Ushauri; Mkasa mfupi kuhusu familia yangu

273

Member
Sep 12, 2017
63
82
Habari wakuu,

Bila kupoteza mda niende moja kwa moja kwenye mada, nimeandika kiufupi ila ni suala la muhimu sana sana kwa mustakabali wa maisha yangu na familia yetu kwa ujumla.

Mimi ni kijana naetoka kwenye familia yenye baba, mama na watoto kadhaa....nitoe historia ya familia kwa ufupi;

Miaka ya nyuma kidgo Baba yetu alkua ni mwenye kipato cha kati kwa maana kuwa alimudu kutatua changamoto kadha za kiuchumi, nawezasema katk ukoo yeye ndo alkua na uwezo mkubwa kdgo.
Maisha yaliendlea lakin shida ikaja kutokea pale ambapo baba aliingia ktk ugomvi na shemeji yake(mke wa kakaake) kufuatia kutoelewana katk baadhi ya mambo. ugomvi uliopelekea shemeji huyu wa baba kutoa lugha chafu na za chuki ikiwemo "familia zetu haztakuja kupatana kamwe" (yaani familia ya baba na ya kakayake ambae ingawa yupo hai ila akili yake n km haiko sawa;inasemekana alirogwa na mkewe) badae yakafuata mambo mengi yaliyoonekana kama ya kishirikina ikiwemo shemeji huyu wa baba kunyofoa mafunda ya majani ya kuezekea nyumba katk nyumba ya baba iliyokuwepo huko kijijini na kwenda nayo kwake haijulkani alienda kufanyia nn.

Baada ya hapa zikapta siku siku baba akaamua kwenda mkoa mwngne kutafta rizik kwan kila alilokua akishika halishikik(ela ilipotea kabisa).
Stori n ndefu sana ila kwa ufupi n kwamba tangu kipndi hiko baba hajawai kufanikiwa kiuchumi na mbaya zaid n kwamba tatzo lmekuja hadi kwetu wanae kwan licha ya kuwa tumeshakua watu wazma ila huwezi amini hakuna mwenye maendeleo, kila ukifanya kitu baada ya muda mfupi huoni faida ni hasara tu.

Jaman kwanza niulize je, ushirikina upo?? kwan kuna mengi tuliyofanyiwa na huyo shemejiye baba ni vile tu mengne sijayaandka, Hivyo ninaamin kati ya watakao soma huu uzi either wapo ambao wanao uelewa na haya mambo au walishawatokewa na mambo kama haya.

Nachohitaji ni ushauri ikiwezekana ata msaada(wa kutatua tatizo) asee nimechoka na haya maisha ya shida(kushika pesa lakin haikai, yaani hatuna maendeleo kabisa) jaman jaman somebody save my family isiangamie......tunaangamia (immagine ndan ya miaka 30 familia yaani baba na wanae haijawai kujenga hata msingi wa nyumba).
 
Inasikitisha sana yaani hadi leo watanzania tunaamini katika ndumba....Pole mkuu, nenda kaombewe wewe na familia yako
 
Sijui ni wa imani gani lakini kama ni mkristu ukifunga na kukemea kwa jina la Yesu, yatafunguka yote hayo.
 
Pole, matatizo ya kushirikina, ungeni mikono kama familia, pigeni goti na kuomba Mungu ni wa rehema atafungua mipago yote ya kishirikina inayowakabili...

Otherwise cheki na Mshana Jr
 
ongeza bidii katika utafutaji wako, maan familia yako siyo ya kwanza kushindwa kwenye utafutaji, hebu weka hizo dhna za kurogana pembeni tilia mkazo kwenye utafutaji, huo ushirikina chukulia kama changamoto na kitu cha mwisho kabisa ukishaona bidii yote haijafua dafu
 
Omba Mungu Sana tafuta viongozi wa kiroho wenye nguvu utasaidika,Mimi nilipata changamoto ya nguvu za Giza ilinisumbua sana ila nilipoamua kuacha kutumia akili zangu mwenyewe na kumfuata Yesu mambo mengi sana yalibadirika na Amani ilirejea.Hallelujah
 
Pole sana mkuuuu ,,izo mambo zipo sana tena sana .. I have brother of mine yeye jamaa alifanyiwa izo mambo na jiran yake mpaka akafukuzwa kazi nailibaki kidogo sana afungwe maana ( alikua manager mmoja Wa benk ).

Sasa uyu jamaa tunashukuru alisaidika baadae na bahat nzuri amekuja kupata kazi nzuri sana zaidi ila Kibaya Now Mke wake ndo majanga majangaaaa !!!.

Refer ,,uzi mmoja ivi ,,niliwahi sema "* mke wakaka anamnyanyasa mama **.....huyo kaka nilomzungumzia ndo huyu namzungumzia tena.


.izo mambo zipo ,,nawatu hapa dunian kazi yao nikutembelea nyota za watu.
 
Unapopitia mambo magumu katuka maisha halaf ukawa unaamini mambo ya kishirikina utapata wakat mgumu zaidi hata wanaotaka kukusaidia utawaona wabaya.


Watu tulipitia wakati mgumu sana lkn tukachukulia kama changamoto za maisha
 
Jaribu kuwa na diary kwa ajili ya mambo uyafanyayo.Pia uwe na maoteo ya mambo unayotaka kuyafanya upatapo pesa.Pia uwe na note book ya kuandika mapato na matumizi kwa kila siku.Ukisha kuwa na vitu hivyo vitakuwezesha kuona sehemu gani pesa yako inapotelea.Kama fedha yako inapotelea kwenye dharura za mara kwa mara(k.m. michango isiyo na maana,kuhonga ,starehe nakadhalika).Pia angalia maoteo yako umeyafanikisha kwa kiasi gani.Kutokana na hayo utafanya uamzi wa namna ya kuondoa kero.Lakini ukiamua kuwa fedha yako inapotea kwa njia za ushirikina tu hutofika mbali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom