Ushauri: Mtalaka anatishia kuvunja ndoa mpya ya rafiki yangu

livewise1

JF-Expert Member
May 25, 2019
837
952
Habari wakuu!

Kuna jamaa yangu amenipa kisa kilichomtokea nibaab-kubwa, na anaomba mawazo mbadala au kama yeye yuko sahihi pia aendelee.

Mwaka juzi alikuwa mkoa wa Mara akifanya kazi kama msaidizi wa familia ya mama mwenye kampuni ya utalii. Huyo mama alimuamini ikafika hatua amemuelekeza mambo yote hapo nyumbani maana yeye mama sio mkaaji sana nyumbani kutokana na kupokea na kupeleka watalii vivutioni kanda hiyo. Kazi ilikuwa inamlipa jamaa kiasi kwamba akaamua akirudi kwao Kigoma akaanzishe biashara ya duka na kutafta mwenza aowe jambo ambalo alifanikiwa.

MCHAKATO WA KUOWA;
Alikuwa amemlenga binti mmoja kati ya kundi la wasichana watatu ambao walikuwa ni marafiki, alipoanza kufanya mchakato wa kumtaka mlengwa kuna msichana baina yao akavuruga mpango na kujiweka yeye. Jamaa akaambiwa ‘’UKINIOWA MIMI SITOTAJA MAHARI NYINGI HALAFU MIMI NAKUPENDA TANGU ZAMANI WALA SINA TAMAA LABDA NA DUKA LAKO’’ KWANZA MARY ANA MCHUMBA WAKE YUPO DAR NA WAZAZI WAKE WANAJUA HILO UKIENDA HUTAKUBALIWA.

Jamaa akaona isiwe kesi maana pia alivoambiwa anapendwa akaona hapa sitasumbuka sana kutengeneza familia. Akaenda kuposa akaowa huyo binti kwa mahari ya laki 6 na maisha yakaanza.

KURUDI KAZINI;
Ghafla jamaa akaitwa na mama wa Mara kuwa kazi zimekuwa nyingi na akaambiwa atapewa bonasi zaidi…kwa kuwa jamaa alikuwa ana mpango wa kurudi baada ya mwezi 1, akaona basi ngoja atangulie bila mke baadae atampeleka tu. Hapo alikuwa ametumia wiki mbili tu na bibie ndani ya ndoa, akaaga na kwenda kazini…alipofika Mara, wiki moja tu mkewe akampigia simu kuwa mamake hampendi anamtesa na kumsimanga mno…alimpigia mamake na kutaka kujua tatizo nin?

MAAJABU;
Mama akasema maneno machache tu, ‘’MWANANGU UMEOWA MKE ANA MIMBA TENA HII BILA SHAKA NI MIEZI 3 KABISA’’ mshituko mkubwa ukichanganyika na hasira za ghafla zilimjia na kupata shauku ya kudadisi mama kajuaje na mbona jamaa hakuona/kuhisi kitu? Mama akasema ugomvi wao ni kuwa, anataka mkwewe aseme mimba ile ni ya nani? Bibie hataki na anasema ya mtoto wao wakati jamaa hakuwahi kuingiliana nae (kwa maelezo ya jamaa mwenyewe) kabla ya ndoa na ndoa ina wiki 2 tangu jamaa aondoke nyumbani.

Akaishi kwa stress sana na kukonda mpaka mama boss akawa anamuuliza, ‘’MWANANGU TATIZO NINI MBONA KAMA UNAPOTEZA MWILI WAKO WA KIGOMA, UNAKONDA VIPI UMEANZA KUWA MVIVU KULA? Akawa hasemi maana hata mama boss hajui kuwa jamaa ameowa.
MIEZI 2 BAADAE;
Miezi miwili baadae jamaa akarudi kushughulikia jambo hilo, akaja kumbana bibie kisawasawa ikiwemo kumtishia kumuuwa ikiwa hatosema ukweli…mara paaa…binti akasema aliwa kubakwa mwaka mmoja ulio pita.

‘’MWAKA MZIMA HUKUZAA UJE UWE NA MIMBA YA MIEZI 3 SAIVI, UTASEMA TU KAMA HUSEMI NAKUMALIZA USIKU HUU HUU, HAPO ALIKUWA AMEMSHIKIA KISU HUKU AKIWA ANATETEMEKA’’

Baadae akaona hapa ntaenda jela bure hapa, akamwacha akatoka zake akaenda kwa mdogo wake yule anaemsaidia kuuza duka…kesho yake akarudi Mara…siku mbili akapigiwa simu kuwa MKEWE AMESEPA KWAO BILA KUAGA.

KUJIFUNGUA;
Baada ya miezi 3 mingine binti akajifungua mtoto wa kike nyumbani kwao…wakwe wakapiga simu kwa wakwe wenzao lakini jamaa Pamoja na wazee wake hawakuonesha ushirikiano wowote maana washajua hapa tumepigwa…AKAMTAKIA AFYA NJEMA NA KUMWAMBIA NDOA YAKE IMESHAKUFA TALAKA YAKE ATAPELEKEWA HUKO HUKO KWAO… hakutaka kuyajenga, na akarudi tena kuja kutafuta mke mwingine.

KUOWA MARA YA PILI;
Haikuwa kazi ngumu maana watu wengi wenye mabinti walimjua ukijumlisha na kauchumi kaliongezeka kwa hiyo akapatiwa mtoto mmoja wa ostaadhi pale kijijini kwao mambo hayakuwa mengi. Wazazi wake walimgomea wakamwambia aowe mtoto wa ndugu yao asitafute matatizo kama yaliyopita, ila jamaa akakaza na kusema huyo ndio amemchagua yeye na wamependana na ana maadili mazuri. Wazazi wake wakamwambia basi USITUHUSISHE NA NDOA YAKO MAANA WE NI SIKIO LA KUFA.

Jamaa akateta na upande wa pili mambo yakaenda kibishi tu…lakini baada ya wiki moja tu wakwe zake wakafa kwa maji mtoni walikuwa wanavuka kutoka mashambani kumbe mto una nguvu na umechimba chini. Msiba ukafanyika lakini ushirikiano kutoka kwa wazazi wa jamaa ni sifuri yaani.

Yule binti wa mwanzo alisogezwa tukae na jamaa mwingine tu aliekubali kulea mtoto sio wake. Jamaa kafungua genge sokoni na kila mtalaka wake akija sokoni na mwenzie wanamkwepa sana lakini jamaa hakuwa na roho ya kwanini maana mzigo ulishamshinda. Yule mke wa jamaa akaanza kumwambia jamaa kuwa MTALAKA WAKO BADO ANAKUTAKA MAANA ANAKUJA KUNITUKANA NA KUSEMA KUWA BADO MNAPENDANA ISPOKUWA MAMAMKWE NDIO KIKWAZO KWAKE.

Jamaa alikasirika na kumfuata yule mtalaka kumpiga mkwara mbele ya mwenzie ili ijulikane wazi…mtalaka wake akamwambia ‘’NTAHAKIKISHA HUDUMU NA HUYO KINYAGO WAKO, HAWEZI KUNIPORA MUME WANGU MIMI HALAFU NIMUANGALIE TU’’

CHA KUFANYA;
Kwa upande wake jamaa anasema anataka ampeleke polisi maana akitaka kuchukua hatua mkononi anaona kabisa kuna kuozea jela.

Pia anataka aende na mkewe Mwanza maana kule kwa mama alishaacha baada ya kushindwa kutulia kutokana na matatizo hayo, LAKINI MKEWE WA HIVI SASA ANAKATAA KUTOKA NJE YA KIJIJI KWA MADAI HAWEZI KUISHI NJE YA HAPO KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA (ANA KIFAFA) AMBACHO KINAMJIAGA MARA KADHAA KWA MWEZI.

Amepata dili mgodini Mwanza kwa mjomba wake akasimamie kazi ambayo itampa pesa na ndio dili ambalo anaona litampaisha kiuchumi, hapo hapo anaona kuishi mbali na mkewe ni ngumu kwa sababu hajui yule mtalaka anataka kufanya nini kwa ile kauli yake na ukizingatia watu wanasemaga TAHADHARI KABLA YA HATARI.

Ushauri wenu tafadhali mimi nimeona huku anaweza kupata mawazo mbadala.
 
Vijana mnAnaoa kwa kukurupuka ndo shida...

Mwanamke unayetaka kumuoa walau minimum 2years of close relationship ni muhimu..

Umepata vipesa kidogo unaparamia mwanamke unataka kuoa.

kwani huyo jamaa hakuwa na mwanamke huko Mara mpaka aende kigoma na ushamba wake wa kutaka kuoa kabila moja km sheria.

Usioe mwanamke km hamna zaidi ya miaka miwili swala la kuoa si km kutafuta hela,kichwani inabidi umuandae mwanamke unayetaka kumuoa na lzm uwe na plans and options tena km wewe ni mkristo ndo koma kabisa kukurupuka.

Wenzetu waislamu mkishindwana unapiga chini unatafuta mwingine akizingua unabamiza chini hivyo hivyo mpk upate wa kueleweka
 
Migogoro ya maisha hasa ya ndoa haijawahi kuisha salama lazima ushirikina utahusika tuu, ila me naona jamaa angetumia busara kukaa chini na huyo mwanamke ili wayamalize
 
Vijana mnAnaoa kwa kukurupuka ndo shida...

Mwanamke unayetaka kumuoa walau minimum 2years of close relationship ni muhimu..

Umepata vipesa kidogo unaparamia mwanamke unataka kuoa.

kwani huyo jamaa hakuwa na mwanamke huko Mara mpaka aende kigoma na ushamba wake wa kutaka kuoa kabila moja km sheria.

Usioe mwanamke km hamna zaidi ya miaka miwili swala la kuoa si km kutafuta hela,kichwani inabidi umuandae mwanamke unayetaka kumuoa na lzm uwe na plans and options tena km wewe ni mkristo ndo koma kabisa kukurupuka.

Wenzetu waislamu mkishindwana unapiga chini unatafuta mwingine akizingua unabamiza chini hivyo hivyo mpk upate wa kueleweka
Tatizo tunaamini ukilemba tuu wenzako wanakuja wanazoa Asa ukiona demu nikisu unaona bora niweke ndani

Hii ilitokea ktk familia yetu jamaa kamtia mimba dogo kumbe hajui hata Dini yake wala kabila lake eti kisa mwenzangu namimi nimweupe 1kwa1 akajua ni Mpemba

Daah tunakurupuka sana sisi hasa tukiona demu mkali ndiyo kabisa tunataka kujimilikisha
 
Habari wakuu!
Kuna jamaa yangu amenipa kisa kilichomtokea nibaab-kubwa, na anaomba mawazo mbadala au kama yeye yuko sahihi pia aendelee.

Mwaka juzi alikuwa mkoa wa Mara akifanya kazi kama msaidizi wa familia ya mama mwenye kampuni ya utalii. Huyo mama alimuamini ikafika hatua amemuelekeza mambo yote hapo nyumbani maana yeye mama sio mkaaji sana nyumbani kutokana na kupokea na kupeleka watalii vivutioni kanda hiyo. Kazi ilikuwa inamlipa jamaa kiasi kwamba akaamua akirudi kwao Kigoma akaanzishe biashara ya duka na kutafta mwenza aowe jambo ambalo alifanikiwa.

MCHAKATO WA KUOWA;
Alikuwa amemlenga binti mmoja kati ya kundi la wasichana watatu ambao walikuwa ni marafiki, alipoanza kufanya mchakato wa kumtaka mlengwa kuna msichana baina yao akavuruga mpango na kujiweka yeye. Jamaa akaambiwa ‘’UKINIOWA MIMI SITOTAJA MAHARI NYINGI HALAFU MIMI NAKUPENDA TANGU ZAMANI WALA SINA TAMAA LABDA NA DUKA LAKO’’ KWANZA MARY ANA MCHUMBA WAKE YUPO DAR NA WAZAZI WAKE WANAJUA HILO UKIENDA HUTAKUBALIWA.
Jamaa akaona isiwe kesi maana pia alivoambiwa anapendwa akaona hapa sitasumbuka sana kutengeneza familia. Akaenda kuposa akaowa huyo binti kwa mahari ya laki 6 na maisha yakaanza.

KURUDI KAZINI;
Ghafla jamaa akaitwa na mama wa Mara kuwa kazi zimekuwa nyingi na akaambiwa atapewa bonasi zaidi…kwa kuwa jamaa alikuwa ana mpango wa kurudi baada ya mwezi 1, akaona basi ngoja atangulie bila mke baadae atampeleka tu. Hapo alikuwa ametumia wiki mbili tu na bibie ndani ya ndoa, akaaga na kwenda kazini…alipofika Mara, wiki moja tu mkewe akampigia simu kuwa mamake hampendi anamtesa na kumsimanga mno…alimpigia mamake na kutaka kujua tatizo nin?

MAAJABU;
Mama akasema maneno machache tu, ‘’MWANANGU UMEOWA MKE ANA MIMBA TENA HII BILA SHAKA NI MIEZI 3 KABISA’’ mshituko mkubwa ukichanganyika na hasira za ghafla zilimjia na kupata shauku ya kudadisi mama kajuaje na mbona jamaa hakuona/kuhisi kitu? Mama akasema ugomvi wao ni kuwa, anataka mkwewe aseme mimba ile ni ya nani? Bibie hataki na anasema ya mtoto wao wakati jamaa hakuwahi kuingiliana nae (kwa maelezo ya jamaa mwenyewe) kabla ya ndoa na ndoa ina wiki 2 tangu jamaa aondoke nyumbani.
Akaishi kwa stress sana na kukonda mpaka mama boss akawa anamuuliza, ‘’MWANANGU TATIZO NINI MBONA KAMA UNAPOTEZA MWILI WAKO WA KIGOMA, UNAKONDA VIPI UMEANZA KUWA MVIVU KULA? Akawa hasemi maana hata mama boss hajui kuwa jamaa ameowa.
MIEZI 2 BAADAE;
Miezi miwili baadae jamaa akarudi kushughulikia jambo hilo, akaja kumbana bibie kisawasawa ikiwemo kumtishia kumuuwa ikiwa hatosema ukweli…mara paaa…binti akasema aliwa kubakwa mwaka mmoja ulio pita.
‘’MWAKA MZIMA HUKUZAA UJE UWE NA MIMBA YA MIEZI 3 SAIVI, UTASEMA TU KAMA HUSEMI NAKUMALIZA USIKU HUU HUU, HAPO ALIKUWA AMEMSHIKIA KISU HUKU AKIWA ANATETEMEKA’’
Baadae akaona hapa ntaenda jela bure hapa, akamwacha akatoka zake akaenda kwa mdogo wake yule anaemsaidia kuuza duka…kesho yake akarudi Mara…siku mbili akapigiwa simu kuwa MKEWE AMESEPA KWAO BILA KUAGA.

KUJIFUNGUA;
Baada ya miezi 3 mingine binti akajifungua mtoto wa kike nyumbani kwao…wakwe wakapiga simu kwa wakwe wenzao lakini jamaa Pamoja na wazee wake hawakuonesha ushirikiano wowote maana washajua hapa tumepigwa…AKAMTAKIA AFYA NJEMA NA KUMWAMBIA NDOA YAKE IMESHAKUFA TALAKA YAKE ATAPELEKEWA HUKO HUKO KWAO… hakutaka kuyajenga, na akarudi tena kuja kutafuta mke mwingine.

KUOWA MARA YA PILI;
Haikuwa kazi ngumu maana watu wengi wenye mabinti walimjua ukijumlisha na kauchumi kaliongezeka kwa hiyo akapatiwa mtoto mmoja wa ostaadhi pale kijijini kwao mambo hayakuwa mengi. Wazazi wake walimgomea wakamwambia aowe mtoto wa ndugu yao asitafute matatizo kama yaliyopita, ila jamaa akakaza na kusema huyo ndio amemchagua yeye na wamependana na ana maadili mazuri. Wazazi wake wakamwambia basi USITUHUSISHE NA NDOA YAKO MAANA WE NI SIKIO LA KUFA. Jamaa akateta na upande wa pili mambo yakaenda kibishi tu…lakini baada ya wiki moja tu wakwe zake wakafa kwa maji mtoni walikuwa wanavuka kutoka mashambani kumbe mto una nguvu na umechimba chini. Msiba ukafanyika lakini ushirikiano kutoka kwa wazazi wa jamaa ni sifuri yaani.
Yule binti wa mwanzo alisogezwa tukae na jamaa mwingine tu aliekubali kulea mtoto sio wake. Jamaa kafungua genge sokoni na kila mtalaka wake akija sokoni na mwenzie wanamkwepa sana lakini jamaa hakuwa na roho ya kwanini maana mzigo ulishamshinda. Yule mke wa jamaa akaanza kumwambia jamaa kuwa MTALAKA WAKO BADO ANAKUTAKA MAANA ANAKUJA KUNITUKANA NA KUSEMA KUWA BADO MNAPENDANA ISPOKUWA MAMAMKWE NDIO KIKWAZO KWAKE. Jamaa alikasirika na kumfuata yule mtalaka kumpiga mkwara mbele ya mwenzie ili ijulikane wazi…mtalaka wake akamwambia ‘’NTAHAKIKISHA HUDUMU NA HUYO KINYAGO WAKO, HAWEZI KUNIPORA MUME WANGU MIMI HALAFU NIMUANGALIE TU’’

CHA KUFANYA;
Kwa upande wake jamaa anasema anataka ampeleke polisi maana akitaka kuchukua hatua mkononi anaona kabisa kuna kuozea jela.

Pia anataka aende na mkewe mwanza maana kule kwa mama alishaacha baada ya kushindwa kutulia kutokana na matatizo hayo, LAKINI MKEWE WA HIVI SASA ANAKATAA KUTOKA NJE YA KIJIJI KWA MADAI HAWEZI KUISHI NJE YA HAPO KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA (ANA KIFAFA) AMBACHO KINAMJIAGA MARA KADHAA KWA MWEZI.

Amepata dili mgodini mwanza kwa mjomba wake akasimamie kazi ambayo itampa pesa na ndio dili ambalo anaona litampaisha kiuchumi, hapo hapo anaona kuishi mbali na mkewe ni ngumu kwa sababu hajui yule mtalaka anataka kufanya nini kwa ile kauli yake na ukizingatia watu wanasemaga TAHADHARI KABLA YA HATARI.

Ushauri wenu tafadhali…mimi nimeona huku anaweza kupata mawazo mbadala.
Wajuvi Mkuje kutiririka huku
 
Mkioana nyote akili zinafanana ni kaz sana. Inabidi huyo jamaa asimame kama mwanaume sasa vitu vingine sio vya kubembelezana.
 
Tatizo tunaamini ukilemba tuu wenzako wanakuja wanazoa Asa ukiona demu nikisu unaona bora niweke ndani

Hii ilitokea ktk familia yetu jamaa kamtia mimba dogo kumbe hajui hata Dini yake wala kabila lake eti kisa mwenzangu namimi nimweupe 1kwa1 akajua ni Mpemba

Daah tunakurupuka sana sisi hasa tukiona demu mkali ndiyo kabisa tunataka kujimilikisha
Duh.
 
Back
Top Bottom