Ushauri mwanamke mjamzito wa wiki ya 38 anaweza kusafiri?

Pendaelli

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
8,917
23,239
wakuu habari za wakati huu?

Mke wangu ana ujauzito wa wiki ya 38 na siku 2. Anatakiwa kusafiri kati ya Dar na Morogoro. Sababu ya kusafiri ni madai ya kua sitaweza kumtunza atakapo jifungua, ni kama wanalazimisha wakakae nae wao.

Kweli sijawai kuwa na mtoto hapo kabla lakini nimejifunza angalao yale ya msingi, na hata majirani wapo ingawa siwategemei. Pamoja na changamoto pesa,umbali wa wa hospiali lakini ningependa kumpokea mtoto wetu katika hayo yote, lakini ndugu wamenitisha hadi nakosa kujiamini.

Naomba ushauri kwenu wakuu kama jambo kama hili linawezekana au ni komae tuu.
nawatakieni kila la heri.
 
Hofu yako ya yeye kurudi akajifungulie kwao ni nini?

Halafu hapo anasafiri tu bila tatizo.

Mpe ruhusa aende kwao (bint anapojifungua kuna vimila mila ) ambavyo wewe huwezi kuvifanya.
 
nashukuru mkuu, hofu yangu anaweza kujifungulia njiani maana niliwahi kusikia muda alio nao si rafiki kwa safari.
 
Wiki 38 yupo ndani kabisa ya Delivery time
Hata Hospital kwa Muda huo anakuwa kashauriwa popote alipo awe timamu na Vifaa vyake vyote vya kujifungulia

Hata akienda Clinic akifika Wiki hizo anatakiwa awe anaenda kamili as if anaenda kujifungua!

Kumsafirisha Safar ndefu katika kipindi hiki si salama kabisa Kama Tatizo ni Mtu wa kumsaidia bora huyo Mtu ndio amfuate huyo Mama Mjamzito akishajifungua hata ndani ya wiki anaweza kusafiri Kama hatojifungua kwa Shida na Mtoto atakuwa Hana Tatizo la Ki Afya

Kuanzia wiki ya 36 Mtoto anakuwa kishakamilka Mara nyingi
 
asante sana ndugu kwa kweli pamoja na ulazimishwaji lakini wiki ya 38 imesogea sana
 
Miezi 9 ni wiki 36 sio? Mimba ya "kawaida" huwa ni ±2 yaani kati ya wiki 34 hadi 38 mwanamke anajifungua. Inaonekana huna taarifa za kutosha kutoka kliniki. Pili bado unasumbuliwa na utoto. Huyo ni mkeo hivyo ni lazima uwe Baba wa ukweli. Beba majukumu yote mikononi mwako kwa Juhudi na Maarifa yote huku mkimtanguliza Mungu. Faida na Hasara ziwe ni juu yenu ukiwasikiliza ndugu ipo siku utalia kilio cha mbwa mwizi.
Ni hayo tu
 
nashukuru mkuu, kadi ya kliniki ndivyo inavyoonyesha kwa mtiririko wa mahidhurio ya kliniki kwamba kwa sasa yuko wiki ya 38 na wamesema itaenda hivyo hadi wiki ya 40 ila lolote linaweza kutokea sasa ndivyo walivyosema. lakini nashukuru sana kwa ushauri wako mkuu maana bado ni kijana mdogo kwa kweli.
 
Back
Top Bottom