Nimeoa 2015 kwa ndoa halali kabisa kwa mapenzi ya Mungu mke akapata mimba, tukakaa baada ya miezi saba mke akasema hawezi jifungulia hapa nilipo ni lazima ajfungulie nyumbani kwao.
Mimi nikasema sawa kulingana na Mila zetu hutaenda nyumbani kwenu bali utaenda kwetu akasema sawa. Nikatafuta nauli akaenda nyumbani kwa sababu nyumbani ni mbali alisafiru peke yake kwa sababu nauli mtu mmoja Kama 85 elfu nauli peke yake.
Baada ya kufika nyumbani wazazu wangu wakampokea na kufurahi.
Baada ya wiki moja akamwambia baba yangu anataka kwenda kwao, baba akamwambia kwani mlipangaje na mume wako wakati wazazi niliwapa taarifa ya kuja huko kujifungua wakashukuru na kufurahi.
Baba akamwambia ngoja niongee na mumeo nisikie anasemaje yeye akamjibu baba mkwe kuwa sikuombi nauli bali ni taarifa nakupa. Baada ya siku moja akabeba mizigo yake akaondoka mama yangu akamzuia ili asubiri maelekezo yangu akakataa.
Baada ya miezi miwili akajifungua huko kwao taarifa nilipewa na wazazi wangu kwani wao walipata kwa mshenga. Yeye toka alivyoenda kwao simi yangu alikuwa hapokei. Baada ya kujifungua mama yangu akaenda huko kumuona na mambo yote yanayomhusu mzazi na mimi nikatuma pesa kupitia mama mkwe kwan ndio tulikuwa tunaongea kwenye simu.
Baada ya miezi miwili nikampigia simu mama mkwe kwa kumuomba nimtumie nauli arudi kwangu kwan kwa wakati huo nilikuwa bize na masomo nisingeweza kwenda huko. Mama mkwe hakutoa jibu na mke wangu jibu alilotoa alisema huko siwezi kurudi, sababu hakuniambia nikasema acha nimuongezee muda labda atabadilika.
Kibaya zaidi akakataa kumleta mwanangu kwa bibi yake na babu yake kitu ambacho wazazi wangu wamechukia kwa sababu nauli kutoka kwao mpaka kwa wazazi wangu ni sh 2000 tu. Wazazi wake wakakata mawasiliano na wazazi wangu.
Mimi nikiwapigia simu kuhusu kurudi kwa mke wangu wanasema hawajui atarudi lini, na kibaya zaidi alibadili laini ambayo mimi siijui ili nisimsumbue.
Mpaka sasa mtoto ana mwaka mmoja na nusu hajui kwao, ninapopata hela ya matumizi natuma kwa mama mkwe kwani toka mama mkwe aseme kunitumia no mpya hiyo mwaka unaenda.
Nilimuoa kwa ndoa halali na kumthamni kwani wazazi wake walitaka mahari nyingi kama milioni na nusu na wazazi wangu wakatoa na harusi kubwa ikachezwa.
Ushauri ninaomba je huyo mwanamke niachane nae nitafute mwingine au nifanyeje maana umri unasogea now nina 32years na wazazi wangu wanaonyesha moyo wakutokutaka nirudiane nae kwani wanasema wamedharauliwa na wazee wenzao.
Ushauri please, nifanyeje nakosa maamuzi.
Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app