Ushauri: Mume wangu ni mlevi sana

Ushauri: Mume wangu ni mlevi sana

sergent

Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
17
Reaction score
8
Jamani kwema,

Mimi ni mwanamke nimeolewa na tuna miaka kumi kwenye ndoa na mume wangu,tuna watoto 4,wakike wawili na kiume wawili. Jamani naombeni msaada wenu mume wangu amekua cha pombe mbaya.

Utadhani anazioga na anarudi nyumbani alfajiri yuko tungi hata hanijali tena na watoto, mi nafanya kazi kwenye taasisi moja siitaji mume wangu pia anafanya kazi wote tumeajiriwa sehemu tofauti.

Lakini mume anapenda tendo la ndoa mno kila akirudi alfajiri lazima tufanye na tunachelewa kufika maofisini na foleni ya Dar kila siku barua ya onyo nimechoka na hii hali.

Jamani nifanyeje apunguze pombe maanayake inakwamisha maendeleo,atalewa laki 3 anarudi nyumbani bila hata mia nahudumia familia mwenyewe naelemewa.

Nisaidieni ushauri jamani
 
hahahha jamii forum vever boaring jamani ,ila shukuru pia unapata tendo la ndoa maana mwingine analewa na anashinda kwa mchepuko hivyo hata utam hawapat ww mbona unabahati hebu ongea na mume nn kinamsumbua yamkin anatatizo kaa nae zungumza nae ukimya kataa
 
Pole sana mkuu,hizo ni changamoto kali sana za ndoa tunazokutana nazo,ila ushauri wangu ni huu;

Kama tatizo limeanza karibuni na hapo mwanzo halikuwepo basi jaribu kuchunguza maeneo haya;inawezekana ana tatizo la kiafya linamsibu na anashindwa kukuweka wazi,ana matatizo kazini kwake au hata hiyo ndoa yenu inawezekana ikawa inachangamoto nyingine ambayo ameshindwa kuivumilia au kuisahau.

Wanaume ni zaidi ya tuwaonavyo inawezekana pia kuna sehemu alijiweka kimahusiano na akaiamini sana na kuweka nguvu nyingi kipesa sasa hivi imemtenga au kupigwachini(Ngumu kumeza hii)

Shirikisha familia,rafiki zake na viongozi mbalimbali wa dini kwa imani yenu ili wakusaidie na naomba usichoke kupambana na ndoa yako ili ikae sawa.

Mungu ndio msaada wa yote haya kwa hiyo usiache kumuomba.
 
Njia rahisi ni hizi:-

Mpeleke msibani = atapata mauidhaa...
Mpeleke Hosiptali akazuru ICU = atajifunza kuheshimu afya...
Mpeleke Magereza akazuru wafungwa = atajilaumu....
Mpeleke Safari kwa basi au Mtumbi = ataona mashaka na shida....
Mpeleke Msikiti au kanisani........
sergent
dawa ni hizo tu!!
 
Last edited by a moderator:
Mkamulie maziwa yako kama unanyonyesha bibie!!trust me atatapika hatareee na hapo ndo utakua mwisho wa kua chapombe!! Ila hizi ndoa jaman mnavumilia mengiii
 
Pombe haina dawa. Wewe nenda kamseme kwa mama yake

Dawa Hii hapa

fungua bar home. ikifika SAA kumi na mbili jioni wewe na binti zako mnaingia Kwenye vazi nusu uchi.... watoto wa kiume wanachoma nyama..... Mbona baba ataipenda bar ya home na Raha, furaha na amani vitaongezeka mara dufu ndani ya nyumba yenu
 
miaka 10 ya ndoa watoto wanne nilishangaa na kubaki na swali imekuaje ?
ila uliposema mumeo anapenda mchezo sana nikawa nimepata jibu
hayo mengine ni changamoto usingekua nazo wewe angekua nazo mwengine
 
Mkamulie maziwa yako kama unanyonyesha bibie!!trust me atatapika hatareee na hapo ndo utakua mwisho wa kua chapombe!! Ila hizi ndoa jaman mnavumilia mengiii

Mjukuu sikujua we ni daktare... Mahari imeongezeka. Mkwe analo
 
fungua bar home. ikifika SAA kumi na mbili jioni wewe na binti zako mnaingia Kwenye vazi nusu uchi.... watoto wa kiume wanachoma nyama..... Mbona baba ataipenda bar ya home na Raha, furaha na amani vitaongezeka mara dufu ndani ya nyumba yenu

dont talk like this it hurt......
hujui tu kiukweli
 
Mkamulie maziwa yako kama unanyonyesha bibie!!trust me atatapika hatareee na hapo ndo utakua mwisho wa kua chapombe!! Ila hizi ndoa jaman mnavumilia mengiii

real???

aisee ila inaonyesha hana watoto wadogo na inaonekena kama hana mpanho wa kuzaa tena
UNAWEZA TUMIA MAZIWA YA MWINGINE?
 
dont talk like this it hurt......
hujui tu kiukweli

Tunamrahisishia. Angekuwa anapenda kusaka suluhu ya kweli ya shida yake angeingia magotini, angefunga na kuomba ili Mungu amnusuru mumewe, lakini kwa Kuwa yeye maana suluhu LA tatizo lake liko Jamii Forums.... wacha wana JF tumpe masolution ya kufa MTU.

NB:-
akiona hajapata suluhu atumie njia Hii.......
Njooni kwangu , ninyi nyote msumbukao na
wenye kulemewa na mizigo, nami
nitawapumzisha. "- Yesu (Mt 11:28)
 
nadhani jibu hili ndo lingekua la kwanza
 
Dah huyo inabidi utumie formula ya kupanda na kushuka unampandia huko ulevini sio kishari kwa upendo unagonga nae drinks taratibu unamuelekeza huku mkizipunguza day by day trust me atapunguza na kurudi kujali familia.
 
fungua bar home. ikifika SAA kumi na mbili jioni wewe na binti zako mnaingia Kwenye vazi nusu uchi.... watoto wa kiume wanachoma nyama..... Mbona baba ataipenda bar ya home na Raha, furaha na amani vitaongezeka mara dufu ndani ya nyumba yenu

mhhhhh bujibuji ushauri gani huo
 
Tafuta source ya tabia hiyo usipoipata ujue source ni wewe. Ongea nae
 
Back
Top Bottom