Basi kama ashakuambia awezi kusoma bora ukamsikilza kuliko kumpeleka tena shule na wewe ukawa unaharibu hela yako ya bure,kizuri amekua mkweli kuwa awezi kusoma.
Kama wataka kumsaidia tena kaa naye chini then muulize nikitu gani tofauti ma shule angependa kufanya ambacho anaona kinaweza kumsidia yeye.
Jibu atakalokupa basi na wewe jaribu kuangalia je nikweli linaweza kumsaidia kimaisha but mshauri asikate tamaa tu!!
kuna kazi ambayo wanaipenda sana hawa wasiopenda kusoma. si nyingine bali ni kushona.mpeleke huko kwenye cherehani labda ataweza.
Dada mimi naona mpe uhuru wa kuchagua afanye nini maana amerudia sana hivyo kisaikolojia imemwathiri na sidhani kama atafanya vizuri,mwite kwa upendo kabisa na upole mtoke sehemu nzuri ya kula na kunywa soda na juice mpe pole kwa kujaribu kwake na usimkasirikie baada ya hapo mwambie achague apendacho na mhakikishie kumsupport kama dada yake just show your love to her she will change drastically after all she is just your young sister so show your sister-hood(mwonyeshe upendo wa dada na si ategemee kwa viboyfriend vivalia mlegezo)Nieleweke ni ndugu yangu 'Damu' mtoto wa Baba Mkubwa.
Kamaliza form four mwaka 2010 kafail alipata ziro na 'D' moja tu, 2011 akareseat ndo kavurunda kabisa, 2012 nikamwambia njoo huku nchi jirani nilipo mie akaja akaanza kusoma Diploma ya HR kaharibu mbaya semister ya kwanza kachemsha na vitabia fulani sio vizuri.
Nikamrudisha home nikamwambia chagua usome nini he jibu nililopata nusu nizimie 'Dada mie kusoma siwezi' nikasema wataka nini sasa. Ngoja nifikirie mie haya he kaenda kwa Mdingi wangu ambaye ni Mdogo kwa Baba yake kawashiwa moto hatari kwa ujinga wake na ushauri wa kipumbavu wa marafiki katoroka akaenda kuishi hostel na rafiki anayesoma CBE. Jana nimekwenda mahali kula kiti ya moto mara namuona kabeba tray anakuja kunihudumia mie mdomo wazi. Namuuliza hii ndo kazi uliyotaka kufanya ama?? Anaanza kulia eti dada nisamehe nimekosa pesa ya kula imebidi nifanye hii kazi nisaidie. Mwenzenu mate yalinikauka, maneno yalipotea sikujibu hata neno moja kiti ya moto yenyewe ilikuja nikafunga hata apetite yote iliyeyuka.
Naomba ushauri wenu NIFANYYEJE
Shida hajanipa jibu anataka kufanya nini naona aibu sana ndugu yangu kuuza baa na uwezo wa kumsomesha ninao
Shida hajanipa jibu anataka kufanya nini naona aibu sana ndugu yangu kuuza baa na uwezo wa kumsomesha ninao
dunia mama! chukua ndugu yako nenda naye nyumbani keshajifunza, sasa hivi ukimuuliza unataka nini atakueleza. kuna jirani yetu mmoja wakati sisi tuko wadogo alikuwa na mtoto wa kike, alichetuka hasa mpaka wazazi kumkana, akaondoka nyumbani sijui hata alienda wapi miaka kama miwili, akarejea kuomba radhi kwa wazazi wakakataa, akaenda kupata hifadhi kwa jirani nyumba ya tatu, kwenda kumwombea msamaha kwa wazazi wakakataa tena kwamba wanamfahamu vizuri hajajirudi, yule jirani akaamua kukaa naye. dada wa watu kaanza kusoma elimu ya watu wazima "taasisi", siku moja akakutana na mama yake njiani amevaa uniform!!...mama wa watu alilia sana, wakamchukua akaendelea na shule, leo hii ni mwalimu, ameolewa ana familia!!
Yaani wewe una kesi ya kujibu ila nimekusamehe sababu hasira niliyo nayo kwa huyu ni kubwa kuliko
Dada mimi naona mpe uhuru wa kuchagua afanye nini maana amerudia sana hivyo kisaikolojia imemwathiri na sidhani kama atafanya vizuri,mwite kwa upendo kabisa na upole mtoke sehemu nzuri ya kula na kunywa soda na juice mpe pole kwa kujaribu kwake na usimkasirikie baada ya hapo mwambie achague apendacho na mhakikishie kumsupport kama dada yake just show your love to her she will change drastically after all she is just your young sister so show your sister-hood(mwonyeshe upendo wa dada na si ategemee kwa viboyfriend vivalia mlegezo)