Ushauri: Mume amenitamkia kuwa hanitaki

Ushauri: Mume amenitamkia kuwa hanitaki

tehamo09

Member
Joined
May 14, 2015
Posts
5
Reaction score
0
Habarini ndugu zangu,

Jamani hapa nilipo nimechanganyikiwa mwanaume amenitamkia hanitaki na mimi moyo bado haujaridhia kosa silioni, nafikiria watoto roho inaniuma mpaka basi. Nataka nirudi tu nyumbani ila moyo unaniuma sana.

Nisaidieni kimawazo nifanyaje?
 
Kaa naye mwongee kwa kina utajua tuu kosa liko wapi wangu. Wanaume huwa hatukurupukagi kwenye maamuzi ya mwisho hapo kuna kitu kashindwa kukivumilia kitabia etc.
 
Mna familia ya watoto wangapi mpaka sasa iv?.
 
tehamo09

Muulize je anawataka watoto akisema ndio mwambie watoto wanakutaka mama yao hivyo mwambie nini umekosa ujirekebishe kwa ajili ya kulea wanenu
 
Last edited by a moderator:
Kaa naye mwongee kwa kina utajua tuu kosa liko wapi wangu. Wanaume huwa hatukurupukagi kwenye maamuzi ya mwisho hapo kuna kitu kashindwa kukivumilia kitabia etc.
nimeongea naye akaniambia yeye hana tatizo na mimi ila ndugu zangu ndo tatizo kisa wanatupush kila siku tubariki ndoa
 
Umechanganyikiwa kisa kakuacha? Au kisa unawaza utaishije bila money yake. Usilazimishe penzi
 
Muulize je anawataka watoto akisema ndio mwambie watoto wanakutaka mama yao hivyo mwambie nini umekosa ujirekebishe kwa ajili ya kulea wanenu

Yote nimemueleza ila amekataa kabisa ila nikikaa baada ya muda anajirudi ananiambia ananipenda sana ila hataweza kuishi na mimi
 
nimeongea naye akaniambia yeye hana tatizo na mimi ila ndugu zangu ndo tatizo kisa wanatupush kila siku tubariki ndoa

Ahaa kumbe jambo lenyewe ndo hilo. Kaa naye chini muongee afu huenda ulionesha mrengo mkubwa kwa wazaz wako sana. Jambo kama hilo ni la kwenu mkae mjadiliane na kwann mda wote huo watoto watatu bila ndoa duuh! Ila bado hujachelewa unaweza mbadilisha mtizamo wake na akawa sawa tuu.
 
pole@tehamo09 unatakiwa kuvumilia.hapa naona bado ujapata ushauri muafaka.jaribu utafute marafiki zake na majirani wema ili umshawishi kwa mapenzi ya watoto.watoto ndio watapo umia wewe tayari umekubali kuenshi na mwanaume miaka yote bila ndoa.Lakini watoto hao hawalikubali na kisha walijue.Mfahamishe vizuri ili muweze kulea watoto.Na jaribu uongee na uongozi yoyote kuhusu hilo suala la watoto.
Ukipata sulihisho la amani funga harak ndoa ili watoto waweze kuenshi katika upendo wa familia
 
Kwa maelezo yako mumeo Ana mapenzi na wewe ila Kuna "ndoa" yenu kuingiliwa na ndugu zako. Waombe wasilazimishe mambo Bali watoe ushauri, kama mahali alishatoa hapo "Tatizo lipo wapi?"
 
Ukikubali kuishi na mtu bila contract yoyote mwisho jamaa anachukua advantage. Pole!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ahaa kumbe jambo lenyewe ndo hilo. Kaa naye chini muongee afu huenda ulionesha mrengo mkubwa kwa wazaz wako sana. Jambo kama hilo ni la kwenu mkae mjadiliane na kwann mda wote huo watoto watatu bila ndoa duuh! Ila bado hujachelewa unaweza mbadilisha mtizamo wake na akawa sawa tuu.
Una mawazo mazuri ya kujenga. Ukweli wake zetu wanatuponza sana wanapokumbatia ndugu zao!!! Ndoa ni ya watu wawili akijumuika wa tatu ni shida sana. Heko kwa ushauri mwanana
 
Pole sana haya ndio matatizo ya kuamua kuishi na njemba bila ndoa na kuamua kuwa na watoto nje ya ndoa. Mwingine angethamini muda mlioishi pamoja na watoto mliojaliwa lakini huyu si hivyo si ajabu hata watoto anaweza kuwatelekeza.
 
Back
Top Bottom