Ushauri: Mpenzi wake anavuta sigara

the viking

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
1,170
1,372
Hali vipi wanajamvi?

Nina mshikaji wangu na ambaye ni mwenzangu kazini majuzi haya amegundua mpenzi wake ana uraibu mkubwa wa sigara kwa taarifa aliyonipa ni kwamba hili ni jipya kwake kwani hajapata kulijua tangu walipoanza mapenzi yao na sasa ana wasiwasi kwani anampenda sana na anatarajia kufunga ndoa naye ila hili la uvutaji sigara limemnyima pozi kabisa, nawaombeni ushauri wenu kwa niaba yake.

Asanteni
 
Wamejuana kwa muda gani? Kama huyo jamaa ni addicted smoker huyu bibie hajawahi kuhisi harufu wakiwa wana kiss? Nijuavyo nicotine kwa mzoefu unaweza kuisikia hata akiwa anatoka kuoga.
 
demu kuvuta sigara ni ajabu kwa utamaduni wetu ila ukitembea kidgo kwa wenzetu sigara ni stimu tuu na ni staree kama mtu anavyokunywa pombe/soda ili mradi asivutie ndani.
 
Wamejuana kwa muda gani? Kama huyo jamaa ni addicted smoker huyu bibie hajawahi kuhisi harufu wakiwa wana kiss? Nijuavyo nicotine kwa mzoefu unaweza kuisikia hata akiwa anatoka kuoga.
wakati mwingine si rahisi kuhisi ile harufu ukizingatia hawako pamoja ila hupatana mara kwa mara katika miadi yao..hivyo huyu mwanadada anaweza akawa ile harufu ana njia za kuidhibiti..tena kuna sigara ambazo zina ile mint ta kupunguza harufu mfano danhill
 
demu kuvuta sigara ni ajabu kwa utamaduni wetu ila ukitembea kidgo kwa wenzetu sigara ni stimu tuu na ni staree kama mtu anavyokunywa pombe/soda ili mradi asivutie ndani.
mkuu huoni hili laweza kuwa tatizo la kiafya kwa siku za halafu?tena wafahamu athari zake kama mwanamke ana ujauzito..
 
Njia pekee ya kumsaidia ni kwanza huyu dada akubali kuwa hili ni tatizo na anahitaji msaada
 
mkuu huoni hili laweza kuwa tatizo la kiafya kwa siku za halafu?tena wafahamu athari zake kama mwanamke ana ujauzito..

haina shida akiwa na mimba apunguze.

haina tofauti na pombe kuna wachina wanakula sigara sana wanazaa vizuri ukiuliza historia wazazi wao na walikuwa chain smoker.

sigara ni kama vitu vingine tunavyotumia sisi ambao sio wavutaji kama pombe unga chewing drugs. vyote ni tatizo. na sio kila mwili sigara inakataa mtu kuna watu wanavuta 40 years wako kawaida tuu
 
Njia pekee ya kumsaidia ni kwanza huyu dada akubali kuwa hili ni tatizo na anahitaji msaada
ushauri anaoutaka ni wa kumsaidia kubainisha hatua atakayochukua..kama kuna matarajio ya kuwa huyu mpenziwe anaweza kuacha kabisa hana tatizo ila kama sivyo basi..
ndio lakini msaada wa kisaikolojia ni muhimu..atakubali kubadilika tu akisaidiwa
nitafikisha ushauri kaka..asante
 
haina shida akiwa na mimba apunguze.

haina tofauti na pombe kuna wachina wanakula sigara sana wanazaa vizuri ukiuliza historia wazazi wao na walikuwa chain smoker.

sigara ni kama vitu vingine tunavyotumia sisi ambao sio wavutaji kama pombe unga chewing drugs. vyote ni tatizo. na sio kila mwili sigara inakataa mtu kuna watu wanavuta 40 years wako kawaida tuu
asante mkuu kwa ushauri..ila si sawa kabisa mwanamke kutumia sigara..
 
Back
Top Bottom