu. Je umbumbumbu wa elimu ya uraia kwa mzee kingunge na chama chake ni mtaji wa kisiasa? - yaani ndio kusema kwamba kutoa elimu ya uraia ndio kutasababisha 'kumshika mkono kipofu' ili ashtuke?
- Katika miezi ya hivi karibuni, kingunge amekuwa akimpinga na kumpondea baba wa taifa na azimio la arusha (siasa ya ujamaa) na badala yake amekuwa akifagilia zaidi azimio la zanzibar.
- Awapishe vijana ili nao waoneshe uwezo wao. Japo ni kikongwe, huyu babu ndiye kaimu kamanda ya uvccm baada ya 'kumpindua' malecela.
- Ongezea...!