Ushauri: Mke kakata Mawasiliano

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
366
1,375
Salaam wanajamvi

Nina Mke na watoto wawili na mmoja ni kijacho

Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke huyu kwa miaka 9 na mwaka Jana tukafunga ndoa ya bomani maana kila mmoja Ana imani yake na hakuna Kati yetu alietaka kubadili na kimfuata mwenzake.

Miaka ya nyuma mapenzi yalikuwa safi Mawasiliano yalikuwa imara Sana,yeye na Mimi tunaishi mikoa jirani Kama Km 220 hivi

Yeye ni muajiriwa na Mimi ni muajiriwa sekta binafsi ambayo salary yake ni ndogo so Mke kanizidi parefu Sana.

Sasa tangu mwaka Jana mwezi wa 6 Mawasiliano Kati yetu yamekuwa finyu mnoo na tuna migogoro ya mara kwa mara na chanzo Cha migogoro hii ni kunituhumu Mimi nachepuka baada ya kupata story toka kwa majirani.

Nimejaribu kuzungumza nae Sana ,mwenzangu haelewi na sasa ndo kaacha kabisa Mawasiliano na Mimi.

Nisipopiga Mimi hata siku 5 ndio imetoka hiyo,mwanamke hajui kupiga simu hajui kutuma msg,inshort Mawasiliano ya maana Kati yake na yangu hamna.

Ninajitahidi kupiga simu mara kadhaa ili niwajulie hali watoto ila nahisi kukata tamaa.

Mwenzangu anaonekana bado Ana kinyongo na Mimi ,lakini pia hali hii ya Mawasiliano kuwa finyu aliianzisha miaka kadhaa nyuma ila kwa sasa hali imekuwa mbaya Sana.

Ushauri wenu tafadhali jinsi ya kumdhibiti huyu mwanamke ili atambue umuhimu wa Mawasiliano hasa kwa wapenzi ambao wanaishi mbalimbali.

Nimechoka kila wakati nianze kumtafuta Mimi.
 
Si rahisi mwanaume achukue mkeo akiwa na mimba yako na watoto wako wawili moja kwa moja unless ww ni mzembe sana au humtaki tena. Watalala nae ila mwishoni watakuachia mkeo na kiburi chake kitaisha.
 
Endelea kumpgia kila siku, sasa nani atamchukua huyo mwanamke mwenye watoto wawili na mimba juu,

Afu fanya kumtembelea mara nyingi kadri iwezekanavyo na zawadi usisahau kumbebea.

Afu kumbuka kumtumia sms nzuri ukimkumbusha unampenda.
 
Acha kazi umfuate kama hali imekewa mbaya! Ila kabla ya hapo kubalianeni mkope mikopo na muielekeze kwenye mradi mnaoweza kuumudu huku ukiwafanya muishi pamoja! Mie sio muumini wa mapenzi ya simu! Yeye aendeler na kazi yake na wewe usimamie mradi wenu hukohuki aliko mkeo! Niishie hapo!
 
Si rahisi mwanaume achukue mkeo akiwa na mimba yako na watoto wako wawili moja kwa moja unless ww ni mzembe sana au humtaki tena. Watalala nae ila mwishoni watakuachia mkeo na kiburi chake kitaisha.
Shida mkewe ndio anaweza kujichukulia😂!
 
Kubali matokeo tu, ndoa ilishakufa muda tu hapo. Kuna asilimia kubwa hiyo mimba ni mume mwenzio.
 
Mke akijichukulia ni suala la muda tu atarudi kwa mumewe. Unless mume awe mzembe sanaaa au awe hamtaki tena.
Ila uharibifu wake ni mkubwa sana! Irreversible damage inaweza kuwa imeshafanyika na kurudi kwake inakuwa haina maana tena!
 
Mkuu hao ndio wapi hivyo hivyo tu sio wako tu kuna watu umewagusa kwenye point kabisa yaani wake zao wanafanya kama huyo wakwako na hayo matendo ni kwa muda mfupi tu na baadae yeye ndio atakuwa anatoa lawama kwako kuwa humpigii simu jambo la msingi ukipata nafasi ya kuwasiliana naye mtafute stage mliyofikia sio mchezo hao watoto akiwa anawaangalia mawazo yake yanarudi kwako sema ndio hivyo wanajipaga ubize ambao hata wenyewe hawaelewi hivyo isimfikirie vibaya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom