Ushauri mie nipo njia panda

sijajua hapa njiapanda upo wewe au yeye? na njiapanda ya kumsaidia au? kama hajakupa jibu wala usiwaze na huyo tayari akili yake imeeshajichanganya na kukomaa. mshaurini umpeleke akaanze memkwa.
 
duuu dogo kazingua
umenifurahisha ulivyosema ulifunga kiti ya moto inamaana ulienda kula ulipofika home huhuhuuuu ai ungeacha tu daaaa mate yashajaa mdomon
 
mwambie akauze matikiti maji yana pesa nzuri
 

Nakubaliana na hili wazo
 
Maadam kaomba msamaha we msamehe na huyo tayar keshajifunza,ingelikuwa bado angekujibu jeuri,lakini kuonyesha anajuta ndo maana alilia.

Muulize tena anataka nini,akishindwa toa jibu msaidie ajitambue,Tafuta siku ambayo una mood nzur na yeye pia hakikisha yuko njema,muulize hivi ulipokuwa mtoto Kazi gani ulipenda ufanye? Au ulipenda uwe nani? Hivi kazi gani inakukonga moyo wako kiasi kwamba nawe unatamani. Akikupa jibu ndo kianzio hicho mjenge kny hicho anachotaman.
 

Dasi; ameshaanza kujitambua!
Nakushauri usianze kuchukua hatua ya kumwondoa haraka hapo alipo!
Mtathimini kwanza kama kazi hiyo anaimudu na ummpe moyo aendelee kuifanya kwa muda kama 2months ila mtahadharishe na tamaa ya wanaume na kama anashida mweleze milango iko wazi ya wewe kumsaidia.

Huwezi jua-pengine anaweza kuwa Mhudumu mzuri na hapo pakawa mwanzo wa yeye kujitambua na kubadilika kimawazo.
Then shule ya Uhudumu-maisha yanaendelea!
 
jaribuni kumpa elimu ya ujasiriamali then mpeni mtaji afanye biashara


Elimu ya ujasiriamali amekwisha ianza .Mie na hesabu yuko field and then theory-na kwa vile yeye ni slow leaner staili hii ya kufanya kwanza kazi kabla ya kuisomea inamfaa zaidi.
Baada ya kuprove kuwa yuko fiti kuhudumu anafaa wamsogeze level nyingine ya kumanage kijisehemu ndogo ya Biashara kuona kama atamudu kuisimamia-mwosho wa siku kama aprove yuko fiti then 100% anaachiwa kama mtaji wake na maisha yanasonga mbele.Hii ni namna nzuri ya kumsaidia mtu kimaisha.




Cc Dena Amsi
 
Last edited by a moderator:
jaribuni kumpa elimu ya ujasiriamali then mpeni mtaji afanye biashara

Mjasiriamali asiyesoma ndio mjasiriamali wa aina gani? Labda kule uchagani...of course with extra curricular activities people hide behind little groceries as their source of wealthy
 
Mchukue, anahitaji msaada zaidi kutoka kwako
 
Tatizo nduguyo hapendi kusikia kabisa habari za madaftari name kuna kazi chache ambazo haziitaji madaftari!

Hiyo kazi si nzuri kabisa na sidhani kama inaweza kukidhi mahitaji yake name huo ndio mwanzo wa kujiuza.
Hivyo basi sidhani kama utapenda kuona ndugu yako ana hatarisha maisha take.
Muite uongee nae na umwambie afikirie biashara ya kufanya Kama utaweza mjikusanye mmtafutie mtaji aanze biashara au fikiria biashara unayo ona itafaa umwambie afanye!
Maisha mazuri hayapatikani kwenye Elimu tuu japo inasaidia kidogo.
Usimruhusu kuendelea na hiyo kazi.
 
sijajua hapa njiapanda upo wewe au yeye? na njiapanda ya kumsaidia au? kama hajakupa jibu wala usiwaze na huyo tayari akili yake imeeshajichanganya na kukomaa. mshaurini umpeleke akaanze memkwa.

Huyu binti hataki kusoma halafu huko Memkwa ndio atasoma?
Suluhu ni kumtafutia biashara nzuri ya kufanya.
 
Unauliza majibu. Hotel management ndo kozi yake. Unasoma vizuri hakuna kufeli kazi ni za uhakika.
 
Aisee ndo maana nimeomba ushauri nishapata majibu hapa asanteni sana angalau hasira imenipungua na nimeshushia na Zanzi zangu za kutosha maana toka jana sikuwa nimekula na ukizingatia Baba Mkubwa aliniambia before arest in peace 'Nakuachia wadogo watunze uwezavyo usiwaache wahangaike' Haya maneno huniumiza na hujirudia kichwani mwangu na mara nyingi naota naona Baba ananiambia nimewaacha daaahh ngoja nione nitaongea nae kesho
 
Pole, Mi naona mpeleke akasomee mambo ya saluni, customer care, receptionist or mambo ya hoteli, kuna mtu shule ilimshinda alipopelekwa mambo ya hotel aliweza na ana kazi yake now, si unaona hotel nyingi zinahitaji receptionists n.k, nafikiri kazi za aina hiyo zitamvutia. (Cherehani asije akakosea vipimo akaharibu nguo za watu bure, kushona inahitaji watu watulivu na wavumilivu pia, ndugu yako anaonekana ana haraka za maisha hata yaonekana akikaa class anatamani ya nje.).

NB:Usimpeleke ishu za ucashier, kushika hela za watu hata duka la jirani, asije akakuletea matatizo zaidi, mpeleke afanye ishu za kusubiri mshahara wake tu.
 
Akili ni nywele na kila mmoja ana zake!! Kaa nae chini umuilize kwa upendo nini malengo yake kwanza! Akisha jieleza ndo utajua kipi umpe msaada
 
Muite kwa mara nyingine ilimradi ametambua kuwa amekosea baada ya kuona hali ya mtaa ilivyo hana jeuri tena cha msingi kama unaweza ukampatia mtaji basi mpeleke kozi za ujasiriamali baada ya hapo akafanye biashara 😛eep:
 
huyo ktu chochote kinachohusisha kuandika kwenye daftali hawezi..... wakati formal na informal education znahitaji kusoma na kuandika...... hakuna jinsi mwambie achague rahisi kwakwe ipi... no way out...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…